RC Homera atoa maamuzi kumaliza mgomo wa daladala na bajaj Mbeya

MPUNGA MMOJA

JF-Expert Member
May 30, 2015
294
500
Baadhi ya Mazimio ya kikao cha pamoja RC Homera na Wamiliki wa Daladala,Bajaj na Wadau wa Usafirishaji Mbeya.

~ Bajaj mwisho kupakia watu 3
~ Bajaj haziruhusiwi kuchukua abiria njiani
~ Ndani ya siku 14 Madereva Bajaj/Daladala na Tax wote wawe na leseni hai
~ katika sheria hakuna sehemu inatambua Bajaj ni Daladala bali ni usafiri wa kukodi.

Sheria za SUMATRA hazitambui kama Bajaj ni Daladala bali ni chombo cha kukodi.
 

Pine Valley

JF-Expert Member
Nov 30, 2020
957
1,000
Ujinga Tu , haya majitu yanayomiliki Hiace yanaona yanahaki kumiliki routes , idiots
 

Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
2,774
2,000
Hii ngoma bado mbichi. This isn't permanent solution. Tengenezeni barabara zinazotoka nje ya jiji,tatizo la jiji la Mbeya halina barabara za mitaa hasa kata za pembezoni

Mipango mji wa Mbeya jiji na Sumatra na wenye mamlaka acheni uvivu wa kufikiria,chezesheni akili zenu mtuletee ufumbuzi wa kudumu kwa tatizo hilo!

Kama mnashindwa njoeni Pm tuwafundishe namna ya kuifanya Mbeya iwe ya kisasa.

Kero nauli kutoka Sai-Simike 800,nsalaga-stand kuu 400,igawilo standkuu 500,nanenane-kadege 800,Mama john-kadege 800,mama joni-standkuu 400,Igawilo-mbalizi 800,Ilomba -Simike 800😲😲🤔

Abiria nasisi tuitishe mgomo wetu huenda tukasikilizwa.
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,575
2,000
Hilo si suluhu sahihi. Japo Bajaji wanapata ugali wao lakini hazipaswi kupita barabara kuu. Kama walitoa hiace barabara kuu wanabakizaje Bajaji? Tunaenda nyuma kwa kufanya maamuzi ili tupendwe. Na ndiyo ubaya wa demokrasia. Miaka michache baadaye hizo Costa zitapotea na usafiri wa Umma utatakuwa ni bajaji na Yebo yebo.
 

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,925
2,000
Daladala, Bajaji, Bodaboda zote ziwepo halafu abiri ndio achague apande nini.

ABIRIA ndio bosi yeye ndio ataamua apande nini. Hili ni soko huria.
 

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
2,798
2,000
Baadhi ya Mazimio ya kikao cha pamoja RC Homera na Wamiliki wa Daladala,Bajaj na Wadau wa Usafirishaji Mbeya.

~Bajaj mwisho kupakia watu 3
~Bajaj haziruhusiwi kuchukua abiria njiani
~Ndani ya siku 14 Madereva Bajaj/Daladala na Tax wote wawe na leseni hai
~katika sheria hakuna sehemu inatambua Bajaj ni Daladala bali ni usafiri wa kukodi

Sheria za SUMATRA hazitambui kama Bajaj ni Daladala bali ni chombo cha kukodi
Wenda mkuu wa mkoa mbeya mpya ameongea vizuri this week nilikua mbeya, na Niko njiani elekea sehem nyingine tafuta ugali wa wafamilia chini ya ratiba ya wanaonipa ugali but

1. Wananchi wa Mbeya kwa kweli wamepata tabu Sana ,hasa wanafunzi ,watumishi kuanzia jtatu ya week hii,

2 ,KWA mda mchache nimekaa Mbeya swala hili la bajaji na daladala sio dogo maana wamiliki hasa wa bajaji ni viongozi wakubwa kuanzia wakuu wa vyombo muhim, usishangae hata aliekua mkuu wa mkoa mh CHALAMILA kua na bajaji zake hapa, japo sio dhambi ila mbaya zaidi hata registration za bajaji mkoa huu hazina limit ,jana naambiwa ziko bajaji elfu sita na zaidi,njia moja na daladala
MWISHO.

MKUU WA MKOA MPYA ,tumia akili kubwa KWA hili vinginevyo utafanyiwa hujuma , na kulogwa ukienda kichwa kichwa ,mtandao wa bajaji ni mpana Sana mkuu
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,328
2,000
Wenda mkuu wa mkoa mbeya mpya ameongea vizuri this week nilikua mbeya, na Niko njiani elekea sehem nyingine tafuta ugali wa wafamilia chini ya ratiba ya wanaonipa ugali but...
Ngoma ngumu hii, hata Tulia Akson yuko nyuma ya bajaji bila shaka.
 

Hawaki

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
642
1,000
Cha kufanya kwanza, ni kuzitambua daladala na bajaj kama vyombo halali vya usafiri na pili, VYOTE vilipe KODI na TOZO sawa bila kujali ukubwa wa chombo chake. Mwenye kuweza awepo barabarani na mwenye kushindwa aondoke. Tatu, wote watoze nauli sawa. Nne, wote watoe ticket kwa abiria (ikibidi efd). Tano, kila bajaj ipewe route moja tu kama daladala. Sita, kila route iwe na rangi sawa na daladala. Masharti haya yazihusu bajaji zinazoenda maeneo yasiyo na route au za kukodi tu.
Hapo hakuna upendeleo hivyo atakayelalamika ni mkorofi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom