Raza: Mshahara wa urais nitawapa wasiojiweza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raza: Mshahara wa urais nitawapa wasiojiweza

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyambala, Jun 28, 2010.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tanzania zaidi ya uijuavyo, inaonyesha watanzania kampeni za namna hii ndiyo unawapata. Kwa kumbukumbu Raza si wa kwanza kuahidi kusacrifice mshahara wake!


  Raza: Mshahara wa urais nitawapa wasiojiweza


  na Tamali Vullu, Zanzibar


  MGOMBEA urais Zanzibar, Mohamed Raza, amesema akifanikiwa kuwa rais wa Zanzibar mshahara wake wote ataupeleka kwa watu wasiojiweza ili waweze kuondokana na hali ngumu ya maisha. (Really???????)

  Raza alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mjini hapa alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kuwania kurithi nafasi hiyo inayoshikiliwa na Rais Aman Abeid Karume.

  Raza ambaye ni mfanyabiashara maarufu Zanzibar, alisema kitendo hicho kwake hakitakuwa cha kwanza kwani alipokuwa mshauri wa Rais Salmin Amour katika kipindi chote cha miaka sita hajapata kutumia mshahara wake bali aliuelekeza kusaidia wazee, watu wenye ulemavu na katika nyumba za ibada.

  “Nilipokuwa mshauri wa rais sikugusa mshahara wangu hata siku moja na hata mafao yangu sikuyagusa niliyapekeka kusaidia wazee, walemavu na nyumba za ibada na niliamua kufanya hivyo kutokana na kwamba Wazanzibari ndio walioniwezesha kufika hapa,” alisema Raza.

  Mambo mengine aliyopanga kuyafanya akiwa rais ni kuongeza maadili ya viongozi, kwani anaona yameporomoka kwa kiwango kikubwa na kuwatengenezea mazingira mazuri mawaziri na watendaji wengine wa serikali ili kukabiliana na tatizo la rushwa.

  “Ili kukabiliana na tatizo la rushwa miongoni mwa mawaziri na watendaji wengine wa serikali nitawatengenezea mazingira mazuri kwa kuwakopesha, ili kujenga nyumba kama hawana na kufanya vitu vingine vya kujiendeleza ili isiwe rahisi kwao kudanganyika kwa kupokea rushwa,” alisema.
  Kwa upande wa kukabiliana na matumizi mabaya ya fedha za umma, Raza atajitahidi kupunguza msafara wa magari ya rais.

  Mfanyabiashara huyo amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuleta mafanikio makubwa nchini na kwamba atakuwa na muda mzuri wa kuyaendeleza mengine yaliyosalia katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo na alimsifu Rais Karume kwa jihitada mbalimbali za kuiendeleza Zanzibar.
   
 2. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  uezo huo atautoa wapi??? why asingeanza kuwapa huo aupatao sasa??? kwani sasa hivi hana mshahara??? hana marupurupu??? he owns soap industries, ana kampuni ya usafirishaji n then ni waziri katika SMZ lakini hajafanya hivyo....mpk awe rais ndo atoe salary yake kwa masikini??? Hana lolote...beside he is saying so koz anajua he cant ba a president of Zanzibar.....Nilisoma juzi hapa JF kuwa hata shule yake ina walakini watoto wa mjini wanaita shule yake CHECHE........kweli ukistaajabu ya MUSA hutaona ya FIRAUNI
   
 3. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Yawezekana Jambo hili kutokea?
   
 4. A

  Audax JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  cyo kweli, maana hawa watu huwezi kuwalisha kwa muda wote na kibaya zaidi huwezi kutoa hiyo kama point ya kuchaguliwa,angeniambia ataanzisha miradi ya maendelea na wtu wawe kwenye makundi kama succos zinavyofanya ningemsifu.Hali ya kusaidia watu ndo inatuletea umaskini-badala yake,inabidi watu wajifunze kufanya kazi.
   
 5. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2010
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  asilete masihala hapa? kwa hamu ya urais watasema kila kitu, hata magari watatoa
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,645
  Likes Received: 21,856
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndio aina ya viongozi wengi wa Tanzania. Hawajui hata nini wanatakiwa kufanya wakichaguliwa kwa nafasi walizoomba. AIBU ni kwa wale wanao wachagua viongozi wa aina hii.
   
 7. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hawa viongozi wetu bana...... Huwa wananifurahisha sana. Kwa hiyo yeye atakuwa ni kuwa-spoon feed tu hawa masikini. Wasiojiweza kwa kiasi gani? Mwaka wa uchaguzi huu, tutasikia mengi!!!
   
 8. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  atawapa wangapi? au anataka urais wa maisha ili aweze kuwazungukia wazenji wote? si wengi wale
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hivi anadhani ndio kipaumbele ya kitu wanataka wazanzibari? Uenda kafanya uchunguzi na kugundua wazanzibar wanatoa urais kwa misaada tu.
  Anakumbuka enzi zake zile alizokuwa mtoa misaada mashuhuri kiasi cha kumpa umaarufu wa kuwa msemaji wa rais Salmin. Anadhani kwa hilo atapata urais.
  mambo yamebadilika sana bwana Raza.
   
 10. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  zote ni siasa tu
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  Wasiojiweza ni wangapi na mshahara wa rais ni kiasi gani? Mshahara ukigawanywa kwa kila asiyejiweza kila mmoja atapata kiasi gani? Kiasi hiki kitatosha kuwaondoa katika umasikini?

