RC atoa wiki mbili waliotafuna Milioni 930 wazirudishe

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ametoa wiki mbili kwa maofisa watendaji kata na vijiji wanaotuhumiwa kutafuna fedha 'mbichi' zaidi ya Sh milioni 930/- kuziwasilisha serikalini.

Wangabo pia ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani humo kuchunguza mikataba ya miradi ya maendeleo na ya kimkakati kati ya wakandarasi na wakurugenzi wa halmashauri mkoani humo.

Alitoa maagizo hayo juzi mjini Sumbawanga wakati akifunga kikao cha kwanza mwaka huu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).

"Sasa hawa wote ambao wame-default hizi fedha zaidi ya Sh milioni 932, ninawapa wiki mbili tu wawe wamezirejesha, vinginevyoTAKUKURU itawasaka na kuwaburuza mahakamani hawa watu, wala sio tena ule mchezo wa kubembelezana kwamba leta kesho leta keshokutwa, waburuzwe mahakamani na nitaarifiwe mwezi ujao, hawa ni wezi hatuwezi kuwavumilia." Alionya Wangabo.

Alisema, viongozi hao wanatuhumiwa kutafuna mapato ya ndani na kutoziwasilisha benki.

"Halafu unakuta ‘mchwa’ ame-default mwaka jana, huyo huyo anapewa tena kukusanya hapo mahali, hatuwezi kwenda namna hii, halmashauri zetu tunazidhoofisha kimapato, tunazimaliza, tunazifilisi, mchwa hawa lazima tuwashughulikie, vinginevyo watakuwa wanaendelea kila siku katika hali hiyo hiyo, wanaona ni mchezo wa paukwa pakawa,"alionya.

Wangabo aliwafananisha viongozi hao na "mchwa" wanaozifilisi halmashauri kimapato huku mamlaka hizo zikiendelea kulalamika kuwa na mapato finyu.

Alionya kuwa watakaokaidi agizo hilo ameiagiza TAKUKURU iwasake na kuwafikisha mahakamani.

Pia alionya kuwa pamoja na hatua kadhaa alizowahi kuchukua awali kwa kuwakabidhi wadaiwa hao sugu TAKUKURU bado hawajabadilika.

Alieleza kusikitishwa kwa kuwa hakuna hata Mkurugenzi mmoja wa Halmashauri zote nne za mkoa huo aliyewahi kuwachukulia hatua wadaiwa sugu au hata kuonesha kuguswa na "wizi"huo.

Chanzo: Habari Leo
 
Bado najiuliza hapa hao jamaa wana meno ya aina gani kutafuna Milioni 930
 
Sasa kuna utofauti gani kati ya awamu hii na ile iliyopita kwenye suala zima la rushwa na upigaji?

Watu wanapiga tu madili!! Baada ya kuona hata baba mwenye nyumba nae anapiga!! Kazi kweli kweli.
 
Wazirudishe au waende jela
Mkuu mpango wa serikali siku hizi ni kwanza rudisha ulichoiba, then taratibu singine zinafuata. Zile mambo za unaiba 500m unazificha na zingine unahonga hakimu ili akupunguzie kifungo, then anakufunga miaka miwili alafu ukitoka unaukuta mzigo wako unautafuna vizuri kabisa, siku hizi hakuna kitu kama hicho. Ukibainika umeiba, unainamishwa kichwa na unatapika mzigo wote kwanza.
 
Sasa kuna utofauti gani kati ya awamu hii na ile iliyopita kwenye suala zima la rushwa na upigaji?

Watu wanapiga tu madili!! Baada ya kuona hata baba mwenye nyumba nae anapiga!! Kazi kweli kweli.
Mkuu upigaji hautokuja kuisha hata siku moja.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ametoa wiki mbili kwa maofisa watendaji kata na vijiji wanaotuhumiwa kutafuna fedha 'mbichi' zaidi ya Sh milioni 930/- kuziwasilisha serikalini.

Wangabo pia ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani humo kuchunguza mikataba ya miradi ya maendeleo na ya kimkakati kati ya wakandarasi na wakurugenzi wa halmashauri mkoani humo.

Alitoa maagizo hayo juzi mjini Sumbawanga wakati akifunga kikao cha kwanza mwaka huu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).

"Sasa hawa wote ambao wame-default hizi fedha zaidi ya Sh milioni 932, ninawapa wiki mbili tu wawe wamezirejesha, vinginevyoTAKUKURU itawasaka na kuwaburuza mahakamani hawa watu, wala sio tena ule mchezo wa kubembelezana kwamba leta kesho leta keshokutwa, waburuzwe mahakamani na nitaarifiwe mwezi ujao, hawa ni wezi hatuwezi kuwavumilia." Alionya Wangabo.

Alisema, viongozi hao wanatuhumiwa kutafuna mapato ya ndani na kutoziwasilisha benki.

"Halafu unakuta ‘mchwa’ ame-default mwaka jana, huyo huyo anapewa tena kukusanya hapo mahali, hatuwezi kwenda namna hii, halmashauri zetu tunazidhoofisha kimapato, tunazimaliza, tunazifilisi, mchwa hawa lazima tuwashughulikie, vinginevyo watakuwa wanaendelea kila siku katika hali hiyo hiyo, wanaona ni mchezo wa paukwa pakawa,"alionya.

Wangabo aliwafananisha viongozi hao na "mchwa" wanaozifilisi halmashauri kimapato huku mamlaka hizo zikiendelea kulalamika kuwa na mapato finyu.

Alionya kuwa watakaokaidi agizo hilo ameiagiza TAKUKURU iwasake na kuwafikisha mahakamani.

Pia alionya kuwa pamoja na hatua kadhaa alizowahi kuchukua awali kwa kuwakabidhi wadaiwa hao sugu TAKUKURU bado hawajabadilika.

Alieleza kusikitishwa kwa kuwa hakuna hata Mkurugenzi mmoja wa Halmashauri zote nne za mkoa huo aliyewahi kuwachukulia hatua wadaiwa sugu au hata kuonesha kuguswa na "wizi"huo.

Chanzo: Habari Leo
Hizo pesa zimeshafanyia maendeleo ya kifamilia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom