Katika tukio la kushabgaza RC Mongella wa kagera ameagiza walimu wa shule anbazao hazikufanya vizuri katika mitahani ya darasa la saba na kidato cha nne kuweka vinyago milangoni. Je hii itasaidia kuinua kiwango cha elimu?
Shule ya mwisho lazima iwepo wakuu,hata ukiweka vigezo vya namna gani.Huu hauwezi kuwa mkakati wa kuinua kiwango cha elimu.Elimu ni mchakato endelevu wa kuangalia fursa katika kutatua matatizo ya jamii kwa wakati muafaka.
Huyu Mkuu wa mkoa nadhani haelewi mahitaji mengine ya msingi ili shule iweze kupata mafanikio. Mahitaji ya msingi(basic inputs) ni pamoja na wanafunzi wenyewe wanaojiunga na shule hiyo. Kwa mfano, kama wamedumaa hata mwalimu afanye nini katika mazingira ya kawaida au bila msaada wa ziada hatofanikiwa kwa sababu hali ya udumavu ni ya kudumu. Pia kuna mazingira ya shule-ni saidizi kiasi gani ? Usisahau mahitaji muhimu kama vyumba vya madarasa, madawati, mbao za kuandikia, vitabu, huduma ya chakula shuleni, vyoo na maji shuleni, viwanja vya michezo nk. Pengine muhimu zaidi ni waalimu-waliandaliwa vya kutosha wakaivaa ?, idadi inatosha, wana ari ya kufundisha, wanapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa kamati ya shule na jamii ? Je wakaguzi wanafanya kazi yao ipasavyo ? Na maafisa elimu je ? Tusiwahukumu waalimu kila mara bila kuungalia udhaifu wa utendaji wa mfumo wetu wa elimu , hususan elimu ya msingi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.