  Raza anajionyesha kwamba hana vision ya kuondoa umasikini, na kama mkakati wake wa kuondoa umasikini ni kugawia wasiojiweza mshahara wake, basi hafai urais.

  Version moja ya msemo maarufu wa kichina inasisitiza, mpe mtu chakula utamlisha kwa siku moja, mfundishe kutafuta chakula utamlisha kwa maisha yote. Raza ana mpango wa kuwapa watu chakula, hama mpango wa kuwafundisha watu kutafuta chakula.

  Na hata hicho chakula anachosema atawapa watu nina mashaka kama kitakuwa na maana.
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  But then again inawezekana huyu Raza anayajua yote haya tunayosema, ila yeye anaangalia local politics za Zanzibar, anaangalia benevolence ya ki Harun Rashid inavyothaminiwa, anaangalia utamaduni wa kiislamu na swala zima la Zakat na kutoa kwa masikini linavyothaminiwa beyond politics.

  Naye anapata pa kutokea hapo hapo.

  In other words hana mkakati wa maendeleo, lakini anaangalia nini kinaweza ku-appeal kwa watu.

  Cheap politricks.
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Well nadhani WanaJF hawamjui Raza kwani kwa ufupi huyu jamaaa ni tapeli na parasite mkubwa anayejifanya mzanzibar kwa kutetea maslahi yake ya biashara include biashara ya nanilii!!! kutokea kulea mpakani mwa pakistan na afghanistan. Huyu jamaa kila mwaka anachukua fomu za urais unadhani kwanini anafanya hivyo ndio anapopata attention na publicity. Vilevile ni njia nyengine ya kuchangia chama cha matapeli (CCM). Hivyo binafsi namuona kama anafurahisha kijiwe tu!!!!
   
 14. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  kwani taabu ipo wapi? Rais anatunzwa, mshahara wake hauna kazi. Hapa Raza anaonyesha kuutaka Urais ili kujiongezea CV tu. Matatizo ya Wazanzibar hayawezi kutatuliwa kwa mshahara wa Rais. Rais akitimiza wajibu wake kwa uaminifu, bidii na ubunifu ataiwezesha nchi kupata maendeleo na wananchi wataondokana na ugumu wa maisha.

  Ugumu wa maisha kwa nchi zetu hauwezi kuondolewa kwa kupewa fedha za chakula.

  hapa nampa pole Raza.
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,645
  Likes Received: 21,856
  Trophy Points: 280
  Pamoja na ujinga aliosema sio ajabu chama chake kikampitisha. Ndivyo walivyo. Kama unataka uhakika wa hilo nenda Singida uwaulize kwa nini walimpitisha Dewji? nenda Igunga nako uwaulize kuhusu Rostam aliahidi nini hadi wakampitisha? na pengine pengi tu. Hivyo ndivyo walivyo ndani ya chama chao, watu wenye vision za maendeleo hawana nafasi kubwa kama ilivyo kupata kiongozi/mfadhili basi.
  Ndio maana CCM wana sema ' KWISHA KWA UCHAGUZI MMOJA NDIO MWANZO WA UCHAGUZI MWINGINE' Wao wanawaza kuchukua madaraka tuu na si vinginevyo, habari ya kutekeleza mipango ya maendeleo kwao ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.
   
 16. s

  sultanwjps Member

  #16
  Jun 30, 2010
  Joined: Jun 27, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du Alu Huyu Raza mkali kweli kweli ,si bora kuwapa tu pesa za biashara zake
  chafu chafu. au ndio anataka kuimarisha biashara yake ya kukwepa custom duty
  na mengineo ambaya ni mzigo mkubwa kwa wazanzibari. Nafikiria kua ana
  kesi kubwa ya kujibu juu ya pesa anazokwepa kulipa ushuru. any how ni juu ya wapiga kura kukosea na kuchagua mtu kama huyu ili wamuache ajitajirishe yeye kwa kuangamiza umma.
   
 17. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 520
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Huyu Raza nafikiri anazeeka vibaya, Wazanzibari wa leo siyo wale wa enzi za ujima, enzi za kupekecha vijiti ndo upate moto, asiwe na mawazo kama Zakayo, ningemuone wa maana kama angeanza na kugawa hiyo faida anayoipata ktk biashara zake kwa watu wasio jiweza, asisubiri mpaka aende Ikulu ndo aanze kutoa, viongozi kama hawa ni wa kuogopa kama ukoma, zunguka duniani kote hakuna mahala wala hakuna mtu anayeweza kutoa misaada ya hela bila yeye kutopata any-return(s), ukiona hivyo ameshapanga mikakati yake ni wapi atapata nyingine, aache kuchezea Ikulu pale ni mahala patakatifu japo wanaoishi pale si watakatifu, wamevaa makoti machafu.yanayotoa harufu ya ufisadi
   
 18. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  We bwana mudogo Raza , gawa mipira tu na ndio upeo wa uwezo wako kifikra.Kugwa mshahara wa rais wa Zenj ikiwa ni kigezo cha wewe kuchguliwa basi ni tusi kubwa kwa watakao kuchagua
   
 19. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #19
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona hakutuambia hivyo wakati anapewa Uwaziri?
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  You have said it all bro!
   
Loading...