RC Gambo aumbuka. Vijana wa CCM Arusha wamshambulia mitandaoni, aamua “ku left “

Ndiyo umetoka kijijini kwenu juzi 3.6 unaanza na posho ya kujikimu ya buku 7
Lema ana hofu ya kila kitu..wale aliokua anaitana nao Makamanda wamemgeuka....sizani hata kama anatamani kugombea kwa kuhofia aibu.
 
Kwa ninavyojua huu utenguzi unaweza kuwa nimoja yatenguzi zilizofanyiwa tafiti za kutosha be4.

Kati ya yote yaliyoletwa na mleta uzi! Kuna hoja kuu mbili zaweza kuwa zimeperekea utenguzi huu.
1.kuwakumbatia wakwepa kodi kwa kuwaita wadau.
Sababu mpaka mda huu kuna aliyekuwa anajiita muwekezaji wa tanzanite one yupo ndani mpaka sasa.

Nahuyu alikuwa akiitwa mdau mkuu wa serikari kiasi cha kumzuia afisa madini wa kufika kwenye eneo lake nakutaka kumshitaki kwa rushwa labda anahusika na gambo.

2. Gambo na mkuu wa wilaya na madeni kwa maana ya mkurugenzi wa jiji wte walikuwa wababe. Hivyo wasingeweza kufanya kazi.

4. Kuna aliye wachoma! Eiza kati yao au wapembeni yao.

Tukutane j3. Mzee wa sifichagi ataliweka wazi wakati akiapisha.
Mkumbuke itakuwa saa2:30

Najua tv zte zitaungana natukio hili kuliko matukio yyte.
 
Rc Gambo aumbuka,vijana wa Ccm Arusha wamshambulia mitandaoni aamua “kuleft”.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo amejikuta akiumbuka katika mitandao ya kijamii hali iliyomlazimu kujiondoa huku baadhi ya vijana wa Ccm Arusha wakimshauri aache jeuri na awe karibu na vijana.

Tukio hilo lilitokea jana usiku katika kundi la Whatsapp la Arusha Youth Forum ambapo Gambo alijikuta akishambuliwa na baadhi ya vijana wa Ccm Arusha baada ya kuandika maneno kwamba “some people are stupid but lucky”akimaanisha “baadhi ya watu ni wajinga lakini wana bahati “.

Mara baada ya kuandika maneno hayo ndipo makada hao walipoanza kumshambulia huku wakimwambia ya kwamba yeye kama mkuu wa mkoa hajawahi kusaidia vijana Arusha na amewatenga.

Jimmy Pamba alikuwa kijana wa kwanza kumshukia Gambo huku akimweleza kwamba amekuwa mtu wa kujikweza na kupenda kutukuzwa.

Kabla hajajibu kijana mwingine Lucas Ngokolo aliibuka na kumwambia kwamba atamke hadharani kijana aliyemsaidia huku akimwambia kwamba amekuwa kikwazo katika mapambano ya kukusanya kodi kwani amekuwa karibu na wakwepaji kodi mbalimbali na mara nyingine huwaita wadau.

Kada huyo bila kupepesa macho alimwambia Gambo hafai kuwa kiongozi wa mkoa wa Arusha kwa kuwa amekuwa akikwaruzana na kila kiongozi anayeletwa Arusha kama wakurugenzi na wakuu wa wilaya.

Hivi karibuni katika kikao cha kuvunja baraza la madiwani Arusha Gambo aliwatuhumu mkuu wa wilaya Arusha,Gabriel Daqaro na mkurugenzi wa jiji,Dk Maulid Madeni kwamba wanamkwamisha katika utendaji wake wa kazi.

Pia itakumbukwa ya kwamba Gambo aliyewahi kukwaruzana na mkuu wa mkoa wa Arusha, Daud Ntinbenda wakati akiwa mkuu wa wilaya mpaka akaondolewa, mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti wakati akiwa mkuu wa wilaya ya Arumeru.

