RC afunga vituo 18 vya mafuta

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
RC afunga vituo 18 vya mafuta


na Julieth Mkireri, Kibaha


amka2.gif

VITUO 18 kati ya 31 vya mafuta vilivyopo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, vimefungwa kutoa huduma ya mafuta baada ya kubainika kuwa vimekiuka taratibu za uendeshaji wa vituo hivyo.
Sababu nyingine ya kufungiwa kwa vituo hivyo ni kujenga karibu na makazi ya watu pamoja na kukosa vyeti vya usalama wa moto na vifaa vya tahadhari.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani (RC), Amina Said, katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, alisema vituo hivyo vitafungwa kufuatia tathmini iliyofanywa na timu ya wataalamu aliyoiunda baada ya kuungua kwa kituo cha mafuta kilichokuwa kikijengwa katika kijiji cha Mdaula Wilaya ya Bagamoyo, pamoja na kukithiri kwa wingi wa vituo vya mafuta katika barabara kuu ya Da es salam-Morogoro, hususan Wilaya ya Kibaha.
Amina alisema Wilaya ya Kibaha pekee ilibainika kuwa na vituo 31 vya mafuta eneo la kilomita 29.7 sawa na wastani wa kilomita 0.95 ambao ungeweza kujengwa vituo 15 ambavyo pia vingeweza kujengwa mbali na makazi ya wananchi.
Mkuu huyo wa mkoa alieleza kuwa kamati hiyo ya wataalamu ilivigundua vituo hivyo 18 kuwa na mapungufu ya kukosa hati miliki ya maeneo, kujengwa ndani ya hifadhi ya barabara, kujenga yadi kubwa ya nyuma ya kituo yenye kuta ndefu, kuendesha shughuli nyingine kwenye yadi kama gereji, na nyingine kutokuwa na cheti cha usalama wa moto na vifaa vya tahadhari.
Aidha mkuu huyo wa mkoa alivitaja vituo vitakavyofungiwa kuwa ni pamoja na New Mlandizi Petrol Station, Fast Filling station, Petrol Gaz Mlandizi Petrol station, Misufini Petrol Gas, JAM Oil, Madafu Petrol station, TAWAQAL Fuel, Mdaula Filling station na Misa Oil Co.Ltd. Vituo vingine ni PANONE Filling station, Fuel Distribution Network, MOGAS Filling station, TANITA Petroleum, GBP Filling station, KOBIL Filling station, ORYX Filling station na NAT OIL. Aliongeza kusema kuwa vituo hivyo vitafungwa kati ya Agosti 4 na 5 baada ya Halmashauri ya Wilaya na mji wa Kibaha kukamilisha taratibu zake na kuweka mabango kwenye vituo hivyo na vitafunguliwa mara tu baada ya kurekebisha mapungufu yaliyogunduliwa na kamati ya kutathmini.
 
Back
Top Bottom