Ray C abadili msimamo kuhusu mwanaume wa kumuoa, asema wanaume wa mitandaoni hamna kitu

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
Ray C anaweza kuwa amezivunja roho za wanaume zaidi ya 500 waliojipanga mstari kujibu ofa yake aliyoitangaza kwenye Instagram kuwa anatafuta mume.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bongo5 Ray C amesema kuwa mume mwema hatafutwi kwenye mitandao bali huletwa na mwenyezi Mungu.

"Huo ulikuwa utani tu," amesema Ray C. "Nilikuwa nataka kuwafurahisha kidogo watu wangu wa Instagram. Watu wengi sana, nimepata simu nyingi kweli kweli. Nimepokea zaidi ya simu 500 mpaka saa sita usiku.

Kwahiyo nimeona mashabiki wangu bado wapo, wananipenda sana," amesema. "Hapana sina mpango wa kuolewa. Mume mwema anatoka kwa Mungu, huwezi kusema unatangaza.

Mume mwema anatoka kwa Mungu nikimpata mtasikia, sasa hivi sipo kwenye mahusiano, sina mtu yoyote."
 
Ray C anaweza kuwa amezivunja roho za wanaume zaidi ya 500 waliojipanga mstari kujibu ofa yake aliyoitangaza kwenye Instagram kuwa anatafuta mume.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bongo5 Ray C amesema kuwa mume mwema hatafutwi kwenye mitandao bali huletwa na mwenyezi Mungu

“Huo ulikuwa utani tu,” amesema Ray C. “Nilikuwa nataka kuwafurahisha kidogo watu wangu wa Insta. Watu wengi sana, nimepata simu nyingi kweli kweli. Nimepokea zaidi ya simu 500 mpaka saa sita usiku.

Kwahiyo nimeona mashabiki wangu bado wapo, wananipenda sana,” amesema.

“Hapana sina mpango wa kuolewa. Mume mwema anatoka kwa Mungu, huwezi kusema unatangaza.

Mume mwema anatoka kwa Mungu nikimpata mtasikia, sasa hivi sipo kwenye mahusiano, sina mtu yoyote.”

Hapo mbona promo iko pale pale ila kabadili style yakutokundika vigezo lakini bado anawahitaji hebu vijana changamkieni fursa: :D:D
 
Ngoja na mimi nitangaze kuwa ninapenda wadada wazuri wenye mvuto, kigezo cha wao kunikubali kitajileta baadaeeeeeeeee.
 
Khaa!! Ray c alikuwa zamani bana enzi zile yuko mawingu fm. Tulikuwa tunakaa juu ghorofan tunamscan na darubini anavyojinyonganyonga mtaa wa samora akienda kazini. Na hii si kesi kwani imepita miaka mingii tu
 
Kila mwanadamu anahitaji faraja ni tendo la kiasili mno, simu 500 alizopata zimemfariji mno kama alivyokiri mwenyewe... Na huu si utani kama anavyotaka kutuaminisha bali ni hisia za upweke zimemzonga zikapitiliza mpaka akaamua kuzitoa
Angepewa ufahamu wa ziada kati ya hao 500 yupo wa kumfaa lakini tayari ameshakejeli kwa kuwaita wanaume wa mtandaoni wakati kiuhalisia mitandao haina wanaume
NB: Asingepata huo mrejesho angeumwa
 
Aliuchezea sana mda wake wa kumpata mtu sahihi, asubiri bwana aliyeacha mke
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom