Rayvanny - I Love You, Mbosso - Ate, Lavalava - Tekenya: Naona mmeamua kutuchezea nyie vijana wa WCB

Nobunaga

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
1,169
4,985
Rayvanny wa I Love You sio yule wa Kwetu na Natafuta Kiki.

Mbosso wa Ate sio yule wa Hodari na Maajabu.

Lavalava wa Tekenya sio yule tulomzoea wa mapini makali kama Bora Tuachane na Niuwe.

Hivi nyie vijana wa WCB ndio mmeamua kuprove kwamba Harmonize alikuwa mkali namba 2 kama sio namba 1 hapo mjengoni mwenu?

Nilitaraji baada ya kuondoka kwake mngejichimbia chobingo kisha mtoke na madude konki ya kutikisa nchi, matokeo yake mnatuletea viuharo visivyo hata tone la chumvi.

Hizo ngoma zenu ni mbovu bora hata ile Babalao ya bosi wenu. Yani ni mbovu kuliko hata ile Kushoto Kulia ya mwenzenu Harmonize, japokuwa nayo ni mbovu, ila zenu ni mbovu zaidi.

Vijana mmepwaya ndio maana hampati shows nyingi kama alivyokuwa Harmonize. Yani ni dhambi kubwa bosi wenu anapata shows nyingi kuwashinda nyie wakati kiuhalisia nyie ndio mlitakiwa mpambane kuonesha kwamba you worth somerhing kama alivokuwa Harmonize.

Sasa nawaambia kama mtaendelea hivi basi mtaishia kuwa watumbuizaji wa shows za vichochoroni na Wasafi Festival tuu. Tena mkiendelea kupwaya hivi hamchelewi kupigwa chini na hiyo lebo yenu ya kiswahili.

Mwisho wa mwaka huu bwana tunataka madude konkii ya kulia Xmass, alaaah.👽

By Bumblebee1 wa Buza kwa Mpalange.
 
We jamaa masikio yako yatakuwa mabovu sio bure, hz nyimbo tatu tu ni playlist ya "magogoni" we unaleta za kuleta hapa? Juzi nimepishana na Shonza simu yake ikaita kumbe kaweka "I love you" ya Vanny boy kama muito wa simu yake.... Ila nisiongee sana inawezekana we ni 'ke', ila km ni 'me' duh...
 
Back
Top Bottom