Ratiba ya Mazishi ya Mpigania Uhuru na Muasisi wa TAA, Dokta Vedasto Kyaruzi

Dk Kyaruzi mwanaharakati muhimu wa uhuru asiyetambuliwa na historia Send to a friend
Tuesday, 25 October 2011 11:05

06kyaruzi.jpg
Dk Vedasto Kyaruzi

Midraj Ibrahim
NI jioni majira ya saa 12:00 nikiwa na mwenyeji wangu Method Katikila aliyekuwa akinisaidia kunielekeza baadhi ya wazee walioshiriki kwenye harakati za kupigania uhuru. Tukafika kwenye nyumba iliyopo eneo la Kashai Matopeni, ina mandhari nzuri tofauti na jina la eneo. Tukabisha hodi, akatokea binti akatuambia tusukume geti, tuingie ndani. Tulipingia tukamwambia kuwa tunataka kuonana na Dk Vedasto Kyaruzi, yule bin ti alitukaribisha ndani.

Tunapoingia ndani macho yangu yanakutana na mzee mmoja mwenye mvi nyingi, huku uso wake ukiwa umejawa na furaha ya kupokea wageni, akijihimu kuamka ili tusalimiane akiwa amesimama, lakini inakuwa shida kidogo na mimi namwambia pumzika mzee.
Tunasalimiana huku akionekana mwenye bashasha anaanza mzaha kwa kusema: "Nimemaliza kusali Magharibi sasa nasubiri Ishaa."
Baada ya kupitisha utani wahapa na pale naanza kumweleza nia yangu ya kufunga safari kutoka Dar es Salaam kwamba, nahitaji kuzungumza naye kuhusu harakati za uhuru.
Akionekana wakati mwingine kupoteza kumbukumbu anaonyesha kufurahi kwa sababu anasema kuwa angalau leo katembelewa na watu wanaotaka kufahamu ukweli kuhusu historia ya Tanganyika.
"Nashukuru nafikiri wewe ni mtu wa watatu kuja kunitafuta, kuna watu wawili wali-flight kutoka Marekani kuja hapa, nimezungumza nao mambo mengi, mwingine ni hivi juzi juzi amekuja na sasa wewe. Nashukuru, sasa njoo kesho ofisini kuanzia saa 4:00 asubuhi sina watu wengi," anasema Dk Kyaruzi.

Tunalazimika kukatisha mzungumzo ili kumpa nafasi Dk Kyaruzi apumzike, tulipokuwa tukimuaga akatuomba msaada wa kumnyanyua kwenye kiti ili aweze kutusindikiza, tunamwambia apumzike, anakataa na kusema kuwa hatuwezi kumuacha amekaa ndani.
Tunamnyanyua kwenye kiti, mara anaposimama anatembea mwenyewe, huku akitusimulia kuhusu ujenzi wa nyumba yake hiyo ambayo inaonekana ya kisasa zaidi baada ya kuvunjiwa nyumba yake ya awali kutokana na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba. Anatufikisha kwenye geti na tunaagana.
Kesho yake saa 4:30 asubuhi, tunapiga hodi ofisini kwake, hospitalini anakofanya kazi, takriban kilomita nne kutoka nyumbani kwake. Dk Kyaruzi anasema anatembea kila siku kutoka na kurudi nyumbani kwake hadi kazini.
Tunaingia ofisini kwake anatupatia kitabu cha wageni, tusaini. Kisha naanza kumdadisi kuhusu umri wake na aina ya chakula anachotumia.
"I think now am spending bonus, namshukuru Mungu nina miaka 90 na miezi sita, sijui kuumwa, zaidi natibu watu na sina chakula fulani, kila chakula nakula. Namshukuru Mungu," anasema Dk Kyaruzi.
Sasa naanza kumdodosa jinsi ya ushiriki wake kwenye harakati za uhuru, nabaini kuwa Dk Kyaruzi ni miongoni mwa wanaharakati pengine Mhaya pekee aliyekuwa kwenye harakati hizo sambamba na wazalendo wa Dar es Salaam.
Historia iliyopo kwenye maktaba mbalimbali inamuonyesha Mwalimu Julius Nyerere na washirika wake akina Rashidi Kawawa, lakini siyo akina Dk Kyaruzi. Anaanza simulizi:
"Nilikuwa na (Mwalimu Julius) Nyerere Chuo Kikuu cha Makerere, nilimtangulia mwaka mmoja wakati tukiwa pale tulianzisha vuguvugu la uhuru, lakini mwaka 1948 nikamaliza na kwenda Dar es Salaam kikazi.
"Baada ya kufika Dar es Salaam, kulikuwa kuna Tanganyika African Association (TAA) nikajiunga, lakini ile ya kwetu haikuwa official (rasmi), iliyokuwa official ikaonekana kama inatuogopa wakati huo ilikuwa ikiongozwa na Dk Tsere.
"Baadaye tukaanzisha vuguvugu ndani ya TAA rasmi iliyokuwa ikiongozwa zaidi na wazee, ile ya kwetu ikiwa ni ya vijana wale wazee walikuwa hawaitishi vikao tukaanzisha vuguvugu, lengo letu tukitaka na sisi kutambuliwa.
"Mwaka 1950, sasa Dk Tsere akahamishiwa Tanga, TAA official wakamteua katibu kutoka kundi letu, Abulwahid Sykes, pale tukaona tunaanza kuingia tukamwambia awahi kuitisha mkutano.

