RC Dar Es Salaam amepokea magari 17 kati ya 28 ya Jeshi la Polisi yaliyokuwa yakifanyiwa maboresho Moshi

Jamani dogo Bashite anamipango.
So far ninekuja gundua huyu dogo ni
1. Futurist
2. Strategist
3. Na influential pia
I wonder amefanya manuva gani mpaka kuweza kumuinfluence mkuu.
Na wasiwasi atahii issue ya Madini kabla haijalipuka yeye ndio aliiandaa
 
Watetea mafisadi chadema, ni matumbo joto
wana lumumba bana hivi tangu lini ccm iliwahi kamata mafisadi haiwezi sababu ufisadi mwingi sana unafanywa na ccm na mafisadi woote chimbuko lao ni ccm mahaama ya ufisadi saa hizi nahisi wanafugia kitimoto
 
mmeamua kuzuga baada ya mpango wenu wa nairobi kuumbuliwa eeh...
Mnaaminishwa kila kitu kama hamtumii zenu vile!.
Ndio walewale waliominishwa ushindi utapatikana nne asubui, haukuja!. Mkaambiwa kuna vijana wametumwa Ulaya, ICJ wanakuja na barua kuzuia kidume kisiapishwe, mkaamini tena! Mkaambiwa Makinikia tunaburuzwa mahakamani na tutanyolewa na kwa chupa, mkaamini tena na mkakata mauno ya kufa mtu kwa furaha, haijawa!!! Mnakoelekea mtaaminishwa 2020 mambo yatakuwa safi.
 
Msaada,kiutaratibu,anaomba mwenye mali, kama ni mkataba wa kukarabati magari basi unasainiwa na mwenye Mali(wizara ya mambo ya ndani/IGP na anayekarabati magari,inafahamika kwamba mwisho wa siku kuna legal implications kwa lolote baya litakalotokea hata kama amekarabati kwa msaada

Mkuu wa mkoa hawezi kusaini mkataba huo kwa kuwa si mmiliki wa mali, katibu utawala mkoa hawezi kusaini kwa kuwa si mmiliki,

Na hata kama ni msaada,mkuu wa mkoa anawasilisha proposal ya msaada huo ofisi ya mkuu wake(Tamisemi)wanamwarifu waziri mkuu,waziri mkuu anatoa maelekezo kwa wizara husika,ni msaada kwa serikali,ownership ya msaada huo,ukishaingia katika mchakato wa kiserikali ili uwe vetted,ukipitishwa basi unakuwa msaada kwa serikali,na kwa maana hiyo,ni msaada kwa wizara ya mambo ya ndani ambayo kimajukumi ndio mmiliki wa mali za jeshi la polisi,

Registry ya magari ya polisi yote Tanzania,pamoja na mahali pengine,iko wizara ya mambo ya ndani chini ya katibu mkuu na IGP

Ndio maana bungeni kama jeshi la polisi lina upungufu wa magari au magari mabovu sehemu fulani,maswali huelekezwa kwa waziri wa mambo ya ndani,sio waziri wa tamisemi
Gari zote za serikali ziko chini ya kitengo kimoja tu, wizara ni watumiaji tu.
 
Mwisho wa siku, je alichofanya ni sahihi ama bora angeyaacha yaoze???
 
Ni mwenyekiti tu! Lakini unajua kwamba hata mali za ofisi ya mkuu wa mkoa haziko chini yake bali ziko chini ya katibu tawala wa mkoa?

Unajua ndani ya kamati ya ulinzi na usalama kuna jeshi la wananchi,jwtz,lina magari na mali mbalimbali,unadhani huyo mwenyekiti anaweza kuchukua magari ya jeshi na kuyafanya anavyotaka bila ruksa ya wizara ya ulinzi na mkuu wa majeshi?

Ndani ya kamati ya ulinzi na usalama mkoa kuna idara ya usalama wa taifa,iko chini ya ofisi ya rais,utawala bora

Kuna Uhamiaji,iko Wizara ya mambo ya ndani

Yeye ana coordinate tu na kuunganisha lakini hakuna lolote analofanya kwa kuwa commanding ya idara hizo iko kisheria,

Hata Mali hizo zikiharibika,mfano za jeshi la polisi,la wananchi,usalama wa taifa,Uhamiaji,watu hao wanawajibika kwenye ofisi zilizowaajiri,kwenye ofisi zinazomiliki Mali na si ofisi ya mkuu wa mkoa

Mkuu wa mkoa hana mamlaka ya kumfukuza kazi hata dereva wake au mfagia ofisi

Mali aliyoingia nayo ni kale ka ilani ka ccm tu!
Mh nashukuru sana umemaliza kila kitu.
 
we live in a country subjugated by hypocritical misogynists;mie nilitegemea atafufua magari ya wagonjwa(ambulances),magari ya kuzoa taka,atasimamia kuona mkoa wangu una public open space kwa watu kwenda kujipumzisha,public toilets,barabara safi na zenye address(maana noe ni vigumu mno kumwelekeza mtu kwako bila ya kutumia land marks kama shule,)magari haya ya polisi mimi ningekuwa natoa leseni yake yasingepata sio salama kwa watumiaji wake ,yako wazi mno kule nyuma .kama kawaida tunaishi nchi ya kusadikika.
 
mzee7 post: 24085775 said:
Anasema hela zilizotumika kukarabati magari ya polisi si za serikali, je ni za nani? na je kwanini hawajatangazwa? Na je udhibiti wa pesa hizo zinadhibitiwa na idara gani? ikiwa yeye mwenyewe mkuu wa mkoa je kuna pesa ngapi anapewa kinyemela ambazo anazifahamu mwenyewe tu!
Wewe hojayao ipi hapo
 
Hakuna gari lililotengenezwa huko Moshi. Magari yote yalisafirishwa kutoka Mikoa mbalimbali na kupelekwa Moshi ionekane yalikuwa yanatengenezwa kumbe kanyaboya tu.

Watanzania kwa sasa ni waelewa sana hatudanganyiki na hizi siasa za maji taka. Kwa taarifa yako magari yenyewe yalisafirishwa kama ifuatavyo;

Kigoma magari 2
Moshi penyewe magari 3
Dar - es - Salaam Magari 7
Arusha magari 2
Mwanza magari 3
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom