RC Aggrey Mwanri akagua miradi ya TARURA Tabora, amsimamisha kazi meneja, aunda tume

Jul 14, 2019
7
1
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amefanya ukaguzi wa miradi ya barabara na madaraja inayosimamiwa na TARURA mkoa wa Tabora, alitembelea miradi hiyo iliyopo halmashauri ya wilaya ya Iguga na halmashauri ya mji wa Nzega.

Akiwa halmashauri ya wilaya ya Igunga, RC Mwanri alitembelea mradi wa daraja na kufanya ukaguzi wa daraja hilo akiongozana watumishi kutoka katika ofisi yake. Mkuu wa Mkoa alishangazwa na mkandarasi wa mradi huo kutokuwa na mpango kazi (program), mkandarasi kusimamisha kazi bila kufuata taratibu, mradi kutokuwa na msimamizi na mhandisi wa TARURA Igunga kukataa kwamba yeye hana barua ya kusimamia mradi,

Akiwa halmashauri ya mji wa Nzega, RC Mwanri akiongozana na wasaidizi wake alifanya ukaguzi wa miradi ya barabara. Mkuu wa Mkoa alishangazwa na mkandarasi kulipwa malipo ya kazi na vipimo vya maabara wakati hakuna vipimo vya maabara vilivyofanyika, kutokuwepo na michoro ya kazi wakati wa ziara yake na meneja wa TARURA halmashauri ya mji wa Nzega Ally R. Mimbi kutokuwa na msaada kwa utendaji hafifu.

Baada ya ziara katika halmashauri ya wilaya ya Igunga na halmashauri ya mji wa Nzega kukamilika. RC Mwanri alitoa maagizo na kusema atarudi tena kujiridhisha kama maagizo yametekelezwa. Maagizo aliyotoa ni kama ifuatavyo;

1. Kusimamishwa kazi kwa meneja wa TARURA Igunga Sadiq Karume ili kupisha uchunguzi. Ofisi yake itatoa taarifa tu
kwa mtendaji mkuu wa TARURA baada ya yeye kumsimamisha kazi meneja huyo.
2. Tume itaundwa kutembelea miradi aliyokagua Igunga na mji wa Nzega. Tume hiyo itaongozwa na Meneja wa
TANROADS Mkoa wa Tabora.
3. Mkandarasi wa daraja katika halmashauri ya wilaya ya Igunga kuhakikisha anakuwa na mpango kazi, kuwepo eneo la
mradi na kuhakikisha vifaa vya ujenzi ikiwemo nondo, sementi vinakuwepo eneo la mradi wakati wote.
4. Mradi kuwa na msimamizi kutoka TARURA na kuwepo eneo la mradi muda wote.
5. Mkoa wake kuitaarifu Bodi ya Wakandasi Tanzania pale atakapozidi kuona wakandarasi hawatimizi majukumu yao.
Mkoa wake hautakubali kufanya kazi na wakandarasi wasiotimiza wajibu wao
6. Mratibu kuvaa soksi sawa sawa, Watumishi wa TARURA Tabora kuacha kuvaa miwani ya zamani, la sivyo yeye
atawavua na kutupa.
7. TARURA Tabora kutambua kwamba wao ni sehemu ya Serikali na kutoa ushirikiano kwa taasisi nyingine ze Serikali
ikiwemo kuhudhuria vikao vyote vya madiwani kwa halmashauri zote za mkoa huo.


Chanzo: ayo TV
 

Attachments

  • RC MWANRI ALIVYOMBANA INJINIA MPAKA KAMKATAA BOSI WAKE '.mp4
    33 MB
  • RC MWANRI AMSIMAMISHA KAZI MENEJA 'TUACHIE, VUA MIWANI SHUKA MTARONI'.mp4
    24.6 MB
Back
Top Bottom