Ratiba ya Ligi Kuu Soka England 2020/21: Liverpool yaanza na vigogo. Man City na Man Utd kuanza ligi wiki ya pili

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,283
2,000
Ligi Kuu Soka England itaanza kurindima Septemba 12, 2020 na Bingwa Mtetezi, Liverpool inaanzia nyumbani ikiikaribisha Leeds ambayo ni Bingwa wa Championship

Baada ya kucheza na Leeds, Liverpool itasafiri kwenda Stamford Bridge kuchuana na Chelsea na mchezo wake wa tatu utakuwa dhidi ya Bingwa wa Kombe la FA, Arsenal

Manchester City itaanza itacheza mchezo wake wa kwanza katika wiki ya pili ambapo itachuana na Wolves, kisha itavaana Leicester kabla ya kukutana na Leeds halafu Arsenal

Chelsea itafungua msimu na Brighton Septemba 14, kabla ya kukutana na Liverpool na kisha kukutana na timu iliyopanda daraja ya West Brom

Vijana wa Mikel Arteta wataanza kazi dhidi ya Fulham iliyopanda daraja kupitia 'play-offs'. Baada ya hapo Arsenal itakutana na West Ham kabla ya kukutana na Bingwa Mtetezi, Liverpool

Manchester United pia itacheza mchezo wa kwanza wiki ya pili ya mzunguko kutokana na kufika hatua za mbali kwenye Michuano ya Ulaya kwa msimu huu. Itaanza kampeni dhidi ya Crystal Palace

Fixture-Release-Updated.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom