Ratiba ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa: Tarehe Muhimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ratiba ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa: Tarehe Muhimu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngambo Ngali, Jul 28, 2009.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160

  Tangazo limetolewa kwenye Daily News ya tarehe 25 Julai, 2009 kuhusiana na ratiba ya uchaguzi wa Serikali za Mtaa kwa mwaka 2009. Uchaguzi huo utafanyika tarehe 25 Oktoba, 2009.

  Baadhi ya tarehe muhimu

  6 Septemba, 2009
  kutangaza majina na mipaka ya mitaa
  10 Septemba, 2009
  Uteuzi wa wasimamizi wasaidizi
  4-24 Septemba, 2009
  Uandikishaji wa orodha ya wapiga kura
  2-5 Oktoba, 2009
  Uteuzi wa wagombea
  15-24 Oktoba, 2009
  Kampeni za uchaguzi
  25 Oktoba, 2009
  Kupiga kura


  Masharti muhimu

  1. Wapiga kura watatakiwa kujiandikisha katika Rejista ya wapiga kura itakayoandaliwa siku ishirini na moja kabla ya siku ya uchaguzi.
  2. Uchaguzi utafanya kwa kutumia karatasi maalum za kupigia kura.
  3. Kura zitapigwa na kutumbukizwa kwenye masanduku ya kupigia kura.
  4. Uchaguzi utafanyika katika ngazi ya kitongoji na mitaa sehemu ya faragha na hakutakuwa na mikutano ya uchaguzi katika ngazi za vijiji, mitaa na vitongoji.
  5. Wagombea wote wa nafasi mbalimbali za uchaguzi watatakiwa wawe wanachama na wadhaminiwe na Chama cha Siasa chenye usajili wa kudumu.

  Sisi kama Raia tunalijua hili, je, tumejiandaa na kujitayarisha vipi kwa uchaguzi huo? Je twajua umuhimu wa uchaguzi huo? Je, uchaguzi huo una athari gani kwenye uchaguzi mkuu wa 2010?

  NB: Hivi magazeti mengine ya Kiswahili hili tangazo limetoka? Ni lini? Naomba mnijuze.
   
  Last edited by a moderator: Jul 28, 2009
Loading...