"Chama kilikuwa kimezorota. Mikutano ilikuwa haiitishwi kwa sababu chama kilikuwa hakina fedha za kujiendesha. Pale kundi letu tukaona sasa ndiyo muda wa kuingia uongozi wa TAA inayotambulika rasmi.
"Baada ya Sykes kachukua madaraka tukamwambia aitishe mkutano mkuu, akaitisha mkutano mara ya kwanza baadhi ya wazee hawakufika, waliohudhuria wakasema chama hakina President kinakuaje, wakanichagua kuwa President.
"Kwanza kukataa, lakini kundi letu likaona kama limeanza kupata ushindi. Baadaye nikakubali. Nikamwagiza Abdulwahid kuitisha mkutano mwingine. Alipoitisha wale wazee wakaja na kuanza kuhoji aliyenichagua nikawambia katibu mliyemteua nyinyi aliitisha mkutano hamkuhudhuria sasa mnamuuliza nani?
Pale nilikuwa President tayari, wakabaini kwamba wao wana makosa, tukaanza kazi sasa. Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kuandika memorandum kwenda serikalini, mojawapo ya mapendekezo ambayo nakumbuka ilikuwa Serikali iteue kamati ya kuangalia hali ya siasa.
Wakati huo TAA imeshakuwa moja. Kwa kweli karibu mapendekezo yetu yote yalikubaliwa na Serikali. Tulikuwa tumeamua kufanya kazi kwa haraka sana.
Lakini, kwa bahati mbaya Serikali haikufurahia sisi kuunganisha nguvu, ikanipa nafasi ya kwenda kusoma Uingereza mambo ya upasuaji. Nikaitisha mkutano kuwaeleza akina Paul Rupia wakaniuliza unatuachaje? Walikataa. Ikabidi niandike barua kuahirisha kwenda kusoma.

Sasa wakati Mwalimu Nyerere anarudi kutoka Edenburg Uingereza, nikapewa uhamisho kwenda Kingurowira Prison kuwa Medical Officer In-charge. Hapakuwa na kazi za kufanya ni kushinda umekaa tu. Basi, nikamkabidhi u-president lakini kulikuwa na mawasiliano kila siku baina yetu.

Baadaye nilihamishiwa Nzega, halafu Biharamulo na Bukoba, baadaye nikaenda Ulaya kusomea Stashahada ya Utawala.
Tulikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Mwalimu Nyerere, wakati Tanu inaundwa nilikuwa Ulaya, niliporudi likizo nikaenda kumsalimia Mwalimu Nyerere aliponiona sikuwahi kumwona hivyo alikuwa ‘so tense.' Akasema, tutafaulu huku akipiga ngumi juu ya meza.

Nikamuuliza kwa nini? Mwalimu Nyerere akijibu: Watu kama nyinyi ndiyo niliokuwa nahitaji, tutafaulu.Tumeendelea na harakati hadi tukapata uhuru. Lakini siku tunapata uhuru nilikuwa bado Uingereza.

Baada ya siku chache tumepata uhuru nilirejea nchini na kumtembelea tena Mwalimu Nyerere, akaniambia anataka kuniteua niwe balozi nilimwomba niendelee na udaktari kwa sababu kwangu ni wito.
Mwalimu Nyerere aliniangalia akaniambia nipe jina la Mhindi au Mzungu awe balozi kwa sababu umekataa.Nikamwambia niko tayari kwenda kokote, ndipo akanipeleka Umoja wa Mataifa (UN), New York, Marekani.
Baadaye akaniteua kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, nikiwa pale nilimshauri Mwalimu Nyerere, maana wakati huo kila ulipokwenda kumwona lazima uwe umevaa suti, nikamwambia kulingana na mazingira yetu suti ni shida, nikamweleza jinsi niliivyoona kwa wenzetu, akakubali.

Nikatoka serikalini nikajiunga na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (Unicef) kama Mkurugenzi kwa nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara. Mkataba ulipoisha, nikaenda London, Uingereza kama mshauri wa masuala ya afya kwenye Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola.

