RATIBA CAF: Kuiihakikishia Yanga SC kutinga hatua ya makundi Klabu Bingwa

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Ratiba ya michuano ya Klabu Bingwa Barani Africa imekamilika rasmi jioni hii.


"HATUA YA AWALI/ Preliminary round"
Mabingwa watetezi wa LigiKuu Tanzania bara wa wamepangiwa na Mabingwa wa LigiKuu kutoka huko Comoro. Inaitwa 'Ngaya De Mbe'.

Mechi ya kwanza:
Ngaya De Mbe vs Young Africans SC (10,11,12-02-2017).

Young Africans SC vs Ngaya De Mbe
(17,18,19-02-2017).

Tusizungumzie sana kuhusu mtanange huu wa awali. Kwa kuwa ni moja ya kazi nyepesi kabisa ambayo hata Mtibwa Sugar FC.

"16 - BORA".

Baada ya kumalizana na hao vijana wa Comoro, mabingwa wa kihistoria wa LigiKuu Tanzania bara watatakiwa kucheza na mshindi kati ya:-

APR(Rwanda) vs Zanaco (Zambia).
....................................................................................


Kwa tafsiri ya Haraka haraka tunaweza kusema(kutokana nanratiba hii) Dar es Salaam Young Africans SC wameshafanya Booking ya seat katika basi lililoandikwa "Group Stage" kwa kuwa sioni kitu chochote kinachoweza kuwazuia Mabingwa hawa kati ya APR na Zanaco.

Labda unaweza kusema Zanaco ni mfupa mgumu sana. Mara ya mwisho 2006 walitutoa kwenye michuano hii kwa Aggregate ya mabao 3 kwa 2.
Yanga SC 2 - 1 Zanaco
Zanaco 2 - 0 Yanga SC


Katika historia ya Klabu ya Yanga SC imeweza kutana mara mbili tu kwenye michuano hiyo ya Mabingwa barani Africa.

(Ukilinganisha ubora wa kikosi cha Yanga SC 2006 na hiki cha sasa tunaweza kusema kuwa matokea hayo dhidi ya Zanaco si kigezo cha kuwazingatia hao kama ni obstacle ya kuzuia mawimbi ya upepo mkali wa Jangwani)

Ila kwa Ubora wa Klabu ya Young Africans SC ya hivi sasa sioni kama klabu hii(Zanaco) ni kikwazo. Ushindi wa hapa utatuhakikishia kusonga mbele kwenye hatua ya Makundi.

Kwanini kwenda hatua ya makundi ni lengo Mama?
Licha ya kuwa lengo kuu ni kuwa Mabingwa wa bara la Africa.
Lengo letu(Mama) ni kifuta makosa ambayo tumeyafanya msimu uliopita. Hakuna mwana Yanga asiye tayari kuona tukifanikiwa kusahihisha makosa yaliyotughalimu msimu uliopita tulipofika hatua ya Makundi. Hivyo basi ningependa kuwa pongeza wapenzi na Mashabiki wa Yanga SC kwa kuwa msimu huu kwenye michuano ya Klabu Bingwa Barani Africa kwa kuwa wanaenda kushuhudia kilicho bora zaidi ya msimu uliopita..

Nawasilisha....
 
Namba 21: Ikionyesha wapinzani wa Dar es Salaam Young Africans SC. Mechi ya kwanza mzunguko huo wa kwanza Mabingwa wa kihistoria wa LigiKuu Tanzania bara watakuwa ugenini....


Namba 22: mechi ya pili ambapo Dar es Salaam Young Africans SC itakuwa nyumbani.
60bf4e88a130cf21d44a14a183edf5bb.jpg



Namba 19 & 20: Ikionyesha mechi itakayotoa wapinzani wa Dar es Salaam Young Africans SC kwenye hatua ya 16 - Bora
d0298a2054d93e2994bdad7afc472199.jpg
 
1e809a0750b485081f6368af4e8a02e1.jpg

Namba 61 & 62: Ikionyesha kuwa Dar es Salaam Young Africans SC itakutana na mshindi kati ya APR & Zanaco!
 
Mishahara wachezaji wa Yanga washapewa au ?

Usijali Mkuu....


Mabingwa watetezi wa LigiKuu Tanzania bara, Mabingwa wa kihistoria wa LigiKuu Tanzania bara washamalizana na Vijana.

Leo hii Jioni wamepata taarifa hizi za wapinzani wao "Kimataifa" wakiwa mazoezi kujiandaa na mechi ya Ligi.

Jitokeze pale Mazoezi kesho ujishuhidie Vijana wakiwa wanasakata soka kwa morali ya kipekee sana.
 
Kocha George Lwandamina alipokabidhiwa majukumu ya kuipa ubingwa wa Klabu Bingwa Barani Africa klabu ya Dar es Salaam Young Africans SC

a0a3ec3fa597556b252f08c6120aa17b.jpg
 
Wamepangwa na TP Mazembe na Medama wakawa wa mwisho kwenye kundi lao kwa kushinda mechi 1.
 
Yanga wana bahati sana na Comoro. Kila mwaka lazima waanzie huku. Mwisho tutawaita Wangazija
 
Kuingia Taifa mechi za CAF ni lazima uvae jezi ya Yanga... Mauzo ya jezi yatafidia viingilio vya mikia viongozi wa Yanga kamatieni fursa.. Mikia wataangalia kwenye luninga
 
Back
Top Bottom