Rayvanny ndio Mangwea wa kizazi hiki cha muziki

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,522
7,368
img_1615007971726.jpg


Nataka tumzungumzie kidogo huyu fundi muziki kutoka WCB yaani Rayvanny aka Chui.

Rayvanny ni msanii anaeujua muziki haswa na anaweza kuufanya muziki vile anavyotaka. Kipaji chake sio cha nchi hii naweza kusema yupo mbele ya wakati.

Anaweza kufanya aina mbali mbali za muziki na akaua.

Anaweza kurap (msikilize kwenye Sugu au Pochi nene)

Anaweza kuimba muziki wa hisia ( msikilize kwenye ex boyfriend au vumilia)

Anaweza kuimba afro pop ( msikilize kwenye Kwetu au Number one)

Anaweza kuimba banger ( msikilize kwenye Gimme dat, Chuchumaa, Amaboko au Tetema)
Anaweza kuimba RnB, singeli mpaka rhumba ( sikiliza ufundi wa rhumba kwenye Kiuno)

Rayvanny anaweza kufanya freestyle toka Mbeya mpaka Pretoria uku anazingatia vina, mizani na context.

Hii package nakumbuka alikuwa nayo Albert Mangwea (RIP).

Nimeona nimzungumze kidogo maana sio msanii anaezungumzwa sana na wadaku japo anauza sana muziki wake (Ndio msanii number 2 kwa kuuza sana muziki east africa). Maana yake watu wanampenda na kumfatilia kwa sababu ya muziki sio drama za insta, wengi wetu hatujui hata gari anayoendesha Ray inafananaje, hatujui anaishi wapi hatujui sura za wazazi wake sisi tunainjoi mziki mzuri toka kwake.

Japo mara chache alizoingia kwenye scandal nchi uwa inasimama ( refer scandal wimbo wa Nyegezi na ya mpenzi wake Paula mpaka serikali ilitoa tamko).

Nafikiri kwa talent aliyonayo tupo sahihi kabisa kusema Vanny Boi ndio Ngwea wa kizazi hiki.
 
Back
Top Bottom