Ratiba ya Mtanzania msomi kwa siku ya kufanya kazi

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,809
2,000
Wana JF,

Wananchi wote kwa ujumla ni waumini wazuri wa ratiba hii kwa siku nzima, huku wakitegemea mafanikio kuiendeleza nchi yao.

RATIBA YA SIKU MZIMA.
1. Saa Kumi kuamka kuoga na kuanza safari.

2. Saa kumi na moja kufika kituoni.

3. Saa kumi na mbili kufika mjini.

4. Saa 1. kupitia magazeti kwenye vibaraza.

5. Saa 2 kuanza kazi.

6. Saa 3, kujibu facebook, Instagram, E-mail za G-mail, Yahoo.

7. Saa 4. muda wa chai.

8. Saa 5 kufanya kazi kidogo nyingine akiweka mafail pembeni kwa ajili ya kesho.

9. Saa 6 kuwakumbusha wafanyakazi kwenda kuchukua watoto na kuwaanda marafiki, wachuna mabuzi kujiandaa na lunch time.

10. Saa 7 lunch time.

11. Saa 8 kupekua mafail yaliyoachwa na mkurugenzi, au kupokea taarifa mpya ya kufanyia kazi kesho.

12. Saa 9 kufunga ofisi.

Kwa kweli tusipobadilika maendeleo tutayasikia Kenya tu.
 

NdegeMwema

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
249
250
Hayo ni masihara kazini, ni kweli kuna baadhi ya office Uhuru ni mkubwa kama wapo kijiweni. Kama hatutabadilika tutaendelea kuwasifia wenzetu kila uchao!
 

Justinejm

Senior Member
Jul 6, 2015
130
170
Watz wenzangu tunataka mabadiliko lakini huenda hatujawahi kufikiri kuwa hata sie wenyewe ccm imeshatufanya sehemu ya tatizo, hivyo mabadiliko yanatuhusu pia,
 

mizarb

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,399
2,000
Ndo maana tunataka mabadiliko kubadili hali hii, baada ya 25 oct hizo namba 1, 2, 3, 4, 6, 8 hazitakiwepo tena
 

ffoas

Member
Feb 23, 2011
33
95
Hiyo sure kiongozi kabisa bro, nimeshuhudia office nyingi zikifanya kazi kwa style hiyo,tunajikuta kimahesabu tunafanya kazi masaa 2 tuu badala ya masaa yaliyopangwa
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,809
2,000
Hiyo sure kiongozi kabisa bro, nimeshuhudia office nyingi zikifanya kazi kwa style hiyo,tunajikuta kimahesabu tunafanya kazi masaa 2 tuu badala ya masaa yaliyopangwa
Yaani ni shida, saa tano wanawake wote wanasikiliza redio clouds kipindi cha umbea, wakati mwingine wanasoma magazeti ya udaku.
 

ffoas

Member
Feb 23, 2011
33
95
Tatizo letu hatupendi kujituma kwa bidii, tumekuwa wavivu na mizigo,thus why kila siku tunalalamika maendeleo yanachelewa wakati tunayachelewesha wenyewe hiyo ni kutokana na misingi mibovu ya malezi toka kwenye familia mpaka kwenye ngazi ya juu ya kiutawala.
 

hekimatele

JF-Expert Member
May 31, 2011
9,897
2,000
Subiria mabadiliko yafanyike kwanza utashangaa mda wa kutoka ofisini serikalini unakuwa saa 11 jioni. We tulia tu uone.
 

Ubavu

JF-Expert Member
Jun 19, 2012
2,793
2,000
Kuna taasisi moja ya serikali niliwahi kufanyia field mfanyakazi wake wa kwanza huingia kazini saa 2:30 asubuhi. Na kuanzia SAA 6 mchana ni full story mpaka saa 9 alasiri muda wa kurudi nyumbani. Na ukiangalia kuna watu wanalipwa mpaka 2M hapo. Nikajiuliza Tanzania tutafika kweli kwa hali hii ??!!
 

kamandawasua

JF-Expert Member
Jun 6, 2013
323
225
Duh ni ukweli kabisa hatuwezi kuwa na maendeleo kama hatufanyi kwa kiwango chetu cha juu "A game" most people wana play their C game ndo maana kunakuwa na magumashi ya kutosha
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,809
2,000
Duh ni ukweli kabisa hatuwezi kuwa na maendeleo kama hatufanyi kwa kiwango chetu cha juu "A game" most people wana play their C game ndo maana kunakuwa na magumashi ya kutosha
Dar /Mwanza/Arusha watu wengi wanategemea madili tu, wengine wanaita michongo hii yote ni mipango ya wizi watu hatujitumi kufanya kazi, michongo ikiferi tunaanza majungu na kuvizia watu, eti leo nilikuwa nilale njaa afadhali nimekuona unipe hata teni nisepe, wakati hajui kuna bajeti ya home, kinywaji kidogo.
 

kamandawasua

JF-Expert Member
Jun 6, 2013
323
225
Dar /Mwanza/Arusha watu wengi wanategemea madili tu, wengine wanaita michongo hii yote ni mipango ya wizi watu hatujitumi kufanya kazi, michongo ikiferi tunaanza majungu na kuvizia watu, eti leo nilikuwa nilale njaa afadhali nimekuona unipe hata teni nisepe, wakati hajui kuna bajeti ya home, kinywaji kidogo.
Ni ukweli mi mwenyewe nimeacha kazi jana.
Mshahara haugawanyiki afu natumia muda mwingi kazini (45 hours per week). Nikiwa mtaani mishe kibao zinafanyika pesa inaingia mfukoni kwa juhudi ndogo sana. Kuwa financially free unatakiwa uweze kuishi bila kutegemea paycheck.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom