Raza aendelea kulumbana na Makamba

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mshauri wa Rais mstaafu Dk. Salmin Amour kwa masuala ya Michezo, Mohamed Raza, ameendelea kulumbana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, juu ya hali ya kisiasa visiwani Zanzibar.
Raza aliliambia gazeti hili jana kwa njia ya simu kuwa, hakumwelewa Makamba, alivyozungumzia kuhusu Zanzibar.
Mwanzoni mwa wiki hii, akijibu tuhuma zilizotolewa na mfanyabiashara huyo kuwa CCM imewatenga baadhi ya viongozi wastaafu wa Zanzibar, Makamba alisema kuwa tuhuma hizo hazina msingi na ni za uzushi.
Makamba alisema kuwa, kauli hiyo ya Raza ni upotoshaji mkubwa na wa makusudi.
Pia alisema viongozi hao walishirikiana katika hatua zote za mikutano ya kampeni hivyo anamshangaa Raza kusema kuwa walitelekezwa.
Makamba alitolea mfano mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kibandamaiti ambao ulihudhuriwa na Rais mstaafu, Dk Salmin Amour pamoja na ule wa Tume ya Taifa ya uchaguzi (Nec) wa kumwapisha Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Pia alimweleza Raza kuwa, CCM itaendelea kuwa katika serikali ya Zanzibar kwa miaka yote hata kama itashindwa katika uchaguzi wowote na sio kama mfanyabiashara huyo alivyodai kuwa, chama hicho kinaweza kuishia mwaka 2015 kutokana na mpasuko.
Aidha, Raza akijibu kauli hiyo ya Makamba aliyoitoa dhidi yake alisema kuwa, wito wake ulikuwa kwa Kamati Kuu na (Nec) kushirikiana na wenyeviti wa wilaya na mikoa kutathmini hali ya kisiasa visiwani humo.
Alisema lengo la ushirikiano huo ni kuondokana na kasoro zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu na kuwa na ushindi mnono uchaguzi utakaofanyika mwaka 2015.
Aidha, alisema uchaguzi uliopita CCM wameponea katika tundu la sindano.
“Uchaguzi uliopita unaonyesha dhahiri Chama cha Wananchi (CUF) wameendelea kujiimarisha eneo la Unguja kwa kuchukua majimbo manne wakati CCM haikuweza kupenya Pemba kuchukua jimbo lolote,” alisema.
Alitaja kasoro zilizojitokeza ni pamoja na viongozi wastaafu kutotumika kwenye uchaguzi uliopita hata katika uzinduzi wa kampeni iliyofanyika uwanja wa Kibanda Uhai.
Alisema katika kampeni hiyo viongozi wa kimataifa hawakuhudhuria kwa mialiko bali kwa machungu na upendo wa chama chao.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizolifikia gazeti hili, zimeonyesha kuwa, viongozi wa kimataifa walipangiwa kufanya mikutano mitatu kila mmoja eneo la Pemba lakini badala yake CCM ilifuta na kubaki miwili miwili.
Aidha, Raza alisema hakuna kundi litakaloongoza chama na kwamba mwenye mawazo kama hayo amepotoka na hawafai hivyo ni bora ajiondoe kwa sababu CCM ni mali ya wanachama wote.
Alisema umaarufu wa kiongozi ni chama ndio maana hata kiongozi aliyepata kura tano Zanzibar kwenye kamati maalum ya CCM Zanzibar, alipitishwa na Nec kuwania nafasi hiyo na kushinda.
Raza amemtaka Makamba kutolipuka kwa sababu yeye ni mwajiriwa tu ndani ya chama na kwamba kama anafikiri ni ubabe aende jeshini akaajiriwe.
Pia alisema kuwa tayari ameshatembelea majimbo 50 visiwani humo na kujionea hali halisi hivyo amemualika Makamba na timu yake nao waende.
Awali, Raza akizungumza na waandishi wa habari, alisema kuwa, matabaka kati ya marais wa wastaafu yalianza kudhihirika ilipoingia awamu ya sita, ambapo mmoja wa viongozi wastaafu Zanzibar alifuatwa nyumbani na kunyang’anywa magari.
Aidha alisema serikali ya awamu ya saba ilipoingia madarakani, kabla ya ile ya awamu ya sita kumaliza kipindi chake, ndani ya siku sita tu, mmoja wa viongozi wastaafu alipewa gari mpya aina Benz.
CHANZO: NIPASHE
 
Huyu Raza ameshachoka kuishi nini? Akiendeleza longo longo ,ataitwa kamati kuu kujieleza na huko kuna maji maalum .... au ka-ayota kake kako fiti?
Amemsahau Kolimba?
 
Back
Top Bottom