Ratiba ya Mazishi ya Mpigania Uhuru na Muasisi wa TAA, Dokta Vedasto Kyaruzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ratiba ya Mazishi ya Mpigania Uhuru na Muasisi wa TAA, Dokta Vedasto Kyaruzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ericus Kimasha, May 24, 2012.

 1. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60

  Napenda kuweka sawa Taarifa ya awali juu ya Taarifa ya msiba na ratiba ya mazishi ya Dokta Kyaruzi kama ilivyoletwa hapa Jamvini awali na Ndg. Pasco wa JF

  Mazishi ya Dr. Vedasto Kyaruzi aliyefariki tarehe 20/05/2012 saa 1:20 Jioni katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera, yatafanyika Jumamosi, tarehe 26/05/2012 saa tisa alasiri Missenye-Nyabianga, Kyaka katika shamba lake.

  Mazishi haya yatanguliwa na misa ya kuaga mwili hapo kesho Ijumaa, tarehe 25/05/2012 kuanzia saa saba (7:00) mchana. Misa hii itafanyika nyumbani kwa Marehemu Kashai-Matopeni. Baada ya misa safari ya kuelekea Kyaka kwa maziko itaanza. Mwili wa marehemu utalala shambani kwa marehemu Missenye-Nyabianga

  Umma unakaribishwa kujiunga na familia kwa sala, hali na mali katika kipindi hiki kizito.

  Bwana alitoa, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana na lihimidiwe.


  Kwa Taarifa zaidi wasiliana na:

  Fredy Nshunju
  M/Kiti Kamati ya Habari
  Na. ya Simu: 0767404113

  Evarista Rugeiyamu
  Katibu-Kamati ya Habari
  Na. ya Simu: 0784888091


  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 939
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Upumzike kwa amani Babu yetu mpendwa...
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Inna Li Llahi wa Inna Illahi Rajiun.

  Poleni wote mnaohusika na msiba huu.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwenyezi Mungu amweke mahapa pema peponi...
  Mkuu umesema unataka kuweka sawa taariufa ya awali mbona sioni lolote hasa kuhusiana na Chama cha CCM kushindwa kumuenzi marehemu kwa heshima zote ambazo anastahili. Ama kuna jingine.
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Jipangeni kwa itifaki Kwani MKUU WA NCHI ANAKUJA PIA
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  RIP Kyaruzi . Lakini CCM wapo radhi watoe milioni 10 kwenye msiba wa mtu aliyefia mapenzi kuliko huyu mpigania uhuru
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Ericus Kimasha, asante kwa taarifa hii. Baada ya ile taarifa yangu ya J.3, jana ndio media nazo zimeanza kuutangaza msiba huu muhimu.

  Kumbe ndie aliyekuwa balozi wetu wa kwanza wa Tanganyika huru kwenye Umoja wa Mataifa, UN.

  Naomba utupatie update from time to time ikiwepo ushiriki wa serikali/CCM kwenye msiba huu.

  Asante.

  Pasco.
   
 8. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Kaka Pasco,

  Ulikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutumiwa Taarifa ya msiba huu Juma Pili saa mbili kasoro usiku kupitia FB wall ya Pascal Mayalla! Taarifa ilifuatiwa na Wasifu mfupi wa Marehemu. Nafikiri kule huendi sana!

  Pili, kuhusu Chama na Serikali siwezi kuwatolea Taarifa. Tuwe na subira nao maana hawaleti dawa ya mgonjwa iwe kwamba wasipokuja anakufa! Tuwape muda
   
 9. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Mkuu Mkandara,

  Hilo la kukanusha au kusemea ushiriki wa CCM namwachia Nape Nnauye.

  Jukumu langu lilikuwa kwenye kuweka sawa Taarifa ya Msiba, ulitokea lini, wapi na anazikwa lini, wapi na saa ngapi.

  Nahisi simanzi yangu kuhama kutoka uchungu wa msiba na kwenda kwenye kukosekana kwa malipo ya fadhila kwa watu stahili wa nchi hii.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  P.Pango, naomba tusichanganye CCM na serikali, japo ni serikali ya CCM, lakini serikali ni serikali ya JMT na CCM ni chama cha wanachama, wapenzi na washabiki.

