Ray Kigosi awatolea povu watanzania, kisa unafiki wao

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray ametoa ujumbe ambao unalenga kutoa uelewa kwa mashabiki hasa wa filamu na muziki nchini ambao wamekuwa wakiponda juhudi za mastaa wa Kitanzania Huku akitolea mfano wa Kanumba na Diamond platnumz

Ray Kigosi ameandika…
1. Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza!!

2. Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa Sana na kuitwa bogus kwa Madai hajui kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama Kanumba!

3. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa
kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema maneno machache Kuwa mtanikumbuka kama si Leo basi Ni Kesho.And alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba !HAO NDIO BINADAMU NA TABIA ZAO Je, Kanumba kaondoka na Bongo Movie yake ya Freemanson ? Kama wengine mnavyodhani industry Ni Mtu sio system !

4. Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia ya mafanikio kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema Ni Freemanson, wengine
wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema Hana muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini na kina Wema.Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa ! Hatuombi baya limpate Diamond ili kudhibitisha tabia na unafiki wa binadamu. But HAO NDIO BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni sehemu ya Maisha.

5. Kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh Diamond Ni mchawi, kasema mleteni huyo mganga wangu mkashindwa kumleta, akajitokeza mganga fake sijui na Madai juu Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwa sababu ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema sawa namtegemea Mungu. Miaka 4 sasa tangu yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema lolote Ni haki Yao.

Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIOBINADAMU na tabia zao. Ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa Uchawi wanageuza walichoamini Ni nyeusi kiwe nye.
Capture-11.png

llllllllllll.png
 
Kweli kabisa ley, hata juzi tuliona baadhi ya wabunge waliokuwa wakimponda kikwete wakimshangilia bungeni na kutamka tumekumiss, lkn ndo waliosema serikari ya jk legelege,dhaifu,wa nataka rais wakuinyoosha nchi, Nikweli binadam mmoja ana roho saba. Bongo move simamieni na kudai haki yenu kwani haki haiombwi ila hudaiwa.
 
Ndio nani huyu?
Huhitaji kumfahamu ni nani bali ujumbe wa kweli umefika japo simfahamu na siangalii movie zake lakini alichokisema ni cha kweli. Mimi nitaenda mbali hata Lowasa tulimuita FISADI lakini baadhi yetu wanamuona LOWASA yuleyule ambaye hajafanya lolote lile la kujisafisha na huo uliosemwa UFISADI leo tunasema ni rais wa mioyo....Na hata Magufuli tunayemsema hajui kiingereza akimaliza muda wake tutamshangilia pia hapo ndipo ubaya wa TAIFA lilojaa wanafiki kila kona utakapoliona...........
 
Mbona huelewi wewe... bongo movie ipi unaiongelea ????!!!!

Pamoja na povu lote mnalotoa lakini ukweli utabaki pale pale...

KANUMBA AMEONDOKA NA BONGO MOVIE YAKE...
 
Huyu Ray mpumbafu kweli,wameshindwa kutengeneza movie tamu zenye sifa ya kujiuza halafu wanaketa mapovu yao hapa. Ndiyo kanumba aliondoka na bongo movie yote bila kujali kama ni Freemason au siyo, bongo movie acheni ujinga leteni movie zenye kichwa na miguu na siyo huo utumbo wenu. Bora tuendelee kula series za majuu. Tena mimi ndiyo huwa sijaribu kabisa maupuuzi yenu ya bongo mavi
 
Kweli kabisa ley, hata juzi tuliona baadhi ya wabunge waliokuwa wakimponda kikwete wakimshangilia bungeni na kutamka tumekumiss, lkn ndo waliosema serikari ya jk legelege,dhaifu,wa nataka rais wakuinyoosha nchi, Nikweli binadam mmoja ana roho saba. Bongo move simamieni na kudai haki yenu kwani haki haiombwi ila hudaiwa.
Kwa sasa hakuna kitu tusiwe tunapindisha maneno, sio wote ambao hatukumuunga mkono Kanumba wale wachache waliosema ivo ndio amewajumuisha ila kiukweli Kanumba alikuwa bora sana tena sana
 
Huhitaji kumfahamu ni nani bali ujumbe wa kweli umefika japo simfahamu na siangalii movie zake lakini alichokisema ni cha kweli. Mimi nitaenda mbali hata Lowasa tulimuita FISADI lakini baadhi yetu wanamuona LOWASA yuleyule ambaye hajafanya lolote lile la kujisafisha na huo uliosemwa UFISADI leo tunasema ni rais wa mioyo....Na hata Magufuli tunayemsema hajui kiingereza akimaliza muda wake tutamshangilia pia hapo ndipo ubaya wa TAIFA lilojaa wanafiki kila kona utakapoliona...........

Jibu swali, unafikiri mi ntasoma povu lote hili?
 
Kwenye jumuia hayo huwa hayakosekani! Kusemwa vizuri au vibaya ni kama utamaduni..., na hufanywa zaidi na watu wenye akili ndogo!!
 
Pole sana Ray, uliishi kwa mbeleko ya the late great Kanumba. Baada ya kuondoka kakuacha na adhabu ya kunywa maji
 
halafu wewe ray mambo yakujiita the greatest uache!!
we ujiite the greatest kwa muvi gani hasa? au huko kusema neno pumbaaavuu kila movi.
kama wewe the greatest sasa akina denzel au kiefer sutherland a.k.a jack buer wajiitaje? maana hawa muvi zao zapendwa dunia nzima wakati ww hata hapo Uganda Hawakutambui
 
Back
Top Bottom