Ratio: Kapuya na waliopoteza kazi 48,000!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Na Waandishi Wetu

SERIKALI imesema Watanzania 48,000 wamepoteza ajira katika sekta rasmi kutokana na kuporomoka kwa uchumi duniani.


Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Prof Juma Kapuya alisema hayo jana wakati akijibu maswali ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika kikao chao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


“Takwimu hizi nina uhakika nazo ndugu wajumbe ninazo ofisini kwangu, tayari Watanzania 48,000 wamepoteza ajira kutokana na tatizo hilo," alisema Kapuya.


Alifafanua kuwa takwimu hizo ni zile zinazohusu sekta rasmi tu, kwa sababu ndio sekta ambayo ni rahisi kuweza kupima utendaji wake.


Kwa mujibu wa Kapuya, miongoni mwa sekta zilizoathirika ni ya nishati na madini ambako uwekezaji umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kuporomoka huko kwa uchumi duniani kulikoanzia na kuyumba kwa taasisi za kifedha kwenye mataifa tajiri duniani.


Alisema, kuna kampuni moja ambayo hakuitaja jina ilikuwa tayari inakusudia kufanya uwekezaji wenye thamani ya Dola 150 milioni za Kimarekani, lakini imeahirisha kutokana na athari za mtikisiko huo.


Mapema mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alisema kuporomoka huko kwa uchumi kulisababisha kampuni ya Xstrata ya Canada kuahirisha mpango wake wa kuchimba madini Kabanga, mkoani Kagera ambao ungetumia Dola 165 milioni za Kimarekani.


Kikwete pia alisema kampuni ya Century Aluminium ya Marekani ilimtaarifu kuwa imeahirisha mradi wake wa Dola 3.5 milioni wa madini kutokana na kuyumba huko kwa uchumi wa dunia.


“Ndugu wajumbe uwekezaji huu ungetoa ajira nyingi kwa vijana wetu lakini kutokana na athari za mtikisiko wa kiuchumi na kushuka kwa bei ya baadhi ya madini kampuni hiyo imeahirisha,” alisema Kapuya ambaye mapema mwaka huu aliwahi kusema kuwa serikali imefanikiwa kutengeneza ajira milioni moja.


Alifafanua kuwa sekta nyingine ambayo imeathirika na kuanguka huko kwa uchumi wa dunia ni ya biashara ambayo usafirishaji wa bidhaa za ndani kwenda nje umeanguka.


“Ndugu wajumbe oda za mazao ya pamba, kahawa na chai zimepungua katika masoko ya nje, huku oda za katani zikipungua hadi kufikia asilimia sifuri,” alisema Kapuya.


Kapuya alisema kuwa maendeleo ya sayansi na teknolojia pia yameathiri maendeleo ya ajira kwa Watanzania katika sekta rasmi na baadhi ya makampuni kujiingiza katika sekta zisizo rasmi kwa lengo la kukwepa kodi.


Kufuatia hali hiyo, Waziri Kapuya alisema serikali ina mpango wa kukutana na wawekezaji wa sekta rasmi ili kuzungumza nao kuhusu namna ya kuondoa tatizo hilo.


“Kwanza tutawashauri watafute mbinu nyingine za kukabiliana na mtikisiko wa kiuchumi badala ya kukimbilia kupunguza wafanyakazi na kuwaomba kuwa hiyo iwe ni hatua ya mwisho kabisa,” alisema Kapuya.


Alisema watawashauri wafanyakazi kutumia njia za busara wakati wa kudai maslahi yao ili kutosababisha waajiri wao kuwafukuza kazi.


Wakati Waziri Kapuya akitoa takwimu hizo, kampuni ya Wembere Shipping ya jijini Dar es Salaam, imekusudia kuwapa likizo isiyokuwa na malipo wafanyakazi 30 kutokana na tatizo hilo.


Msimamizi wa fedha wa kampuni hiyo, Beatrice Natianota alithibitisha suala hilo na kusema limetokana na kuanguka kwa uchumi wa dunia


“Hebu angalia makampuni makubwa ya huko nje yanawapunguza wafanyakazi wake, iweje kwa kampuni yetu ambayo ni ndogo sana,” alisema Beatrice.


Katika hatua nyingine, serikali imeunda kamati ya watu 10 kuchunguza athari za mtikisiko wa uchumi duniani katika sekta ya utalii na kuweka mikakati inayofaa kuchukuliwa kukabiliana na tatizo hilo.


Tanzania imechukua hatua hiyo wakati ambapo nchi jirani ya Kenya tayari imechukua hatua za kukabiliana na mtikisiko huo wa kiuchumi kwa kushusha kiwango cha ada za shughuli za utalii.