Hata hivyo, muda mfupi baadae aliibuka kijana aitwaye Bernad Trump ambapo alimchana na kuelezea tukio la kumweka katika mahabusu ya kituo cha polisi cha kati Arusha kwa siku tisa bila dhamana.

Trump alimwambia Gambo kwamba amekuwa akitumia mamlaka yake vibaya kuwaumiza baadhi ya watu wanaomkosoa huku akisisitiza kwamba hafai hata kuwa mbunge wa Arusha Mjini.

Akijibu mashambulizi Gambo alidai kwamba pamoja na jitihada za kuifuta Chadema Arusha kuna muda alikuwa akiishi maisha ya hofu kwani alivamiwa nyumbani kwake Muriet mara mbili na wafuasi wa Ccm kama hasira za kuifuta Chadema.

Gambo alizungumzia kwamba kila jambo baya amekuwa akisukumiwa yeye kama hatua ya mfanyabiashara maarufu Philemon Mollel “Monaban” aliponyang’anywa kiwanda cha NMC watu walipotosha kwamba yeye ndio alichangia.

Gambo alijitetea kwamba hata wakili maarufu, Albert Msando alipokamatwa na kuwekwa mahabusu Polisi kati kwa kutoa kauli kuhusu masuala ya korona watu hao hao walidai ni yeye aliamuru.

Hata hivyo, pamoja na majibu hayo Baadhi ya makada waliendelea kumshambulia kwa kumuita mnafiki na anayependa kujisikia na ndipo alipoomba kujiondoa katika kundi hilo la Whatsapp.

Gambo ni miongoni mwa watu wanaotajwa kulimezea mate jimbo la Arusha Mjini lakini amekuwa akikumbana na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya makada na viongozi wa Ccm Arusha.

Wengine wanaotajwa ni pamoja na Meya aliyejiuzulu, Calist Lazaro, mfanyabiashara maarufu, Phillemon Mollel maarufu kama Monaban, Dk Batilda Burian, Wakili Albert Msando, Edmund Mgemela, Mustapha Panju, Thomas Munisi na wengine kadhalika ambapo kwa upande wa Chadema mpaka sasa ni Godbless Lema.

Soma pia > Mrisho Gambo: UVCCM kumejaa vijana wanafiki ambao wakizeeka watakuwa Wachawi!
UTEUZI WA RC ARUSHA NA DC ARUSHA WATENGULIA

Rais Magufuli, leo ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta

Pia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro na nafasi yake imechukuliwa na Kenan Kihongosi wa UVCCM Iringa

Aidha, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni na kumteua Dkt. John Pima kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri

#JFLeo #Magufuli
View attachment 1483586

Soma pia:

1) Arusha: RC Gambo aibua sintofahamu Soko la Samunge, abeza taarifa ya DC na Mkurugenzi

2) Nini tatizo la RC Mrisho Gambo na wasaidizi wake?

3) Ugomvi baina ya RC Gambo na Mkurugenzi wa Jiji Arusha lashika kasi

4) RC Gambo aumbuka vijana wa CCM Arusha wamshambulia mitandaoni, aamua “ku left “

5) Ntibenda: Kama kuondolewa kwangu kama RC Arusha kuna mkono wa mtu; Mungu atalipa
Duh...!.
Kuna kitu niliwahi kushauri kumhusu Mrisho Gambo.
Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako linahitajika
P
 
Sijawahi kuingiliana wala kukutana na Gambo kwenye suala lolote ila nimefurahi mnoo.Bado Hapi ,afuate Komanya mwisho Konda boi .
 
Hili la kuwafunga viongozi wenzake analipenda, naona limeanza kumtudi maana hata huko alikotoka Uvinza, Kigoma alikokuwa mkuu wa Wilaya alkuwa akiwaweka ndani watumishi.
 
Back
Top Bottom