Elections 2010 Ratiba ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa: Tarehe Muhimu

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,360

Tangazo limetolewa kwenye Daily News ya tarehe 25 Julai, 2009 kuhusiana na ratiba ya uchaguzi wa Serikali za Mtaa kwa mwaka 2009. Uchaguzi huo utafanyika tarehe 25 Oktoba, 2009.

Baadhi ya tarehe muhimu

6 Septemba, 2009
kutangaza majina na mipaka ya mitaa
10 Septemba, 2009
Uteuzi wa wasimamizi wasaidizi
4-24 Septemba, 2009
Uandikishaji wa orodha ya wapiga kura
2-5 Oktoba, 2009
Uteuzi wa wagombea
15-24 Oktoba, 2009
Kampeni za uchaguzi
25 Oktoba, 2009
Kupiga kura


Masharti muhimu

1. Wapiga kura watatakiwa kujiandikisha katika Rejista ya wapiga kura itakayoandaliwa siku ishirini na moja kabla ya siku ya uchaguzi.
2. Uchaguzi utafanya kwa kutumia karatasi maalum za kupigia kura.
3. Kura zitapigwa na kutumbukizwa kwenye masanduku ya kupigia kura.
4. Uchaguzi utafanyika katika ngazi ya kitongoji na mitaa sehemu ya faragha na hakutakuwa na mikutano ya uchaguzi katika ngazi za vijiji, mitaa na vitongoji.
5. Wagombea wote wa nafasi mbalimbali za uchaguzi watatakiwa wawe wanachama na wadhaminiwe na Chama cha Siasa chenye usajili wa kudumu.

Sisi kama Raia tunalijua hili, je, tumejiandaa na kujitayarisha vipi kwa uchaguzi huo? Je twajua umuhimu wa uchaguzi huo? Je, uchaguzi huo una athari gani kwenye uchaguzi mkuu wa 2010?

NB: Hivi magazeti mengine ya Kiswahili hili tangazo limetoka? Ni lini? Naomba mnijuze.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom