Kuwatisha walimu, kuwaagiza maafisa elimu na Dc kwenda kufundisha ni kupoteza muda wa kutatua tatizo. Suluhu ya mgogoro wa walimu ni serikali ikubali kukaa na walimu ili kukubaliana kwa kile kinachowezekana na siyo vitisho kama wanavyofanya sasa. Wilaya moja ina Dc na afisa elimu wangapi? Je shule, madarasa na masomo yako mangapi, je Dc au afisa elimu atamudu? Au ni kupoteza muda tu. Kama hawa ndiyo viongozi tulio nao kazi tunayo. Maana yawezekana hapo ndiyo uwezo wao wa kufikiri unapoishia. Pole kwa watanzania.