RC Gambo aagiza kamera za CCTV kufungwa vituo vya utalii kudhibiti Trafiki wala rushwa

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo ameagiza kufungwa kamera za usalama (CCTV )katika vituo maalumu vinne vya ukaguzi wa magari ya kusafirisha watalii ili kudhibiti matukio ya rushwa yanayojitokeza wakati wa ukaguzi.

Gambo ameeleza hayo wakati akizungumza na askari wa jeshi la Polisi Mkoani hapa, wakiwemo wa usalama barabarani katika hafla ya kutunuku zawadi askari waliofanikisha kukamata Madini yaliyokuwa yakitoroshwa katika mpaka wa Namanga.

Amesema kuwa vituo hivyo vimewekwa katika maeneo ya Kikatiti,Engikareti, Makuyuni na Karatu ,vitalenga kukagua magari yanayosafirisha watalii ,ukaguzi wa vileo kwa madereva pamoja na usalama wa magari.

Amesema kuwa kufungwa kwa kamera hizo kwenye vituo vya ukaguzi wa magari ya utalii ni kutasaidia kuondoa utata kwa baadhi ya matukio yakiwemo ya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa askari wa usalama barabarani.

"Msimamo wa mkoa ni kuhakikisha watalii wetu hawabughudhiwi na Trafiki kwa kuwa wanachangia kipato kikubwa kwa mkoa wa Arusha ambapo mkoa wa Arusha unachangia asilimia 86 ya pato la taifa" Alisema Gambo

Amesema vituo hivyo vimeanzishwa maalumu ili kuondoa usumbufu uliokuwepo wa magari hayo kusimamishwa mara kwa mara na Trafiki barabarani jambo ambalo limekuwa likisababisha usumbufu kwa watalii ambao huliingizia pato taifa kupitia utalii wao.



IMG_20190816_112257.jpeg
 
Zitatimiza nia ikiwa tu panapotokea ripoti ya rushwa footage inaangaliwa kupata ushahidi wa tuhuma.
 
Amesema kuwa kufungwa kwa kamera hizo kwenye vituo vya ukaguzi wa magari ya utalii ni kutasaidia kuondoa utata kwa baadhi ya matukio yakiwemo ya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa askari wa usalama barabarani.


Gambo hii itasaidia sana kupunguza tatizo la rushwa, lakini ni vituo vyote vya ukaguzi vifungwe hizo cctv kukomesha rushwa zinazopelekea baadhi ya ajali zinazosababishwa na ukaguzi usiofanyika kwasababu wakaguzi wanakuwa wapewa hongo
 
Back
Top Bottom