Ray the greatest na tamko rasmi la kuhusu kuhusishwa na kifo cha kanumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ray the greatest na tamko rasmi la kuhusu kuhusishwa na kifo cha kanumba

Discussion in 'Celebrities Forum' started by ngoshwe, Apr 24, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Yapata wiki tatu sasa tangu msanii mwenzangu Steven Kanumba aage dunia, na kama ilivyo kwa kila kitu kinapotokea huandamana na kila aina ya maneno na hisia mbali mbali kutokana na mitazamo ya watu kupishana kuhusiana na jambo husika. Kulingana na muktadha huo, msiba wa Steven Kanumba umekumbwa na maneno na hisia kama hizo, hususan mazingira ya kifo chake; kinachosikitisha zaidi watu wengi (ambao wanajitambulisha kama wapenzi wa Kanumba), na baadhi ya vyombo binafsi vya habari vimekuwa vikinihusisha na kifo hicho, kwa kusema kwamba kwa njia moja au nyingine ninahusika na mauaji ya Steven Kanumba. Kwa muda wote huo tangu msiba ulipotokea mpaka leo hii nashika kalamu kujaribu kuyaweka sawa na kuondosha hisia chafu katika fikra za watu, nimekuwa nikipitia katika wakati mgumu sana kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikinyooshewa vidole kila upande nikihusishwa na kifo hicho, kiujumla nimezingatia maoni ya wapenzi ya mashabiki wangu wakinitaka kuwa na subira, ila kuna ukweli usemao kwamba, uongo ukirudiwa sana jamii huusadiki na kuuona ukweli, nimeona nisikae kimya ila niweke sawa hili kwamba sihusiki na kifo cha Steven Kanumba.

  Nasema wazi kwanza sihusiki kabisa na kifo cha Kanumba kwanza kwa kuzingatia mazingira yenyewe ya kifo kilivyotokea. Wakati kifo hicho kinatokea, nilikuwa sehemu nyingine kabisa na mimi nilikuwa mtu wa tatu kutaarifiwa kwamba Kanumba amepatwa na mkasa ambao baadae ulisababisha kifo chake. Na na hata nilipofika katika hospitali ya Muhimbili (tofauti na watu wanavyodhani kuwa nilifika nyumbani kwake; ukweli mimi nilimkuta tayari amepelekwa Muhimbili), nilikuta tayari alikuwa ameshafariki ndio maana hata Polisi wanaohusika na usalama wa raia, si tu kwamba hawakuniweka chini ya ulinzi, sikuitwa hata kuhojiwa kwa sababu hakuna mazingira yoyote yanayonihusisha mimi na kifo hicho.

  Pili, watu wanahusisha tofauti za kibinadamu zilizokuwepo baina yetu na kifo hicho, nasema hii sio sahihi kwa sababu kwanza ni kawaida kwa binadamu kutofautiana, isipokuwa kwetu sisi baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vinakuza kwa sababu nisizozijua, hivyo jamii ikachukulia kuwa tofauti zile ni uadui kitu ambacho sio sahihi, kwani sisi hatukuwa watu pekee tunaotofautiana kwani huu ni mwenendo wa kawaida wa dunia; hivi jana tumeshuhudia Waziri mmoja akieleza bayana katika mkutano na waandishi wa habari kuwa na tofauti na naibu wake, lakini hatuajasikia ikiandikwa wana ‘bifu' bali imetafutwa lugha nzuri ya kupamba tofauti hizo, kwa kuwa waliohusika ni waheshimiwa, ila kwa wengine kutokana na sababu tusizozijua, inaonekana kama ni haki yetu kuandikwa vibaya.

  Kinachosikitisha, kwa nini jambo hili linachukuliwa kwa mkazo mkubwa sana, kwani hatujawahi kusikia watu wakiwa wanatofautiana na ndugu jamaa hata na marafiki zao na inaonekana kawaida tu? Kwani vyombo vya habari havikuwahi kuandika kuwa marehemu Steven Kanumba alikuwa na tofauti na baba yake, na yeye mwenyewe alitamka hivyo katika vyombo vya habari, mbona wameliongea bila kuongeza chumvi, na jamii inaona kuwa ni jambo la kawaida la kibinadamu.


