Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Chris wood

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
1,667
5,008
Kwanza niseme tu mimi ni kati ya watu, waliokuwa wakiamini betting kwa asilimia 100, nilikuwa na imani betting ndio kitu itanitoa kimaisha, kuhusu betting ulikuwa huniambii kitu, kuna ile kauli watu huwa wanasema beti kama starehe, Lakini mimi nimekuwa nikiifanya kama kazi ya kujiingizia kipato.

Nilikuwa mstari wa mbele kutoa Matusi, kejeli husda na masimango kwa wale wote, waliokuwa wakionesha kupinga ama kuleta hoja kinzani kuhusiana na gambling/betting.

Katika kipindi kifupi takribani mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo ndio nilianza kuifanya betting kama kazi.

Lakini kwa huo muda mfupi, imeniletea hasara kubwa kubwa kubwa ambayo sitokuja kuisahau, yaani zile pesa ambazo nimepoteza ningesema badala ya kutuma kwenye betting company, niziweke kwenye kibubu now ningeweza kufungua biashara kubwa sana.

Baada ya vipigo kuzidi, huwa kuna msemo wanasema sikiliza wataalamu inaonekana strategies unazotumia sio salama, Hao wanaojiita watalamu watakwambia usiweke timu nyingi weka timu chache ,"tafuta odds mbili halafu tia laki," Aloo huo msemo ndio umenifukia kabisa hadi sasa naandika hapa sina hata mia mbovu.

Jana kuna mkeka niliucopy kutoka kwa jamaa mtata sana humu Jamiiforums nikaweka pesa ya nauli ambayo leo nilikuwa naelekea Dar es Salaam, kwa mazingira ya kutatanisha sana pesa yote nimeliwa, mpaka muda huu nimejilaza hapa nasingizia naumwa.

Kwenye betting sio kwamba watu hawashindi wanashinda ila kunautofauti mkubwa sana kati kuliwa na kushinda so ukiifanya kwa muda mrefu ukaja piga mahesabu baada ya mwaka utajikuta na hasara kubwa Hadi utaogopa kama sio kulia.

Betting imefanya nashindwa hata kununua nguo mpya hadi zile nilizomaliza nazo masomo zimeanza kupauka sio kwamba hela sipati hapana zote zinaishia kwenye mikeka, yaani getto unaweza kuta nimenunua sukari robo, mchele kilo mbili halafu kwenye simu nimebet 50000 na yote inaliwa.

Mwaka jana nilikuwa nasimamia mashamba ya jamaa fulani sasa nilikuwa nikipokea hata pesa za kupalilia, na mimi boss wa vibarua najitengea ekari yangu moja ya palizi maana nimepita JKT halafu 60000 naweka mfukoni kisha wale vibarua badala ya kuwalipa 60000 nawalipa 40000 kwa ekari, tutalima weee nikimaliza pesa yote naenda kuliwa kwenye betting.

Usiku wa leo nimekaa nikafanya projection nikiendelea hivi baada ya miaka 5 ijayo nitakuwa mmoja kati ya watu masikini zaidi Tanzania, At 20s vijana wengi hutumia kujenga future zao mimi natumia kubomoa, Betting imeniletea uvivu, muda wote sina furaha, nilikuwa napenda kusoma, kuongeza ujuzi, kutafuta kazi, kuwekeza, kuchangamana na watu, kufanya kazi, mdau wa michezo, mapenzi but now nimekuwa kama mtu aliepigwa bomu.

Bado sijachelewa, nina muda wa kutosha kusahihisha makosa niliyoyafanya, sihitaji tena kuwa mtumwa, nimekubali kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya, sioni kama ni tatizo kuanza moja, ninaamini tatizo ni kuendelea kukumbatia adui na adui wangu anaehujumu uchumi wangu ni betting.
 
Safi sana safi sana

Tunabeti ila basi tu huo ndo ukweli hamna faida yoyote hakuna cha strategy wala njia gani hii ni kamali na inaleta umaskini na uvivu kwa vijana wengi wa kitanzania bora umeamua kujinasua kwenye mtego wa shetani ila kama ni hasira badae utarudi tu utaanza kuweka mikeka upya utakuwa mkamaria tena mtata wanasema"THE FIGHT AGAINST ADDICTION HAS NEVER BEEN EASY"

Betting & Forex na kamari nyngne hakuna pesa huo ndo ukweli tufanye kazi vijana hakuna pesa rahisi.

IMG_20210501_033846.jpg
 
Safi sana safi sana
Tunabeti ila basi tu huo ndo ukweli amna faida yoyote hakuna cha strategy wala njia gani hii ni kamali na inaleta umaskini na uvivu kwa vijana wengi wa kitanzania bora umeamua kujinasua kwenye mtego wa shetani ila kama ni hasira badae utarudi tu utaanza kuweka mikeka upya utakuwa mkamaria tena mtata
wanasema"THE FIGHT AGAINST ADDICTION HAS NEVER BEEN EASY"
Betting & Forex na kamari nyngne hakuna pesa huo ndo ukweli tufanye kazi vijana hakuna pesa rahisi View attachment 1771824
Kweli mkuu betting hapana, ninaroho ngumu lakini nimesarenda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom