Rasmi sasa wafuasi wa Hayati Magufuli wamegawanyika makundi mawili

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,115
35,128
Hakuna siri tena kwa sasa, kila kitu kiko wazi kwenye siasa za Tanzania, wafuasi wa Magufuli wamegawanyika kwenye makundi makubwa mawili.

Kwa sasa kuna vita kubwa ya maneno, vijembe, kashfa, fitna, husuda, mivutano na hila za wazi wazi baina ya wafuasi wa Magufuli. Kuanzia mtaani, mitandaoni, bungeni, kwenye vyombo vya habari ni mtifuano tu.

Kuna kundi moja limeamua kuishi kwa uhuru pasipo kujali kivuli cha Magufuli. Kundi hili halioni shida wala woga kusema chochote kumhusu Magufuli hususani kuusema ubaya na udhaifu wa utawala wa Magufuli. Kundi hili kwa sasa linatumia ripoti ya CAG kama uthibitisho wa hoja zao. Hawa wanasema wazi wazi kuwa utawala wa Magufuli ulikuwa ni utawala wenye kasoro kubwa na haupaswi kudumishwa. Kwa sasa kundi hili limepashikwa jina la WANAFIKI.

Kundi la pili ni lile linalopambana usiku na mchana kumtetea na kumsifia Magufuli. Kundi hili halitaki na wala halipendi kusikia chochote kinasemwa vibaya kuhusu Magufuli. Kundi hili linamuona Magufuli kama ndio mwanzilishi na muhitimishaji wa mipango yote ya kisiasa na kimaendeleo hapa Tanzania. Kundi hili linatamani Magufuli aenziwe kwa gharama yoyote. Watu wamelipachika jina kundi hili kama MISUKULE.

#wanafikiCCM
#misukuleCCM
 
Natamani JPM achuje saana Ila najiuliza, Ikiwa atachuja hivo, mitandaoni kutaandikwa nini?

Maana sasa kila anaejua kuandika slabi na kuzipangilia, basi anatupia tu chochote hata kama ni ujinga!!
 
CCM WAMEAMUA KUGAWANA FITO!!!
Ndiyo mnavyojidanganya huko ufipa duuu.Subiri mkutano mkuu 30/4/2021 ushuhudie ile ng'ara ccm ng'araaaaaa.Tunaimani na Samia wengine wa piga debe tuuuu. Ccm ni ile ile jana leo na kesho
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nchi ilipitia pagumu sana...
images (2).jpeg
 
Kichwa cha habari hakiakisi vizuri yaliyomo ndani yake. Ni wafuasi wa Magufuli au wa CCM waliogawanyika makundi mawili?
 
Back
Top Bottom