  Pengine watu wanaojaribu kuongea hayo, hawajui mimi na Steven Kanumba tumetoka wapi? Sisi si watu tuliokutana barabarani, tuna historia katika kazi yetu ya sanaa na pia katika maisha maisha yetu. Mwanzoni kabisa, mimi ndiye niliyempokea Kanumba pale Kaole na ndiye niliyemfundisha sanaa pale (nadhani watu wanakumbuka tamthiliya za wakati huo ITV) na baada ya hapo tulienda pamoja katika kampuni ya Game 1[SUP]st[/SUP] Quality pamoja na tukafanya filamu kama Johari, Sikitiko Langu, Dangerous Disire na nyinginezo, na tuliendelea kuwa pamoja katika kampuni hiyo mpaka tulipofanya filamu ya Oprah mwaka 2008 ambapo niliingia rasmi kufanya kazi za kampuni yangu, lakini tuliendelea kuwa pamoja hata wakati nikiendelea na kazi za kampuni yangu. Pia mimi nilikuwa wa kwanza kuanza kufanya kazi na Steps na baadae Kanumba alipoanza kufanya kazi zake mwenyewe na kunikuta huko tuliendelea kuwa pamoja kama siku zote. Kitu kikubwa kilichokuwa kinaendelea baina yetu, ni kwamba tulijenga ushindani wa kuendeleza kazi mbele kwa kila mmoja akitoa kazi, mwingine anamjibu, Isitoshe hata vitu vyetu binafsi utaona kama kuna kufanana; kuna wakati Kanumba alinunua Toyota Ruv 4 nyeusi mimi nikanunua ya kijani, aliponunua Harrier na mimi nikanunua pia, na hata gari za hivi karibuni, ukitazama utaona kuwa zinafana kwa karibu; hii ilikuwa ni kama maisha yetu, hatukuwa na uadui, ilikuwa tunapeana changamoto za maendeleo.

  Watu wanaojaribu kuonesha kuwa tofauti zetu ilikuwa ni uadui, huwa hawajui wapi tulikotoka ndio maana wanasema wasemavyo na katika kuthibitisha kuwa tofauti hizo hazikufikia katika uadui, kuna watu ambao wanafanya kazi nami katika kampuni yangu ya RJ ndio hao hao Kanumba alikuwa anawatumia siku zote katika kazi zake, hata baada ya tofauti hizo hakuna aliyekoma kufanya kazi na yeyote kati yetu. Hii inathibitisha kuwa tofauti ilikuwa kati yetu kama binadamu, sio chuki za kimafanikio, ingekuwa hivyo watu kama Junior Syaary ambaye mara nyingi hufanya final editing katika RJ ndio huyo huyo alikuwa akifanya na Kanumba, Ally Yakuti ambaye anaandika script za RJ, ndiye huyo huyo aliyekuwa anaandika kwa Kanumba, Steven Shoo ambaye ni mtaalamu wangu wa light, ndiye huyo huyo anayetumiwa na Kanumba na wengine wengi kama Juma Chikoka aliyecheza kikamilifu katika filamu ya kijiji cha Tambua Haki, ambaye pia anashiriki filamu nyingi za RJ, na wote hao, hawakuanzia kwa Kanumba, wote wameanza kwangu mimi ndio niliompatia na hata baada ya hayo yanayosemwa kuwa kuwa ni uadui, sikuwahi kuwakataza kufanya kazi na Kanumba.

  Tatu kumtuhumu mtu kwa namna yoyote ile bila ya uthibitisho wa tuhuma hizo, ni kosa kwa sheria za nchi na pia kama ni mfuasi wa dini yoyote ni dhambi, kwani wakati ukisema hayo huku hujui uhalisia bali unasukumwa na nguvu za hisia tu ni sawa na kumchafua mtu huyo katika jamii bila ya kujua jamii inamchukuliaje. Napenda kusema wazi wazi kuwa, kwa kila anayetekwa na wimbi hili, ajaribu kufikiria leo ipo kwangu mimi, kesho inaweza kuhamia kwako, kwani mimi sio wa kwanza kufikwa na haya, inaweza kukukuta hata wewe au ndugu yako, utajisikiaje. Na kama kweli mimi nimehusika na kifo cha Kanumba kwa namna yoyote ile, basi Mungu atanihukumu na kila aliye hai atashuhudia, ila kama sijahusika kwa lolote, Mungu hatonihukumu na badala yake ataniinua, kwa kuwa ninapita katika kipindi kigumu mno sasa hivi kwa madhila haya.
  Mwisho kabisa napenda kumaliza kwa msemo usemao, ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke, kwani kadri mambo haya yanavyoendelea, usidhani yataishia kwangu, kwani mkono wa dhuluma haushii karibu, ukisikia jirani anapiga kelele za mwizi, usilale kamsaidie, usiseme kuwa hatuhusiki kwani hayupo kwetu, kesho utafikwa na wewe utakosa wa kukusaidia. cha msingi kama tunampenda sana ndugu yetu ni kumuombea kwa Mungu, kwani hatujui makao yake huko aliko, na sio kuunda vitu ambavyo kamwe hata yeye angekuwa hai asingeviafiki.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA MAHALI PEMA
  PEPONI
  MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA


