Ratiba ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 yatolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ratiba ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 yatolewa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Oct 29, 2011.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  ?


  Shirikisho la Soka barani Afrika Caf limetangaza mechi za awali za kuwania kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.
  Baada ya vigogo kadhaa kushindwa kufuzu kucheza fainali za 2012, kuna mechi muhimu mapema katika ratiba hiyo.

  Mabingwa mara saba, Misri watapambana na Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku Cameroon ikipambana na Guinea-Bissau.

  Nigeria itapambana na Rwanda. Timu hizo mbili zinasaka kocha mpya.

  Mechi za 2013 zinatokana na kubadilsiha ratiba ya michuano hiyo kutoka miaka witiri kwenda miaka shufwa na hivyo kufanya kuwepo kwa mwaka mmoja tu wa kufanya maandalizi.

  Hii inamaanisha kutakuwa na muda mfupi kwa nchi zitakazofuzu kucheza fainali za 2012 kujiandaa kwa ajili ya michuano ijayo.

  Ngwe ya mechi za awali itaanza na nchi ambazo zitashindwa kufuzu kucheza michuano ya Gabon na Equatorial Guinea mwezi Januari 2012.

  Nchi kumi na tano ambazo zitafuzu katika ngazi ya awali zitapangwa kucheza dhidi ya timu kumi na tano zitakazocheza michuano ya 2012.

  Afrika Kusini inaingia moja kwa moja kwa kuwa ni nchi itakayoandaa michuano hiyo, baada ya kuchukua nafasi ya Libya, ambayo sasa itaandaa michuano ya 2017.

  Timu zote 16 zitakazopambana nchini Equatorial Guinea na Gabon mwaka 2012 zitaondolewa kwenye raundi ya mwisho ya zitakazofuzu.

  Kwa kuanza Ushelisheli itacheza na Swaziland na Sao Tome kupambana na Lesotho kuwania kuingia katika droo ya awali.

  Halafu kuna michuano 14 ya kuamua nani anasonga mbele kwenda raundi ya mwisho, ambapo timu hizo 16 zilizofuzu kucheza 2012 zitajiunga kuwania kucheza michuano ya 2013.

  Mechi za ufunguzi za michuano ya kufuzu kucheza 2013 zitaanza mapema 2012 na raundi ya mwisho ya kufuzu itachezwa miezi ya Septemba na Oktoba mwakani.

  Raundi ya kwanza ya awali:

  Seychelles v Swaziland

  Sao Tome v Lesotho

  Raundi ya pili ya awali:

  (Timu za Afrika Mashariki zenye maandishi yaliyokoza wino)

  Ethiopia v Benin

  Rwanda v Nigeria

  Congo Brazzaville v Uganda

  Burundi v Zimbabwe

  Algeria v The Gambia

  Kenya v Togo

  Sao Tome/Lesotho v Sierra Leone

  Guinea Bissau v Cameroon

  Chad v Malawi

  Seychelles/Swaziland v DR Congo

  Tanzania v Mozambique

  Central African Republic v Egypt

  Madagascar v Cape Verde

  Liberia v Namibia
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mmmh! Sijui tutaweza kufuzu kwa maandalizi yetu haya!
   
 3. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Labda Watanzania tutaweza fuzu hii.
   
 4. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 810
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 60
  i dont think so! Against mozambik!
   
 5. P

  Piazza jr Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania kwisha habari yetu
   
Loading...