G-Mdadisi
Senior Member
- Feb 15, 2018
- 157
- 99
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Salama Mbarouk Khatib ameagiza kurejeshwa wizarani wafanyakazi watatu wa baraza la Mji Wete baada kushindwa kutekeleza maagizo ya Serikali ya kuifanyia matengenezo ya dharura barabara ya ndani unayounganisha wananchi wa shehia ya Utaani iliyokatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Agizo la kuifanyia matengenezo barabara hiyo limetolewa mapema asubuhi tarehe 22/4/ 2021 lakini hadi inafika saa kumi jioni hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ambapo Mkuu wa Mkoa anafika katika eneo hilo na kutoa agizo.
Mkuu wa wilaya ya Wete Mgeni Khatib Yahya amesema kushindwa kufanyiwa kazi agizo lake ni utovu wa nidhamu huku Mkurugenzi wa Baraza la Mji naye akazungumza.
Nao baadhi ya wananchi wanaotumia barabara hiyo wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuifanyia matengezo kwani ndio wanayotumia kufuata mahitaji yao.
Abushir Khamis yeye ni injinia ya baraza hilo, na hichi ndicho kilichomkuta.