  ------------------------------

  [h=2]UYO RAY HATA BAADA YA KUFANYA MA INTERVIEW KIBAO NA KUPELEKA STORY KWENYE MAGAZETI[/h][h=2]MASKINI YA MUNGU HATA PICHA YAKE HAWAKUWEKA GAZETINI, AMENUNAJE HUKO ALIKO....,...[/h][h=2]MAMA U-TURN NIMEUZAJE SURA???? NA FULL NAME JUU....LOLEST....[/h]
  [h=6]Gosh, this is the kind of silly news a main stream paper in Tanzania writes.[/h][h=6]The country is going through a major crisis right now and they actually find space, tena a really visible space to write such a stupid untrue story.[/h][h=6]Ok, this is the last time im addressing this stupid.[/h][h=6][/h][h=6]SIJAWAHI KULALA NDANI IN MY ENTIRE LIFE AISEE…I HAVE NEVER SEEN THE INSIDE OF A CELL.[/h][h=6][/h][h=6]I mean vitu vingine tujaribu kutumia common sense, hivi Ray ni wa kunilaza mimi ndani au kunifunga????? Gosh, that will be the day!!!![/h][h=6][/h][h=6]Mtanzania Daima, Irene whoever, u got wrong information and its so stupid of you to publish it without speaking to me first. I spoke to a policeman on the phone and was told wataniita if ever nitahitajika because some dude called Ray complained about something that he thinks originated from me, how is a phone conversation being translated into spending a night in jail?????[/h][h=6][/h][h=6]And some blogger from Minessota, instead of kumaliza shule, maana for 6yrs now bado anasoma bachelors which is a 4 yr degree. Huo muda unaotumia kuspread negativity about Mange Kimambi na kujisifia nimemkomesha Mange,Mie ndo kiboko wa Mange. Why don't u study and try to graduate kabla hujajikuta unasoma bachelors degree for 10yrs??? By the way I will keep ignoring your insults siwezi kujibishana na mtu ambae highest completed education ni secondary school, maana clearly upeo wetu ni tofauti sana.
  [/h][h=6]hivi ukiona unamtukana mtu daily on your facebook page and that person doesnt respond, instead of kusema kaniogopa why dont u think KANIDHARAU AU KANIONA MJINGA???? Anyways, ndo hivyo tena inabidi uwe umesoma ili uweze kufikiria kidogo. Maana sidhani kama nitaweza ku argue na mtu ambae anaenda kusimama kwenye magari ya watu huko marekani then anapiga picha na kupost on her blog saying gari lake. and definately siwezi kumtukana mtu ambae for 5yrs anatembea na mume wa mtu, alafu anasema ye mzuri sana ungekuwa mzuri ungekuwa na mume wako mwenyewe shoga, au huyo mume wa mtu angemwacha mkewe akuoe wewe.unajiona mzuri alafu kutwa kudandia waume za wenzio...THIS GIRL REALLY NEEDS TO GO SEAT DOWN SOMEWHERE AND SHUT THE **** UP!!! [/h]http://www.u-turn.co.tz/
   
 2. Mkare_wenu

  Mkare_wenu JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Pole sana kaka.dedication:mapito by bahat bukuku
   
 3. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Thats great RAY...Wote wanaokuchukia ilhali hata hawajui wanakuchukia kwanini Mungu awasamehe bure, Be strong brother!
   
 4. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Najaribu kuvuta picha ni kwa namna gani nafc yako inafeel ryt nw, na vile ambavyo psychological upo, najkuta na huzun ya hal ya juu sana sabab ya wabongo wenye fkra finyu na mlegezo! But go strong na 'majaribu ni mtaji'.
   
 5. k

  kagame Senior Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Dec 6, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bora umefunguka kaka, wale watakaoshindwa kukuelewa itakuwa wametaka iwe hivyo, nakupongeza kwa kutokea hadharani na kusema juu ya hili suala coz mtaani kulijaa sana gossip hii, peleka andiko lako hili global publisher pia coz wao wanacheza kama petrol katika tuhuma hii kwa lengo la kibiashara coz it is hot of the town hii news.
   
 6. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  i think ray is suffering because of obe great ***** we allowed to flourish kama yule lusinde wa zeutamu
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kama jambo hajafanya sidhani kama ana haja ya kuumia..
  Binadamu tumeumbwa kuongea ..mazuri na mabaya yote tunaongea..
  Shika sana imani yako..
   
