Ray na wengine kibao wahojiwa juu ya kifo cha kanumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ray na wengine kibao wahojiwa juu ya kifo cha kanumba

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Gumzo, Apr 18, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BADO sakata la kifo cha Steven Charles Kanumba ‘The Great’ ni bichi na kwa mambo yalivyo, kuna uwezekano watu wengi zaidi wakaingia matatani kwa namna moja au nyingine.

  Habari zinadai kuwa wakati upelelezi ukiendelea, kuna ambao tayari wamehojiwa na inawezekana wengi watahojiwa kwa kadiri ishu hiyo inavyozidi kuchukua sura mpya.


  WALIOHOJIWA
  LULU
  Ukimwondoa mtuhumiwa namba moja wa kifo hicho, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ambaye alishahojiwa na kupandishwa kizimbani kisha kuwekwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Segerea, Dar, kuna wengine walio roho juu.  SETH BOSCO
  Katika tukio hilo, pia tayari ndugu ambaye ni mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco naye alishafikishwa kwenye kituo cha polisi cha Oysterbay Kinondoni na kuhojiwa kuhusu anachokijua juu ya kifo hicho kwa kuwa ndiye mtu wa kwanza kuingia chumbani baada ya staa huyo kudondoka.  DAKTARI
  Naye aliyekuwa daktari wa marehemu Kanumba aliyetajwa kwa jina moja ka Kabugi maarufu kama Kidume, alikuwa mmoja wa watu waliofika kituo cha polisi Oysterbay kutoa maelezo akiwemo mwigizaji swahiba wa marehemu Kanumba, Vincent Kigosi ‘Ray’.


   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hata wale waliokuwa wakiandika habari za kifo cha Kanumba KIUDAKU lazima watahojiwa waleze source ya habari waliyoandika.................. Najua kuna watu watakimbia ID zao humu....................
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Gustavo huachi vituko?
  Sasa naona wataanza na magazeti ya Shigongo maana hayo yalidai pia kumuona Kanumba Tabata baada ya mazishi yake
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Yale yaleeeeeeeeeeee!
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Pia humu JF kuna wadau walichonga sana juu ya kifo cha KANUMBA....................sasa wote Mbombo Jilipo..............

   
 6. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  wallah! heri mimi sikusema!
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hahahah,ndo wajasiriamal we2 hao mdau,
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  Afadhali, maana humu ndani ilikuwa kanumbaaa kuanumba wote walioleta uzi humu wahojiwe.....


   
Loading...