  Fedha TSH, Milioni 10 zilitolewa na serikali na sio na CCM.

  Serikali ilipotoa fedha zile ilikuwa na sababu na justification ikatengenezwa na kuweka precedence kumbe misiba muhimu, basi serikali hupaswa kuchangia angalau TSH. Milioni 10!.

  Fedha hizo zingetolewa na CCM kwa vile hiki ni chama tuu cha siasa, kinaweza kimchangia huyu na kisimchangie yule na hakuna wa kukiuliza kwa sababu vyama ni private entities.

  Lakini serikali ni public entitiy, kama serikali yetu ilitumia milioni 10 kumpatia Kanumba maziko stahiki kutokana na mchango wake kwa taifa hili, sisi kama public tonayo haki ya kujua jee serikali yetu imetoa kiasi gani kumpatia maziko stahiki huyu shujaa wetu wa taifa, mwanzilishi wa Taa na mpigania uhuru?. Tena kwake fedha hizo sio favour bali sasa ni right kwa precedence ya Kanumba!.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Ericus,
  Asante kwa taarifa, ni kweli sikubahatika kuitembelea wall ya Pascal Mayalla na bahati mbaya mimi Pasco wa jf sio member wa fb na kule sitembelei kabisa!.

  Maadam sasa wewe mwenywe upo, keep us updated!.
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  huyu alikuwa mwenyekiti wa TAA?

  mbona sikuwahi kusoma hiii?????????
   
 13. RUGAHIMBILA E R

  RUGAHIMBILA E R Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 90
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Rip mzee wa ukweli na mzalendo halisi. kwa wale tuliomfahamu ni pengo kubwa hasa, hawa ndio watu waliostahili kutunukiwa nishani za utumishi uliotukuka na uaminifu mkubwa.
  tutakukumbuka doctor,
  upumzike kwa amani
  amina
   
 14. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  The Boss,

  Waweza kuwa ni muathirika wa mabadiliko ya mitaala yaliyofanywa na Mungai! Zamani vitabu vya historia ya ukombozi dalasa la pili Dr. Vedasto Kyaruzi alikuwemo. Lakini pia hapa JF mwaka jana kuelekea kilele cha sherehe za Uhuru tumekuwa na simulizi la Waasisi wa Tanganyika. Jaribu kulitafuta!

  Pia waweza kupata dondoo hapa http://www.mwananchi.co.tz/magazines/61-miaka-50-ya-uhuru/16864-dk-kyaruzi-mwanaharakati-muhimu-wa-uhuru-asiyetambuliwa-na-historia.html
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Pasco,

  ..lakini kila wanapofanya jambo lolote lile husema ni serikali ya CCM ndiyo iliyofanya.

  ..mfano, masuala ya ukombozi wa kusini mwa Afrika nimemsikia Mkapa akisema ni CCM ndiyo waliofanya, hasemi wa-Tanzania.

  ..they like to create that confusion and it has been working for them for a while. sasa mambo yamebadilika wananchi wanaaza kuhusisha matatizo yao na CCM na serikali yake.
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  R.I.P Kiongozi wetu,
  hawa hawakuwa mafisadi.
   
 17. raybse

  raybse Senior Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RIP Daktari!!
   
 18. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  RIP babu nadhani nyie ndo mlikua wasomo wa kwanza kabisa kwani ata degree zake inaonesha ni kabla ya uhuru ..Damu ya wazalendo inapotea nadhani magamba yanafurahi kwani poin of reference hazitakuwepo live nani wa kuwakemea hakuna...poleni wafiwa na mungu amlaze mzee wetu kwa utumishi wake wooooooooooooooooooooooooooote...AMEN
   
 19. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  RIP babu nadhani nyie ndo mlikua wasomi wa kwanza kabisa wakati Tanganyika inapata uhuru na sijui madaktari walikua wangapi....magamba wanafurahi kwani wazee wa chama na serikali ndo wanaisha ivyo tutegemee nchi kuuzwa katika kasi mpya,hari mpya na nguvu mpya,,,,,,,,,,
   
 20. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,682
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Well done Pasco!
   
Loading...