 8. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ray angalia mbele,pambana na maisha.lakini kuna kidudu mtu kinaitwa kimambe sijui nan....anajitapa sana na anakuzonga sana anakutaka nin?mpeleke mahakaman kwani anakuchafua kwenye u-turn,
   
 9. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  RAY THE GREATEST vs KANUMBA THE GREAT!! Hapa ndipo watu wanapohisi vibaya juu ya THE GREATEST unashindana na mwenzio ya nini??
   
 10. Zabibu

  Zabibu JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pole Ray kwa hizo tuhuma ulizozipata,mtumaini MUNGU tu na yote yatapita.
   
 11. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nadhani Ray anatania.
  Mtu aliye katika wakati Mgumu sana na anastahili kuonewa huruma ni Lulu.
  Kwa kiasi sympath on you inakuja but Lulu anaonewa sana tena sana.

  Maumivu yangu kwa Babu Seya ni sawa na kwa Lulu.
   
 12. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ray, I have never liked your films, but nakufagilia sana kwa hili tamko. Bravo!

  As for the blog you have cited (u-turn) when reading what she writes on her blog, there is only one conclusion one can derive...

  She might be a psychiatric case.....
   
 13. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  I know Ray,nimemsoma Mange na kufuatilia marumbano yao,tuhuma za kila mkmoja kwa mwenzie na hasa tuhuma za RAY.Nimejifunza jambo moja kuwa Mange ni mwelevu asie na busara na hivyo RAY uwezi kushindana na binti yule. Alichokisema kwa kuwa nae anamatatizo ya kisaikolojia japo alitaka kusema jambo la MAANA kukuhusu lakini njia alizotumia kukusema ndio tata.Ni sawa na kusema UTAJIRI sio dhambi bali dhambi itakuwa justified kwa njia ambayo iliyotumika kupata UTAJIRI huo.

  Hivyo kusemwa kwa Ray kuwa kahusika na kifo cha Kanumba ni mfumo mbaya wa mwelevu mlevi wa material asie na busara za kuchangua njia sahihi ya kufikisha ujumbe wake kwa muhusika pasipo kuacha makovu kama haya ambayo Ray sasa anaangaika kuyatibu.

  Binafsi aliyepiga picha za Kanumba akiwa kesha fariki au bado ajafariki katika hali ile,hakika HAIPASWI AWE RAY au mwingine yeyote aliyekaribu na Kanumba.Ndio jamii inaitaji picha hizo lakini wapigaji wa picha hizo walipaswa kuwa ni waandishi wa habari na sio mtu wa karibu na marehemu.Na kama ilifanywa na Rai,kama sehemu ya kumbukumbu kama Ray ungekuwa Smart ungeziifadhi kama kumbukumbu ya jamaa yako na sio kuwa Public na hakika kwa watu wa elevu pengine ungekuja kuzitoa ukiwa na miaka 80 kama Mungu akikupa uhai kama sehemu yako ya kuwaachia walimwengu kumbukumbu na kuonyesha kuwa kweli ulikuwa karibu.

  Lakini hiii ya kumphotoa marehemu ambae alikuwa jamaa yako,Mange kukuita muuaji kwa waelevu na watu wenye busara akumaanisha kitendo cha wewe kutenda bali huo UTU WAKO wa kuangaika na CAMAERA wakati Moyo wako ulipaswa kuwa na JAKAMOYO [Consciousness] dhidi ya tendo la kumuona mwenzio kwenye hali ile uku ukishindani na dhamila yako kuwa UNAYOYAONA MBELE YA MACHO YAKO NI KWELI MWENZIO KAFA KWELI!!.

  Tendo la wewe kupiga picha kisha kusemekana ukazipost kwenye fb, BBM yako ni dhahili dhamira yako dhidi ya marehemu HAKIKA UPENDE USIPENDE KWA WATU MAKINI INATIA SHAKA NA HIVYO KUHOJI KULIKONI,UPATE MUDA WA KUPIGA PICHA ZA MTU AMBAE KWAKO NI MTU MUHIMU NA SWAHIBA MBALI YA YOTE HE IS YOUR HOMIE.

  Ingekuwa sahihii kuwa kabla ya kifo cha marehemu,labda masaa matatu ulipiga picha na marehemu sehemu fulani,na ghafla unapata taarifa ya kifo chake basi kwa tahaluki ungekuwa sahihi kutuwekea picha hizo kua jamaani oneni nilikuwa nae muda mfupi uliopita nimekuwa shocked!!

