RC Ally Happy atoa wiki mbili kwa wakurugenzi 9 waoneshe ziliko fedha za Umma kiasi cha TZS 1.7BL

Serikali ya Hapi inaenda kuanguka kwa mara ya pili.

Ninaona Hapi akienda kasi bila mpangilio na hatimaye Serikali yake kuanguka bondeni.

Huyu kijana maji moto sana
 
View attachment 2122291
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi ametoa wiki mbili kwa wakurugenzi wa halmashauri tisa zilizopo mkoani humo kuhakikisha jumla ya shilingi bilioni 1.7 za mapato ya ndani ambazo hazijaingizwa benki ziwe zimeingizwa.

Aidha Hapi amewataka wakuu wa wilaya kuchunguza utolewaji mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya wanawake, watu wenye ulemavu na vijana na kuongeza kuwa ndani ya muda huo iwapo wahusika waliokula fedha hizo watabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo, Samweli Kiboye naye amewaagiza wenyeviti wa halmashauri za Mkoa wa Mara kuhoji juu ya madai ya upotevu wa fedha hizo kwa wakurugenzi wao.

Hayo yanakuja kufuatia maagizo aliyoyatoa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake mkoani humo ambapo alimuagiza mkuu huyo wa Mkoa wa Mara kuchukua hatua kwa baadhi ya watendaji ambao wanatuhumiwa katika upotevu huo wa fedha za miradi ya maendeleo.
Anabweka kujisafisha ccm ni genge la majambawazi
 
Back
Top Bottom