Ratiba ya vikao vya uteuzi wa mgombea wa CHADEMA Arumeru Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ratiba ya vikao vya uteuzi wa mgombea wa CHADEMA Arumeru Mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Tumaini Makene, Feb 28, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]
  TAARIFA KWA UMMA[/FONT]


  [FONT=&amp]RATIBA YA VIKAO VYA UTEUZI WA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI[/FONT]

  [FONT=&amp]Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inatoa taarifa kwa umma kuwa muda wa uchukuaji na urejeshaji fomu kwa wanachama wa CHADEMA wanaowania uteuzi wa chama kugombea ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki ulimalizika rasmi Februari 25, 2012.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Itakumbukwa kuwa sekretarieti ya chama ilitoa muda wa kutosha kwa shughuli hiyo, tangu Februari 14 hadi Februari 25, 2012, ambapo ndani ya muda huo, jumla ya wagombea saba walijitokeza kuchukua na kurejesha fomu.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Wagombea hao ni; [/FONT][FONT=&amp]Anna Mghwira, Godlove Temba, Joshua Nassari, Samueli Shamy, Yohane Kimuto, Rebecca Magwisha na Anthony Musami.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kukamilika kwa shughuli hiyo bila kuwepo malalamiko yoyote rasmi kwa mujibu wa katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama miongoni mwa wagombea, sasa kunatoa fursa kwa mchakato huo kufuatiwa na vikao vya chama kwa ajili ya uteuzi wa jina la mgombea.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kama ilivyoelezwa awali, vikao vya chama vinavyohusika na uteuzi wanachama waliochukua fomu na kutimiza masharti kadri inavyoelekezwa, vitakaa kufanya uteuzi na hatimaye kumpata mgombea mmoja, ambaye chama kitamsimamisha na kumsimamia kuwania jimbo hilo, ili ashinde na kuongeza nguvu ya wapambanaji ndani ya wabunge, kuwawakilisha Watanzania.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Hivyo kwa kufuata taratibu, kanuni na katiba ya chama kukamilisha mchakato huo kama ilivyo ada ya CHADEMA, Mkutano Mkuu wa Jimbo unatarajiwa kuketi kesho Jumatano, Februari 29, 2012, kwa ajili ya kura za awali (maoni), kisha kitafuatia Kikao cha Kamati ya Utendaji Wilaya ya Meru, kitakachofanyika Machi 1, 2012, kwa ajili ya kufanya uteuzi wa awali.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Kamati Kuu ya CHADEMA inatarajiwa kuketi mjini Arusha, Machi 3, 2012 kwa ajili ya kufanya uteuzi wa mwisho wa jina la mwanachama mmoja atakayepeperusha bendera ya CHADEMA, kuwania kuwatumikia watu wa Arumeru Mashariki.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mpaka sasa mipango ya maandalizi ya awali kuhakikisha CHADEMA inaibuka mshindi katika uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, inaendelea vizuri, ambapo makamanda wote wana ari ya ushindi ili kuongeza idadi ya wapambanaji na utumishi bora ndani ya bunge, kwa maendeleo watu na maslahi ya taifa zima.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Kwa umakini na uimara ambao kimeendelea kuudhihirisha katika kuwatumikia na kuwawakilisha Watanzania kupitia majukwaa mbalimbali, tangu Watanzania walipoonesha dalili zote za kukiunga mkono na kukiamini kuwa kinaweza kupewa dhamana ya uongozi wa nchi hii, ari ya chama hiki imezidi kuongezeka siku hadi siku, kikijiandaa kupokea dhamana kubwa zaidi kadri siku zinavyokwenda. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Hivyo katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki, wanachama na wananchi kwa ujumla wazingatie kwamba CHADEMA itaendelea kutimiza dhima yake ya kuhakikisha uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni dhabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Imetolewa leo Dar es Salaam, Februari 28, 2012 na;[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Tumaini Makene[/FONT]

  [FONT=&amp]Afisa Habari wa CHADEMA[/FONT]
   
 2. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Makene wagombea wako sita au saba?
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mimi binafsi napenda J.Nassari apitishwe kuwa mgombea wa CDM.
   
 4. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  nassari joshua
   
 5. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #5
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Asante kamanda. Concern noted and action taken mkuu. Pamoja sana.
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nasari akabiziwe pendera aipeperusha...
   
 7. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #7
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Me to.

  [​IMG] vs [​IMG]
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  yeah,,angalau jama hatakuwa mgeni kabisa machoni kwa wana arumeru na nadhani,, still yuko competent huyu jamaa!
   
 9. ZALEOLEO

  ZALEOLEO Senior Member

  #9
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  apewe huyo alotoka ccm
   
 10. K

  KakaNanii JF-Expert Member

  #10
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hapana ubishi Nassari joshua ndo muda wake huu.avune alichopanda 2010.
   
 11. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #11
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hata bila kufuata utaratibu? Kama ndio hivyo hata hizo ratiba za vikao hazina maana.
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Joshua Nassary for Arumeru
   
 13. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #13
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nami pia namuunga mkono huyu dogo
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Crashwise,

  Mkuu,hapa kidogo sijakuelewa.Akabidhiwe kivipi?si kuna uchaguzi wa kura za maoni mkuu? do you mean akabidhiwe kama hisani au kwa kufuata mchakato mzima wa demokrasia kwa uwazi?
   
Loading...