Ratiba ya ziara ya Tundu Lissu barani Ulaya na Marekani hii hapa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,451
215,245
Tundu Lissu ambaye ripoti za kuaminika zinaonyesha kwamba ndiye Mwanasheria bora kabisa kuwahi kuwepo kwenye eneo la Maziwa Makuu tangu kuumbwa kwa mbingu na ardhi , ataanza ziara ndefu ya kimkakati kwenye nchi za Ulaya na Marekani ili kuieleza dunia kilichotokea kwenye shambulio lake , wahusika wote na waliowatuma kutenda uovu ule na hali ya kisiasa ilivyo nchini Tanzania kuanzia muda huo hadi sasa

Hii ndio ratiba ya ziara yenyewe :
.......... .. .......................................
Kuanzia January 14 amealikwa na Shirika la utangazaji la BBC mjini Brussels ambapo pamoja na kuongea na BBC pia imeelezwa kwamba amepata mwaliko mwingine wa kuonana na viongozi wa juu kabisa wa jumuiya ya Ulaya ( EU )

Baada ya kumaliza hili taarifa zinaonyesha kwamba amepewa mwaliko mwingine mapema February wa kuonana na maofisa wa ngazi ya juu kabisa wa serikali ya Marekani huko Washington , ambako kutakuwa na mazungumzo yatayochukua angalau wiki moja

Taarifa zaidi kuhusu ziara hii muhimu ya Mh Tundu Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema itaendelea kuboreshwa kwa kadri tunavyoletewa habari za ziara yake kwenye nchi mbalimbali.

Mungu mbariki mtumishi wako Tundu Lissu

UPDATES
...................
1.BBC : HARD TALK , Tayari
2.DW , Tayari
3.USA , Ndio habari inayobamba
4................

Kaeni mkao wa kula .
 
Sifurahishwi na Tukio la tundu Lisu ila pia huwa sifurahishwi sana hii tabia ya waafrika kuwasubiri wazungu waje kutatua mambo yetu wakati ni rahisi na tunaweza ila hatutaki tu, mgogoro wa Zanzibar tulisimama kidete wakati ule mpaka tukatengeneza serikali ya umoja wa kitaifa hali ikawa shwali, lakini kwasababu shetani anapenda kula nyama basi tumeuwa yale makubaliano na kwa kuwa sisi huwa mpaka kichafuke ndo tunatafuta suluhisho na hatuamini katika kinga basi mengi huwa tunasubiri yahatibike.
 
Tundu Lissu ambaye ripoti za kuaminika zinaonyesha kwamba ndiye Mwanasheria bora kabisa kuwahi kuwepo kwenye eneo la Maziwa Makuu tangu kuumbwa kwa mbingu na ardhi , ataanza ziara ndefu ya kimkakati kwenye nchi za Ulaya na Marekani ili kuieleza dunia kilichotokea kwenye shambulio lake , wahusika wote na waliowatuma kutenda uovu ule na hali ya kisiasa ilivyo nchini Tanzania kuanzia muda huo hadi sasa

Hii ndio ratiba ya ziara yenyewe :
.......... .. .......................................
Kuanzia January 14 amealikwa na Shirika la utangazaji la BBC mjini Brussels ambapo pamoja na kuongea na BBC pia imeelezwa kwamba amepata mwaliko mwingine wa kuonana na viongozi wa juu kabisa wa jumuiya ya Ulaya ( EU )

Baada ya kumaliza hili taarifa zinaonyesha kwamba amepewa mwaliko mwingine wa kuonana na maofisa wa ngazi ya juu kabisa wa serikali ya Marekani huko Washington , ambako kutakuwa na mazungumzo yatayochukua angalau wiki moja

Taarifa zaidi kuhusu ziara hii muhimu ya Mh Tundu Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema itaendelea kuboreshwa kwa kadri tunavyoletewa habari za ziara yake kwenye nchi mbalimbali.

Mungu mbariki mtumishi wako Tundu Lissu
Awabariki na hao mabwana zenu
 
163 Reactions
Reply
Back
Top Bottom