RC Kafulila: Tanzania gharama za umeme ni ndogo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,061
2,000
Mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila, amesema licha ya kuwapo kwa baadhi ya changamoto ya utoaji wa huduma za umeme, lakini Tanzania ni nchi pekee katika mataifa ya pembe ya Afrika Mashariki yenye gharama ndogo zaidi ya tozo za umeme, ikilinganishwa na nchi nyingine za ukanda za huo.

Hayo ameyasema katika mkutano wake wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero zinazowazonga wananchi, uliofanyika Stendi ya zamani ya mabasi mjini Bariadi mkoani humo, ambapo amesema Tanzania pia inaongoza kwenye ukanda wa nchi za Afrika Mashariki kwa kufikisha umeme katika maeneo ya pembezoni.

Aidha, RC Kafulila akatumia nafasi hiyo kutoa siku 60 kwa taasisi za umma mkoani humo kuondoka kwenye majengo ya kupanga na kuelekea Nyaumata, ili kuiondolea serikali mzigo wa kodi.

Chanzo: EATV
 

MC44

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
2,109
2,000
Kwa hiyo hata hiyo nyerere dam ikikamilika bado umeme hautashuka?
wanatuandaa kiakili hawa
 

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
5,564
2,000
Hii tabia ya kusema au kulinganisha hali ya nchi yako na nyingine haipaswi kufanywa kwa kukurupuka
Lazima tatizo kama lipo basi litatuliwe sio kuanza kulinganisha na nchi tafauti
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom