RC, DC watishwa kuuawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RC, DC watishwa kuuawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 30, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Monday, May 30, 2011, 5:45  • Ni Mkuu wa Mkoa Pwani na DC Bagamoyo
  • Wanatishwa na watumishi waliosimamishwa

  Na Gustaphu Haule, Kibaha
  [​IMG]

  MKUU wa Mkoa wa Pwani, Amina Said, juzi alitokwa na machozi akiiomba Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhakikisha inaokoa maisha ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Magesa Mulongo.

  Alisema Mulongo anatishwa kuuawa na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo waliosimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

  Pinda aliwasimamisha kazi baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mwanzoni mwaka jana akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Rhoda Nsemwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi zaidi ya Sh milioni 900.

  Amina aliiambia kamati hiyo kuwa hata yeye kwa sasa yupo hatarini kuuawa kutokana na kile kinachodaiwa kuwa baadhi ya watendaji hao wamekuwa wakitoa matamshi ya kumkashifu kwa kumuita ‘kimbelembele’.

  Hali ya Halmashauri ya Bagamoyo bado ni mbaya kwani DC amejaribu kufanya kila jitihada kuiokoa Halmashauri hiyo lakini ameshindwa, alisema.

  Alisema wapo baadhi ya vigogo wanaochezea akili yake.
  Mkuu wa mkoa alisema natambua kuwa Halmashauri ya Bagamoyo ina upungufu mwingi hususan katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

  Alisema ndiyo sasa anafanya jitihada za kuhakikisha hali hiyo inakomeshwa lakini kinachoshangaza ni kuona ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akiendelea kutoa hatia safi katika halmashauri hiyo.

  Mara nyingi amekuwa akipingana na Tamisemi kuhusu taarifa zinazoandaliwa na ofisi yake, alisema.
  Alisema kila taarifa inayotolewa na ofisi yake Tamisemi imekuwa ikiikataa hivyo haoni sababu ya kuendelea kushughulikia suala hilo.

  “Kwa kweli mimi nimeshindwa kutatua hili la Bagamoyo kwani kila ninachokifanya Tamisemi na CAG wanakataa na badala yake watu wanatuwinda mimi na Mkuu wa Wilaya kwa kutuambia tunafuatilia mambo yasiyotuhusu huku tukitishiwa kuuawa,”alisema na kuongeza:

  “Naiomba kamati hii ya bunge niivulie mzigo huu itafute njia mbadala ya kusalimisha maisha yangu na ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kinyume na hapo siku yoyote nikipoteza maisha msishangae.’

  Alisema jambo linalosikitisha zaidi ni kuona baadhi ya watendaji waliosimamishwa kazi wakiendelea kuishi katika nyumba za watumishi huku serikali ikiendelea kulipa gharama kubwa na kumuacha
  Mkurugenzi wa sasa Samwel Sarianga akiendelea kupanga katika nyumba za kulala wageni.

  “Hili ni jambo la utata kwa sababu tangu Mkurugenzi mpya aje kufanya kazi katika Halmashauri ya Bagamoyo hadi sasa anaishi kwa kupanga katika nyumba za kulala wageni.

  ‘Badala yake nyumba aliyotakiwa kuishi anaishi mtu ambaye tayari alisimamishwa huku serikali nayo inaendelea kulipa gharama,” alisema.

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Idd Azzan,alisema kamati yake haijafurahishwa na matumizi ya fedha katika wilaya hiyo.

  Alisema kamati imegundua mvutano kati ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Tamisemi na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali.

  Aliitaka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuhakikisha inafuatilia kwa karibu nyaraka zote za halmashauri hiyo ambazo zimedaiwa zimepotea na kama hazijapatikana wahusika wachukuliwe hatua.

  Hata hivyo, alisema hatua ya Mkurugenzi aliyesimamishwa kuendelea kulipiwa fedha na serikali na kumuacha yule wa sasa akiendelea kuishi katika nyumba za kulala wageni ni ubadhirifu wa fedha za umma.
   
 2. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,083
  Likes Received: 1,729
  Trophy Points: 280
  Mashushushu wanafanya nini hata DC alilie msaada kutoka nguvu ya umma? Ama kweli mafisadi wameteka hata dola letu la uswahilini.
  wakhtanabahu:pound:
   
 3. T

  Twasila JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,913
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Rc hajui haki za watumishi?! Ded hajafukuzwa. Huyu rc hata angewekwa darasani mwaka mzima itakuwa sawa na kumpigia mbuzi gltaa. Hii inaonyesha rc na dc wake ni vipofu na viziwi. Kawa wao wanalalamika, itakuwaje kwa mtendaji wa kijiji? Safari kwa tz kupata maendeleo iko mbali sana!!
   
 4. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii inawezekanaje nyumbani kwa Mh. Rais? Hawa wanafanya utani. Namwomba Mh Rais atoe maelekezo mara moja.
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Nadhani mwajiri wa DC na RC awatafutie kituo kingine cha kazi au aina nyingine ya kazi, kazi hii imewashinda,
   
 6. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Hayo ndiyo ni matokeo ya kuteua kwa kuangalia udini au jinsia pekee bila kujali elimu. Inaonekana hawajui utaratibu wowote! Cheers to CCM and JK
   
Loading...