Baada ya mkataba huo kwisha, nilirudi Arusha kwenye Ofisi ya Kanda ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, ambako niliamua kustaafu na kurejea wito wangu wa kutibu watu.


Source Mwananchi
 
Mayenga asante kwa makala hiyo ya Dr. Kyaruzi kutoka Mwananchi. Nimeisoma na kugundua kuna maswali mengi muhimu mwandishi ama hakuuliza ama aliuliza lakini hakuandika!.

Alitakiwa pia amuulize
1. Kwa nini alitoka serikalini?.
2. Uhusiano wake na Mwalimu ulikuwaje?.
3. Jee aliridhika na utawala wa Mwalimu?
4. Baada ya kurejea nchini aliendelea
kumtembelea Mwalimu?.
5. Baada ya kukataa ule uteuzi wa kwanza wa Mwalimu na hatimaye akakubali,
jee aliwahi kuteuliwa tena nafasi
nyingine yoyote akakataa?.
6. Baada ya kustaafu rasmi, jee serikali
inamuenzi kwa namna yoyote kama
mpigania uhuru?.
7. Akikumbuka enzi za harakati, jee
anazo any regret kushiriki harakati
hizo?.
8. Nini maoni yake kuhusu utawala wa
Mwalimu, Mwinyi, Mkapa na sasa JK?.
9. Ana maoni gani kuhusu vyama vya
Upinzani?.
10. Anaweza kukumbuka tukio gani zuri
la kisiasa katika maisha yake na lipi ni
lipi ni baya?.
11. Jee ana jambo gani kubwa la kujivunia
alilolifanyia taifa hili angependa
historia imkumbuke hata
atakapokuwa hayupo?.
12. Baada ya kumaliza kuswali Magharibi
na sasa anasubiria Isha, jee ana maoni
ushauri na wito gani kwa Watanzania
atakaotuachia baada ya Isha?.
 
Mayenga asante kwa makala hiyo ya Dr. Kyaruzi kutoka Mwananchi. Nimeisoma na kugundua kuna maswali mengi muhimu mwandishi ama hakuuliza ama aliuliza lakini hakuandika!.

Alitakiwa pia amuulize
1. Kwa nini alitoka serikalini?.
2. Uhusiano wake na Mwalimu ulikuwaje?.
3. Jee aliridhika na utawala wa Mwalimu?
4. Baada ya kurejea nchini aliendelea
kumtembelea Mwalimu?.
5. Baada ya kukataa ule uteuzi wa kwanza wa Mwalimu na hatimaye akakubali,
jee aliwahi kuteuliwa tena nafasi
nyingine yoyote akakataa?.
6. Baada ya kustaafu rasmi, jee serikali
inamuenzi kwa namna yoyote kama
mpigania uhuru?.
7. Akikumbuka enzi za harakati, jee
anazo any regret kushiriki harakati
hizo?.
8. Nini maoni yake kuhusu utawala wa
Mwalimu, Mwinyi, Mkapa na sasa JK?.
9. Ana maoni gani kuhusu vyama vya
Upinzani?.
10. Anaweza kukumbuka tukio gani zuri
la kisiasa katika maisha yake na lipi ni
lipi ni baya?.
11. Jee ana jambo gani kubwa la kujivunia
alilolifanyia taifa hili angependa
historia imkumbuke hata
atakapokuwa hayupo?.
12. Baada ya kumaliza kuswali Magharibi
na sasa anasubiria Isha, jee ana maoni
ushauri na wito gani kwa Watanzania
atakaotuachia baada ya Isha?.

Kaka Pasco,

Baadhi ya maswali yako majibu yake ambayo ni kutoka kwenye kinywa cha marehemu yapo. Wacha kwanza tumalize msiba.....wajua huu msiba unaleta huzuni na simanzi kubwa ambazo zaidi si za ki-msiba!
 
Baada ya kelele nyiiiiiingi leo ndo nimeona Nipashe Kurugenzi wametuma Rambi Rambi.... Jamani Jamani Hii nchi inakwenda wapi? mbona habari ndogo tu ikitoka wanakimbilia kutoa tamko? Je CCM wako wapi? mbona mhasisi wa Chama Chao anazikwa Kibudu? Iko haja ya kurudisha nyuma muda mpaka miaka ya 1948-1960 ambapo mzee Nyerere na Dr Kyaruzi walikuwa anakunywa na kula meza moja huku wakililia ukombozi wa Nchi yetu....Mh Nape UKO WAPI? au ndo unashangilia ushindi wa Mnyika maana mbaya wako ameshindwa?.....CCM wenzangu AMKAAAAA
 
Back
Top Bottom