Ratiba ya Rais Magufuli ziarani Mbeya na hofu ya usalama yafanya wananchi kukaguliwa

Kwani ni lazima kilichokuwa kinafanywa katika Awamu na Uongozi wa Rais Mstaafu Kikwete ufanywe au ufanyike na katika Awamu na Uongozi huu wa Rais Dkt. Magufuli? Hebu wakati mwingine tuwe tunatumia Viungo sahihi kwa kutuwezesha Kufikiri na siyo vile ambavyo vinatusaidia Kupunguza Mizigo ' Taka ' iliyopo Matumboni mwetu.
Kwani ni lazima kilichokuwa kinafanywa katika Awamu na Uongozi wa Rais Mstaafu Kikwete ufanywe au ufanyike na katika Awamu na Uongozi huu wa Rais Dkt. Magufuli? Hebu wakati mwingine tuwe tunatumia Viungo sahihi kwa kutuwezesha Kufikiri na siyo vile ambavyo vinatusaidia Kupunguza Mizigo ' Taka ' iliyopo Matumboni mwetu.
unaogopa hadi kivuli chako mwenyewe, kunywa maji upunguze presha.
 
Nilitoa ushauri angalau Praise Team iwe na watu angalau wenye elimu kuanzia kidato cha nne! Mnavyojazana darasa la saba D inakuwa ni tabu.
Hata hujui mfumo wa vyama vingi ulianza lini. Naalabuk
 
RC ALBERT CHALAMILA ATOA RATIBA RASMI ZIARA YA RAIS MAGUFULI MBEYA.



Leo majira ya saa 8 mchana, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amekutana na waandishi wa habari ofisini kwake na kutoa ratiba rasmi ya ziara ya Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli katika Mkoa huu.

RC Chalamila amesema Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli atafika Mkoani Mbeya jioni ya tarehe 25/04/2019 kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo Wilaya ya Mbeya jimbo la Mbeya Vijijini.

Tarehe 26/04/2019 pamoja na mambo mengine atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya CCM maarufu kama Rwanda Nzovwe Jijini Mbeya.

Tarehe 27/04/2019 ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Rungwe na Kyela ambapo atasalimiana na wananchi katika eneo la Kiwira, Tukuyu na kufungua kiwanda cha maparachichi, mabweni nk katika chuo cha Ualimu Mpuguso Wilayani Rungwe kisha kuelekea Wilayani Kyela ambako kumejengwa Barabara kisha atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya John Mwakangale Wilayani humo.

Tarehe 28/04/2019 atakuwa katika viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya katika tukio la uapisho wa Askofu Nyaisonga wa Kanisa Katoliki.

RC Chalamila ametoa wito kwa watakaohudhuria sherehe hizo kuingia uwanjani kabla ya saa 4 asubuhi na kwamba kila atakayeingia uwanjani humo atakaguliwa kwa ajili ya usalama.

29/04/2019 ataelekea Wilayani Chunya.

30/04/2019 atafanya ziara Jijini Mbeya na atazungumza na wanazuoni wa vyuo na vyuo vikuu katika eneo la Chuo Kikuu cha sayansi na Teknolojia (MUST).

Tarehe 01/05/2019 atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wafanyakazi (MEI MOSI) zitakazofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

02/05/2019 atamalizia ziara yake katika Wilaya ya Mbeya (Mbeya Vijijini) kwa kutembelea Kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement.

RC Chalamila amewakaribisha wananchi wote kumlaki Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli na amesema mabango yenye tija yasiyo ya uchochezi yanaruhusiwa.
Kumbe mkoa mpya wa Songwe haendi.......
 
Wananchi wanatakiwa kuingia uwanjani saa 4 halafu rais anaingia saa 10, chakula watapewa? halafu huyu ni kipenzi cha wanyonge sasa hofu ya nini mpaka kukaguana au mbeya siyo kwa wanyonge?

Huyu jamaa bwana! 🤣🤣🤣. Anajua kwa nini anaogopa. Manyanyaso yote haya anayotupa lazma aogope.
 
Back
Top Bottom