johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,616
- 141,450
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema anatengua nia yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Iringa mjini na kwamba ataendelea kuwatumikia wana Mbeya.
Chalamila amesema baada ya kumsikiliza Rais Magufuli jana kwa tahadhari aliyotoa kwa wateule wanaoomba ruhusa, alimwelewa vizuri na ameamua kubadili gia angani.
Source: Azam tv
Maendeleo hayana vyama!
====
RC Mbeya, Albert Chalamila Atengua Uamuzi wake Wa Kugombea Ubunge
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amesema kuwa hawezi kukiuka maagizo ya Rais Magufuli aliyowataka wateule wake kuridhika na nafasi walizonazo, hivyo ameamua kuendelea kuwatumikia wananchi wake na hivyo hawezi tena kukimbilia kugombea Ubunge.
“Nilikuwa miongoni mwa watia nia ya kugombea ubunge Iringa mjini, kwa sasa sintofanya hivyo zaidi ya kuendelea kuwatumikia wananchi wa Mbeya na kutii maelekezo ya Rais Magufuli,” amesema Chalamila na kuongeza;
“Ni hekima na busara na itakuwa ni utoto wa kupindukia kama leo hii nitakwenda kuchukua fomu kugombea nikashinda kwenye kura za maoni, halafu huku Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi nimekwishamkwaza kwa kuwaacha Watanzania wake wakilia na kuhangaika”.
Kauli hiyo ameitoa leo Jumanne tarehe 7 Julai 2020 jijini Mbeya wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kuongeza kuwa kuna miradi mingi amepewa kuisimamia, hivyo itakuwa ni utovu wa nidhamu kuukimbia Ukuu wa Mkoa na kukimbilia Ubunge, huku akiacha miradi hiyo bado haijakamilika.
Wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma Rais Magufuli alisema ili kazi ziendelee, taifa lazima liendelee kutatua matatizo ya kila siku ya wananchi, hivyo alisema hawezi kusubiri mtu anayeomba ruksa ya kusaka ubunge, akakose ndo arudi tena.