Akitangaza uamuzi wa kuunda kwa kamati hiyo jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga alisema kuwa serikali haiwezi kuchukua uamuzi sawa na wa Kenya kwa sababu haina vigezo vinavyothibitisha kuwa sekta ya utalii nchini imeathirika.


Alisema kuwa watalii waliofika nchini mwaka jana ni 750,000, idadi ambayo inaonyesha kuwa sekta ya utalii inaendelea kukua, lakini akakiri kuwa baadhi ya makampuni binafsi yanayoendesha shughuli za kitalii yametoa malalamiko kuwa yameanza kuathirika.


Aliwataja walioteuliwa kwenye kamati hiyo kutoka sekta binafsi kuwa ni Richard Rugimbana (Chama cha Makampuni ya Utalii Tanzania-TCT), Charles Dobie (Chama cha Hoteli Tanzania-HATI), Michael Allord (Chama cha Wawindaji Tanzania-TAHOA) na Abdul Samad Ahmed (Chama cha Wawekezaji Zanzibar-ZATI).


Kutoka serikali ni Amant Macha (Bodi ya Utalii Tanzania), Bernard Murunya (Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro-NCAA), Erasmus Tarimo (Idara ya Wanyamapori), Maria Mmari (Mkurugenzi wa Utalii) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa-Tanapa ambaye Mwangunga hakumtaja jina.


Habari hii imeandaliwa na Salim Said, Peter Edson na Leon Bahati

Wazo: Kuna kitu hakiko sawa kwenye hizo takwimu kwani mmomonyoko wa kiuchumi hauna hata miezi sita na miezi mitatu uliyopita serikali ilisema hautatugusa.. ina maana watu hao karibu hamsini elfu wamepoteza kazi (sekta rasmi) ndani ya miezi hii mitatu au minne hivi.

Hawa watu walikuwa wameajiriwa wapi? Isije kuwa wanaposema "ajira" wanazungumzia wale ambao wangeweza kuajiriwa kwenye sekta rasmi?
 
Hii inanikumbusha katuni moja iliyochorwa hivi karibuni, kitu kama sugar dadi anawambia sugar baby wake kwamba hawezi kumkidhi mambo ya shopping kutokana na muanguko wa uchumi wa dunia, watu watashindwa hata kufua nguo za ndani kutokana na muanguko wa uchumi wa dunia, si kila kitu kimeungana?

Waziri hatakiwi kujibu swali na kusema takwimu zipo ofisini, sema kati ya 48,00 hao 5 walikuwa Dar-es-salaam stock exchange na uchumi wa dunia umewahusu hivi, wengine walikuwa Citibank na hili lina apply hivi.

Siyo mmeshindwa kuendeleza mbuga za wanyama, watalii walishaanza kukata mguu tangu zamani, ajira zimeota mbawa leo mnasingizia uchumi wa dunia.

Si kikwete alisema hatubadilishi kitu, sasa tume ya watu 10 ya nini? Na kwa nini iundwe tume wakati kuna watu kibao wizarani? Kazi zao nini?
 
Last edited:
Tume, tume. Kazi za hawa akina waziri ni nini, kama sio hizo hizo za akina tume?

MMwanakijiji,
Hivi unazo nukuu za hawa jamaa wa Sirikali waliposema kuwa Tanzania haitaadhirika na misukosuko ya dunia? Ni nani alisema na wapi. Itasaidia kuwabana, na kuwazuia kubwatuka hovyo. Asante
 
Swala hili halieleweki, kama ajira nyingi zimepotea, watu wanaokutano mbona wengi wako kwenye sekta ya UTalii. Hii itakuwa na kamati ya ajabu ukiangalia uchumi wenyewe umeshuka na hata watalii watapungua.
 
Give me a break!!!Tume za nini kila siku tume tume huu ni ujinga. Viongozi wa tanzania wamelogwa wote na aliyewaloga alikufa siku nyingi.kwani ninyi hamjui kama ni uzembe wenu umekithiri katika sekta ya utalii na ufisadi kwa kwenda mbele. Kapuya kapuyange huko usituleteee za kuleta hapa kama hazimo vile. Ndio uchumi umeporomoka lakini isiwe sababu ya watu wengine kujitajirisha na hizi tume mnazounda kila siku fungueni miradi watu waliopoteza kazi wapate ajira kwa pesa ambayo mnataka kulipana na tume uchwara.
 
Tume tume!! tume!! tume!! tume!! tume!! Lazima ziundwe ili watu wapate utume wa kula!!
 
Back
Top Bottom