Inasikitisha saana pale mtuhumiwa anapoambiwa ajitetee kutokana na tuhuma zinazomkabili badala yake anaanza kutafuta mchawi kwa visingizio kibao. Kwa ufupi hakuna anayepinga juhudi unazozionyesha RC katika kupambana na janga la madawa ya kulevya, 'big up for that!' lakini kinachozungumziwa kwa sasa na ambacho unatakiwa kukifanya (kwa kuacha kujiondoa akili). Kwanza kabisa ni kukubali kuwa mzigo ulopewa sio haki yako kuubeba na ukiri wazi kuwa jambo hili ulilifahamu tangu mwanzo na mbaya zaidi unajua kuwa wewe ndio unatakiwa kuwaondolea aibu walokupa dhamana ya kushika mamlaka usiostahili kutokana na makosa kede kede uliyoyafanya katika kuutafuta utukufu huo ulio nao kwa sasa. Unachokifanya kwa sasa wewe pamoja na wanaokukingia kifua ni sawa sawa na mtu anayeanzisha ugonvi wa mawe na majirani zake ili khali akiishi kwenye nyumba ya vioo.Kwa kukusaidia ni kwamba wanaokulinda kwa sasa hawatakulinda tena baada ya miaka (8) iliyopo ndani ya uwezo wao Mungu jalia wakiwa bado wapo madarakani. Uamuzi uliokuwa umeufanya juzi wakukubali yaishe na kuachia ofisi kwa kukimbilia bondeni ulikuwa mzuri saana na kamwe usingekubali mawazo ya watu wengine walokushawishi kuwa urudi na watakulinda. Nimeshakwambia watakulinda maximum ni miaka (8) tu. Ndo maana wachina husema sikuzote ukishafanya maamuzi kwa jambo linalompendeza Mungu kamwe usirudi nyuma...kwa kukimbilia Bondeni 'that was a great decision' mwisho wa siku tungekusahau kama tulivyomsahau Kihiyo...Nafasi bado unayo na usijejidanganya kwamba hili jambo litaisha kirahisi tu pengine kwa kutengeneza matukio kama tukio ulilofanya leo...la kukusanya wasiojiweza na wachache wasiojitambua na kufanya 'mean press conference'.....Mwisho nasema hujachelewa saana hii vita ya madawa ya kulevya unayojificha ndani yake kwa ajili ya kuondoa kovu la makosa yako ya nyiuma 'still' unaweza pigana nayo hata ukiwa nje ya URC.