  Hivyo kwa ushauri wangu ACHANA NA MANGE,Mange ni uzao wa mtu mwelevu sana tena Engineer,bahati mbaya inaonyesha anagenetics za kishari ambazo zaweza kuwa ni kasoro japo alichosema kwa Waelevu wanajua alimaanisha nini!Hivyo kushindana nae atakuhumbua kuna mtu kwenye magazeti yenu ya UDAKU sijui RISASI katoa ukulasa mzima akikuomba umpuuze na uendelee na maisha yako.Nami naomba usimpuuze maneno aliyosema bali UTAFAKARI KAULI YAKE na KUPIMA KWANINI ALIYASEMA YALE!!Uende itakusaidia kesho na kesho kutwa ukawa imara na kuijtambua.

  Tatizo lenu nyie mnaojiita masuperstar mkipata umaalufu mnasahau na kumezwa na umaalufu kiasi kuwa mnawasukuma mbali watu wa kuwashauri,na kubakiza watu ovyo ovyo kwenye mazingira yenu na hivyo kutokuwa japo na rafki mmoja mwenye busara wa kukushauri.Angekuwepo hakika angekushauri usizipost picha za marehemu kanumba kwenye BBM na FB.

  Kingine nenda shule,kuna english courses kibao,kuna walimu wa sanaa chuo kikuu pale kaombe seminar jifunze kuact kama professional,binafsi nakupenda wewe kama Ray ukizingatia nakufahamu toka enz hizo za kambarage/soko mjinga.lakini sikufichi SIZIPENDI KAZI ZAKO kwa kuwa naona kama unalopoka na kupiga makelele na kuwa mtu yule yule kama Ray na sio mhusika wa part anaendeshwa na mwili wa Ray [Acting].Picha nyingi za Ray zinakelele [Shouting ] kuliko kuongea na mbaya zaidi,unashindwa kuwa George [Ray ] wa picha A kukutofautisha Peter [Ray] wa picha B,na hasa neno linalonichefua 'Pumbaf!!!' kutumika kwa wahusika wote kama vile ni Ray mchezaji na sio mwigizwaji [actor].

  Shule ni kitu muhimu sana,hakika ukiweka mshipa wa aibu pembeni ukatumia kwa siku japo masaa mawili kuwa darasani kama pale UDSM,baada ya miaka mitatu utakuwa another RAY.Jibidiishe kuongeza maarifa pia ondoa hiyo egoism ya kishamba, to me your Ray I know from the hood I respect you as a man,lakini ili la kujifanya USUPERSTAR MNALINGA MABALALANI NA KUJIFANYA MKO BUSSY,KUNAWANYIMA MAARIFA.

  Achna na Mange,she is another level,sio ya kipesa,bali hapo kichwani kwake,najua mazingira ya malezi yako,na kupitia historia ya mzazi wa Mange unaweza kujua mazingira aliyolelewa binti ni ya kiwango gani cha ufahamu na genetical ana gene gani za ufahamu ukilinganisha na wewe na pia ameenda shule ya kiasi chake!!!Jipange jaribu kuwa bussy kutafuta vichwa vya kukusaidia kuengeneer Film industry ya filamu za kibongo kwa kuwa model wako ndio hivyo Mungu kamchukua kazi unayo wewe kuonyesha kuwa UNAWEZA.Ila nasisitiza shule ni muhimu sana sana sana kwa kukusaidia nenda pale UDSM tafuta mtu anaitwa KASABUBU atakusaidia kukuongoza upate mwelekeo wa pa kuanzia.
   
 14. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Pole sana kijana ray.
   
 15. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,834
  Trophy Points: 280
  pole sana ray
   
 16. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  Rey tulia tu ni upepo utapita tu.
   
 17. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  The JK style.....
   
 18. P

  PINER Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  well said....MDAU....Na hata muandishi amesema RAY na Mange hawafanani wako totauti sanaaaa...NADANI PALE MUANDISHI ALIMAANISHA RAY STD 7 NA MANGE MBA...NAKUBALIANA NA MWANDISHI KUWA HAWA WATU HAWAFANANI WAKO TOFAUTI KABSAA
   
 19. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,458
  Trophy Points: 280
  Haaa hiyo mbona kawaida sana mbona wanamziki wanashindana, si hapa tanzania tu hadi nje ni sababu za kibiashara katika sanaa
   
 20. M

  Marytina JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hamna ubaya wowote kushindana na mwenzio kibiashara na kimkakati
  jamaa walifanya kazi na kanumba pamoja na ray sasa hapo personal ugomvi upo wapi??
   
Loading...