Ratiba ya awali, mazishi ya Mzee Philemon Ndesamburo.

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,388
24,947
Habari wakuu..

Kwa wale ambao wangependa kujua kuhusiana na ratiba ya mazishi ya kumpumzisha mzee wetu Mh Philemon Ndesamburo ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo la Moshi mjini kwa tiketi ya CHADEMA kabla ya kustaafu ni kwamba ipo hivi :


Tarehe 5/06 siku ya Jumatatu katika uwanja wa Mashujaa Moshi ndipo ndugu jamaa na marafiki na wageni watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho.


Tarehe 6/06 siku ya Jumanne ndiyo siku rasmi ya kumpumzisha mzee, ibada ya mazishi inategemewa kufanyika nyumbani kwake kdc-kiboroloni na ndipo atakapozikwa.


Tutaendelea kujuzana kila litakalojiri.

Inna Lillahi Wa Inna Ilayhi Rajiun.

Chanzo : MOSHI-Fm
6cfa5efe29b11781fad38601ca28677d.jpg
 
Aliyekuwa Mbunge wa Moshi mjini kwa Takriban miaka 15, Marehemu Mzee Philemon Ndesamburo Atazikwa siku ya Jumanne Tarehe 06/06/2017.

Mwili wake utaagwa rasmi katika viwanja vya mashujaa Moshi

Habari zaidi tutaendelea Kuhabarishana
 
Back
Top Bottom