Ratiba za mabasi ya mwendokasi pasua kichwa!

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,961
2,139
Muda huu karibu saa moja kasorobo asubuhi ndiyo napita maeneo ya stand ya Jangwani.

Njia nzima tangu Kimara hadi hapa Jangwani stand vituo vimejaa watu kwa mamia kama wako kwenye msiba.

Mabasi yanayoenda Kimara hayawachukui na yakitoka Kimara yanakuwa yamejaa yanawapita tu.

Niko najiuliza hawa waendeshaji wa hii kampuni ya mwendo kasi kwanini wanawatesa abiria wao hivi? Sumatra wako wapi? Uongozi wa jiji uko wapi? Wizara iko wapi?

Ushauri wa bure, wizara, sumatra, jiji wawasimamie kikamilifu hawa mwendo kasi kwani ni majanga matupu.

Wanawatesa sana abiria wakati daladala bado zipo, je zikiondoka si itakuwa majanga?

Kuna siku watu watachoka wataamua kufanya maamuzi mabaya. Wanaweza piga watumishi, kuharibu miundo mbinu au kuvuruga utumiaji wa barabara.

Nawasilisha
 
Ni kweli kwa leo wamewaweka abiria zaidi ya saa na ushee vituoni.Mimi kwa mfano toka saa12 niko Kimara mwisho,nimepanda gari saa 1:15 hii si haki watu tulikuwa wengi mno, huku magari yanayoanzia mbezi yakishusha abiria.

Dart mnatakiwa kujipanga sana kuanzia asubuhi mapema magari yawe mengi,watu wamelalamika sana kwa leo.Mtakuja kuharibu hata miundo mbinu yenu.

Kwa mfano leo,kimara mabomba yakuturemshia maji yameng'oka kwa watu kugombania na vilevile ajali inaweza kutokea.

Dart mbadilike msisingizie jumatatu watu huwa wengi vituoni.
 
Yaani ni shida toka saa 11:45 niko Kimara kituo kimejaa abiria, mabasi hakuna linakuja moja moja likiwa limeshajaa abiria, hatujui nini kimetokea leo ni nimeondoka kimara saa 01;45, UDART tatizo nini? utaratibu wenu haueleweki kabisa mabasi yanaongozana kama nyumbu yakija kimara ni yote yakiondoka ni yote, wekeni utaratibu mzuri pia sio vibaya mkaomba ushauri kwa kakaangu Mwaibula
 
Watu walivyopiga kelele kuwa UDA 'imeibwa' mliwabeza na hata meya alivyokuja na wazo la kuirejesha UDA jiji mkaona ni siasa, hayo mnayoyaona ni baadhi tu ya matokeo ya hizo kelele. Walisema hiyo kampuni iliyojivika huu mradi haina uzoefu lakini pia pesa walizotumia kujenga huu mradi zingelielekezwa kwenye ujenzi wa kawaida wa barabara matokeo yangelikuwa mazuri zaidi ya kilichofanyika.
 
sipandi tena magari haya, juzi waliniweka kwenye kituo cha Msimbazi dk 40 mpaka nikachelewa Basi la Mkoani.
Kadi yao nimewapa watoto.......wachez.............
 
Poleni, sasa rudini kwenye daladala muwaachie hayo mabasi yao wapakie dagaa wa ferry
 
Hii bila shaka ni public service na si mradi wa MTU binafsi... Ukilenga zaidi kukusanya faida badala ya Huduma basi hill nalo ni JIPU
 
Najiuliza siku madereva wa mwendo kasi wakigoma na daladala hazipo mjini
 
Kuna kauli moja aliongea mfanyakazi WA ulinzi pele ferry anadai kuwa wameamuwa kutusaidia lakini tunashindwa kujipangia utaratibu WA kuingia kwenye bus.. Na hiyo kauli sio mara moja sasa najiuliza kuwa Kama madereva wanaacha abiria anapita mtupu.. Lile basi nila babaake au mamaake.. Uongozi uko wapi au mshazipata kazi matako kuanza kulia beats.. Mnatuchosha sana kwenye vituo vyema.. Wabadilike wakumbuke isingekuwa huu mradi wangekuwa wanaomba poo tu kitaani.. Wamepata kazi wanaleta bwebwe
 
Wanaosimamia huo mradi wamekosa 'organizational skills'.
Tena ikiwezekana daladala ziongezeke mjini, huu usafiri sio reliable tena.
 
Back
Top Bottom