RC Gambo, kumbe ulikasirika kweli?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Nilipokutana nawe juzi Arusha, tulizungumza mengi. Mojawapo ni juu ya msiba mzito uliowakumba CHADEMA wa Hayati Ndesamburo. Tukazungumza na kuteta mengi: ya kichama na kiserikali. Nikakutania kuwa wana-Kilimanjaro wanaogopa ushiriki wako msibani kwa Ndesamburo kwakuwa 'wanalinda' rambirambi zao.

Ukatabasamu kiaina. Tulipoendelea kupiga soga, nikaanza kushikwa woga. Ukawa hujibu kama mwanzo. Ukawa unaitika kwa kichwa na kuguna tu. Ukawa unaniacha hadi nasema peke yangu kwa muda mwingi. Ukawa unahamisha mada kwa 'lazima' ili tuzungumzie 'mafanikio' yako hapo Arusha. Mwishoni tukaagana.

Nilikuaga kuwa nakuja hapa Moshi kushiriki maombolezo na mazishi ya kaka yangu, mtani wangu kisiasa na mwanamaendeleo Philemon Ndesamburo. Ukaahidi kuwa ungekuja au kutuma Mwakilishi kwa shughuli ya kuaga jana. Hukufanya hivyo. Hukutokea wala kusikika hata kupitia Mwakilishi. Ndiyo mambo ya 'kutoshirikishwa'? Kumbe ulikasirika?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa msibani Moshi, Kilimanjaro)
 
Bora hakuja.Tena Rafiki angalia huyo ni kati ya wale watoto wapendwa wasio guswa asije akakupoteza ukakosa ugali wako
 
Umeshajulikana wewe ni nani Vuta Nkuvute. Mimi naona kama vipi wewe fanya kama Paskali utumie jina halisi ili wote tukujue.
 
Back
Top Bottom