Rav 4 kilitime inagonga, miguu ya mbele nimebadilisha shockup na stablizer link lakini bado inagonga

super cup

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
212
91
Rav 4 kilitime inagonga, miguu ya mbele nimebadilisha shockup na stablizer link lakini bado inagonga, naombeni msaada wadau tatizo ni nini?
 
inagonga wapi, engine au huko chini kwenye shock ups?

maana bora igonge huko chini kuliko kwenye engine! kama ulishaicheleweshea service ndo zake hizo,kutafuna piece bearing,kusaga block baada ya chujio kuziba na kuzuia engine kufikiwa na vilainishi.

Huwa ni tatizo kubwa sana ambapo lazima ishushwe engine either kubadilisha nilivyovitaja juu au kuweka engine nyingine! anyway omba liwe tatizo la hizo shock ups ila siyo engine utaiona gari chungu
 
Rav 4 kilitime inagonga, miguu ya mbele nimebadilisha shockup na stablizer link lakini bado inagonga, naombeni msaada wadau tatizo ni nini?

inagonga wapi, engine au huko chini kwenye shock ups???

maana bora igonge huko chini kuliko kwenye engine! kama ulishaicheleweshea service ndo zake hizo,kutafuna piece bearing,kusaga block baada ya chujio kuziba na kuzuia engine kufikiwa na vilainishi,....huwa ni tatizo kubwa sana ambapo lazima ishushwe engine either kubadilisha nilivyovitaja juu au kuweka engine nyingine! anyway omba liwe tatizo la hizo shock ups ila siyo engine utaiona gari chungu
Inagonga kwenye miguu boss, cjui tatizo litakuwa ni nini.
 
Hakuna kitu nachukia kama gari ikianza makorokoro ya matengenezo. Mbaya zaidi unakutana na fundi hajui tatizo la gari atakuchaji ufundi na atakwambia na spea za kubadilisha.

Halafu ukitoka hapo tatizo la gari bado liko palepale na hela zimekutoka.

Kungekuwa na fundi gereji ambae ni muaminifu hakupigi cha juu.... unamuachia gari anakurudishia iko poa na pesa anakuchaji sawa na tatizo la ufundi. Wangeingiza hela sana ila sasa looh kichefuchefu.

Pole mwaya mtoa mada, hapa atokee fundi gari anayejua magari kwelikweli akusaidie laah mwenye kujua fundi akupe namba.
 
Rav 4 kilitime inagonga, miguu ya mbele nimebadilisha shockup na stablizer link lakini bado inagonga, naombeni msaada wadau tatizo ni nini?
mwambie fundi wako acheck steering rack kama ina tatizo lolote maana ikiisha huwa inagongagonga sana na unaweza ukatafuta ugonjwa usione
 
Aisee acha ni kacheck kesho, maana gari haina, raha kabisa.
Tairi ya gari inaunganishwa na body na vitu vingi
1. control arms/wishbone-hizi zina bushes,bush zikiisha utasikia matairi yanagonga ukiingia barabara mbovu.

2. ball joints-zikichoka gari itagonga ukichelewa zinachomoka.

3.stabilizer link zikichoka nazo zinagonga.

4.stabilizer bar-hii ina bush,zikiisha gari inagonga vibaya sana.

5.tie rod/rack ends zikichoka nazo gari utaichukia
6.top mounts za shock absorber hizi zikiisha gari inagonga unaweza ukanunulishwa shocks mpya!

7.shocks zikiisha gari inakita haigongi,ikigonga huwa ni mounts.

Kwahio kugonga kwa gari yako kunaweza kusababishwa na moja kati ya hivyo hapo juu.
 
Tairi ya gari inaunganishwa na body na vitu vingi
1.control arms/wishbone-hizi zina bushes,bush zikiisha utasikia matairi yanagonga ukiingia barabara mbovu
2.ball joints-zikichoka gari itagonga ukichelewa zinachomoka...

Another observation.
 
Hakuna kitu nachukia kama gari ikianza makorokoro ya matengenezo. Mbaya zaidi unakutana na fundi hajui tatizo la gari atakuchaji ufundi na atakwambia na spea za kubadilisha...

mafundi wajinga sana, kuna mahala siku moja fundi mmoja ananiambia tairi inalika upande mmoja afanye allignment yaan gari ilikuwa inakatika viuno kila ikifka speed 120, ilinisumbua karibu mwaka ndio mtaalam mmoja akairudisha katika normal yaan kichefuchefu kweli
 
Mkuu tatizo lilikuwa nn?
 
Nisaidie kumpata huyu mtaalamu. Nina shida sawa na yako ilivyokuwa.
 
Mbona mnatutukana sana mafundi bila sababu
Ukienda pale muhimbili unamkuta daktari anampima ndugu kila ugonjwa na dawa anakununurisha kwa bei mbaya na mwisho wa siku doctor anaferi mgonjwa wako unamtoa muhimbili unampeleka kwa babu kijiji anarudi bomba kapona kabisa mbona uwa amuwatukanagi madaktari kwa kushindwa kugundua ugonjwa na huku anakutia hasara ya kukununurisha dawa.

Ufundi auna tofauti na udaktari.
 
Tairi ya gari inaunganishwa na body na vitu vingi
1.control arms/wishbone-hizi zina bushes,bush zikiisha utasikia matairi yanagonga ukiingia barabara mbovu
2.ball joints-zikichoka gari itagonga ukichelewa zinachomoka...
Prondo uko vizuri mzee baba nakuelewa sana tuu
 
Back
Top Bottom