RC Chalamila: Hatuwezi kuzuia bajaji kutumia barabara Kuu Mbeya

Anatania huyu. Mabasi mangapi ya jeshi, police na Magereza yatasomba Wanambeya zaidi ya 1 million....!!?
 
Kuna viongozi wengine wa kisiasa ni wapumbavu sana, unadhani unaweza kucommand jeshi hivyo hovyo tu, ayaingize basi tuone, na wewe mleta mada unashabikia upumbavu kama huu hadi kuanzisha thread na wewe uache ukunduma
 
Zero brain. Haya mabasi ya majeshi yako idle, yamepaki tu na hayana kazi yoyote? Kilangila.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya mh. Chalamila amesema hatasita kuingiza barabarani mabasi ya JW, Polisi, Zimamoto, Mahakama na Magereza kubeba abiria endapo daladala zitaendelea na mgomo.

Chanzo: ITV habari

My take; RC Chalamila ana mamlaka hayo?

Maendeleo hayana vyama!
 

Attachments

  • Umekabidhi ubongo wako kwa.....docx
    393.7 KB · Views: 9
Wenye magari wanateseka Sana mbeya.

Bajaji hazina madereva.

Zina wajinga fulani wanaojua kunyoosha tu barabarani.

Sheria za barabara hawajui Wala hata leseni hawana.

Wenye magari yanachubuliwa Sana na bajaji.

Hawa wangekuwa feeders wa barabara kuu.

Za huko pembeni ziboreshwe ili wapeleke abiria majumbani kwao.
 
RC chalamila hatumii akili anaropoka tu kwakuwa yeye, maaskari, mwamnyange na wengine serikalini ndio wamiliki wa bajaji wakiwemo wana jeshi wanaotumia vibaya nafasi walizo nazo.

Wenye daladala wanalipa kodi nyingi, TRA, LATRA, Ushuru wakati bajaji hawalipi hizo hasa hiyo sticker ya LATRA.

Vile vile bajaji wanaendesha rough barabarani na wamekuwa ndio wasababishaji wa ajali na ajali zikitokea faini anapigwa mwenye daladala kwa kuwa mwenye bajaji ni mwanajeshi, au bajaji ya mwamnyange au ya chalamila mwenyewe.

Bajaji hawana vituo rasmi wao wana simama na kupakia popote amabapo ni hatari huku ukizingatia udereva kenge wao+rough driving)

Bajaji zimekuwa kero mjini kwasababu hawafuati wala kuzingatia usalama barabarani kwenye zebra hawasimami hatakama kuna wenda kwa miguu wapo, bajaji wao wanachomekea tu kwasababu udereva wao ni wa kenge.

Bajaji ndio zimekuwa chanzo cha foleni mbeya mjini kitu ambacho kina didimiza uchumi na ustawi wa jiji kwasababu watu wanachelewa kazini nk

Bajaji wengi kuanzia madereva hadi mabosi zao wengi wamefoji kuanzia license hadi sticker kitu ambacho kinaipunguzia mapato serikali.

Bajaji zitumike kutanua jiji badala ya kubanana mjini. Bajaji zifanye safari za pembezoni mwa jiji mfano uyole - isyesye, ilomba - isyesye, mwanjelwa - ilemi iyunga - must n.k. ili daladala tuziache high way hii itasaidia kupunguza kero zote za bajaji hapo juu.

Chalamila jifunze kuzungumza kwa staha na kwa amri hiyo ni Biashara ya watu, hao ndio wawekezaji wenyewe uwekezaji sio hadi atoke nje au ajenge kiwanja.

Bajaji zitumike kupanua jiji liwe kama dar sio jiji limejibana kisa watu wanaogopa kwenda kufanya biashara nje ya jiji kwa kuhofia changamoto ya usafiri.

Otherwise Sumatra mu assign route mpya za daladala au LATRA na TRA muondoe kodi katika daladala au takukuru na vyombo vingine vya usalama wafanye kazi ya ziada kitu ambacho hawakiwezi kwasababu wao ndio wamiliki na ndio wanaongoza kumiliki bajaji jijini mbeya.

Acheni kufanya siasa kwenye uchumi.
 
Kwa hili naungana na mkuu wa mkoa ningeshanga sana kama angekubali wazo la hao madereva wa daladala la kuziondia bajaji njia kuu.

Shida ya daladala za Mbeya ni moja wao hawajali muda wanachoangalia ni kujaza watu kwenye daladala hata kama watasimama kituoni saa nzima, unakuta daladala inatoka Nsalaga inakwenda Mbalizi inafika Kabwe inakaa nusu saa mzima na abiria inao wakutosha ila inataka kusimamisha wakati huohuo kuna abiria anatoka Kabwe anakwenda Iyunga lakini anaopt kupanda bajaji ya 500 na kuacha kupanda daladala ya Mbalizi ya sh. 400 hapo ndipo waelewe tatizo lipo wapi.

Tatizo ni tamaa zao hao madereva wa daladala, bajaji hawana tatizo tena abiria wanawapenda sana kwa kuwa wanaokoa muda sana. Daladala yawapasa wawe wabunifu kama walivyoshauriwa na mkuu wa mkoa sio kulalamika lalamika. Biashara huria inahitaji akili nyingi sana ikiwa wewe bei yako ya chini lakini bado watu wanafuata cha bei ya juu ujue unashida mahali. Hongera mkuu wa mkuu kamatia hapohapo.
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya mh. Chalamila amesema hatasita kuingiza barabarani mabasi ya JW, Polisi, Zimamoto, Mahakama na Magereza kubeba abiria endapo daladala zitaendelea na mgomo.

Chanzo: ITV habari

My take; RC Chalamila ana mamlaka hayo?

Maendeleo hayana vyama!
Swali ni je yatakidhi mahitaji?
 
Bwashee mkiambiwa kuwa kuna baadhi ya wateuliwa wanafanya kazi kwa mihemko mnakuwa wakali na kuanza kuita watu bavicha
 
Aah kashajikuta amiri jeshi mkuu siyo. Hivi vyeo hivi vinajuwa kulevyaa
 
Back
Top Bottom