Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Hongera uamuzi mzuri sana.
Huo uamuzi wa hasira tu! Kapumzika tu huyo! Akirudi akala mikeka miwili atarudi rasmi!

Tatizo wasichokijua watu betting ina upepo! Ukiona siku umebeti mara 3 mfululizo unamla bookmarker tu jua siku hio una upepo! Jiwashe mpaka ambapo utaona game zinaanza kukukataa.Zikichana 2 mfululizo tulia jua upepo umebadilika!

Sasa utakuta pale mtu ndio anaingia mawenge anataka arudishe hasara matokeo yake anafumuliwa marinda! Mi nishaliwa na game moja hela yote nilikuwa nazuia corner kila nikizuia inachana kwa kuongezeka corner moja mara ya tatu mchezo uko mwishoni nikasema narudisha hasara weee 😂😂😂😂😂😂 account ilifuka moshi!
 
Mkuu tatizo unabet kimaskini unaweka 500 ili ushinde million unaona inawezkana? Hio ni bht sana asee. Mimi niliweka 500k nikala 6m na usheee lakin ningeweka 500 hapo ningeshinda 6000 unaona utofauti hapo nmepata faida ya 5.5m. Ukibet ukaweke pesa ndogo lazma uweke tim nyingi ili dau liwe kubwa lakin ukiweka timu chache dau kubwa unakua na probability kubwa ya kushinda.
Bora hata ningekuwa na bet hiyo 500 angalau ninge survive kilicho nifirisi ni hizo hizo 2 odds halafu unaweka laki
 
Kwanza niseme tu mimi nikati ya watu, waliokuwa wakiamini betting kwa asilimia 100, nilikuwa na imani betting ndio kitu itanitoa kimaisha, kuhusu betting ulikuwa huniambii kitu, kuna ile kauli watu huwa wanasema beti kama starehe, Lakini mimi nimekuwa nikiifanya kama kazi ya kujiingizia kipato.

Nilikuwa mstari wa mbele kutoa Matusi, kejeli husda na masimango kwa wale wote, waliokuwa wakionesha kupinga amakuleta hoja kinzani kuhusiana na gambling/betting
Katika kipindi kifupi takriban mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo ndio nilianza kuifanya betting kama kazi.

Lakini kwa huo muda mfupi, imeniletea hasara kubwa kubwa kubwa ambayo sitokuja kuisahau ,yaani zile pesa ambazo nimepoteza ningesema badala ya kutuma kwenye betting company, niziweke kwenye kibubu now ningeweza kufungua biashara kubwa sana.

Baada ya vipigo kuzidi, huwa kuna msemo wanasema sikiliza wataalamu inaonekana strategies unazotumia sio salama,, Hao wanaojiita watalamu watakwambia usiweke timu nyingi weka timu chache ,"tafuta odds mbili halafu tia laki," Aloo huo msemo ndio umenifukia kabisa hadi sasa naandika hapa sina hata mia mbovu,
Jana kuna mkeka niliucopy kutoka kwa jamaa mtata sana humu jamii forum nikaweka pesa ya nauli ambayo leo nilikuwa naelekea dar es salaam, kwa mazingira ya kutatanisha sana pesa yote nimeliwa, mpaka muda huu nimejilaza hapa nasingizia naumwa.

Kwenye betting sio kwamba watu hawashindi wanashinda ila kunautofauti mkubwa sana kati kuliwa na kushinda so ukiifanya kwa muda mrefu ukaja piga mahesabu baada ya mwaka utajikuta na hasara kubwa Hadi utaogopa kama sio kulia.
Betting imefanya nashindwa hata kununua nguo mpya hadi zile nilizomaliza nazo masomo zimeanza kupauka sio kwamba hela sipati hapana zote zinaishia kwenye mikeka, yaani getto unaweza kuta nimenunua sukari robo, mchele kilo mbili halafu kwenye simu nimebet 50000 na yote inaliwa.

Mwaka jana nilikuwa nasimamia mashamba ya jamaa fulani sasa nilikuwa nikipokea hata pesa za kupalilia ,na mimi boss wa vibarua najitengea ekari yangu moja ya palizi maana nimepita jkt halafu 60000 naweka mfukoni,.kisha wale vibarua badala ya kuwa lipa 60000 nawalipa 40000 kwa ekari ,tutalima weee nikimaliza pesa yote naenda kuliwa kwenye betting.

Usiku wa leo nimekaa nikafanya projection nikiendelea hivi baada ya miaka 5 ijayo nitakuwa mmoja kati ya watu masikini zaidi Tanzania, At 20s vijana wengi hutumia kujenga future zao mimi natumia kubomoa, Betting imeniletea uvivu ,muda wote sina furaha ,nilikuwa napenda kusoma,kuongeza ujuzi,kutafuta kazi,kuwekeza,kuchangamana na watu, kufanya kazi, mdau wa michezo, mapenzi but now nimekuwa kama mtu aliepigwa bomu.

Bado sijachelewa, ninamuda wa kutosha kusahihisha makosa niliyoyafanya, sihitaji tena kuwa mtumwa, nimekubali kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya, sioni kama nitatizo kuanza moja, ninaamini tatizo ni kuendelea kukumbatia adui,na adui wangu ane hujumu uchumi wangu ni betting.
Kamari haijawahi kuwa nzuri.
 
Tatizo wengi huwa wanatangaza kuacha lakini hurejea kimya kimya.

Ukiendekeza betting hata nguvu za kiume zitapungua.
Ulipo hapo hata demu utakuwa huna, kama unaye basi migogoro haiwaishi.
Kuliko kumpa shem matumizi unaona bora umpe mhindi akutunzie hela.
 
Siwezi tembeza mihogo ndugu. Ila pesa yangu kuliko kuipeleka kwa muhindi ni bora nifanyie vitu vya maana.

Kuhusu hiyo 70% unajidanganya labda uwe newbie kwenye gemu. Kwa kiswahili hiyo ni bahati nasibu

Kumbe Bado Unaendeshwa Na Maono Ya Bahati Basi Cheza Biko.

Bahat Ni Kitu Cha Ziada Tu Kene Maisha, Betting Ni Kazi Ndo Maana Tunawekeza Muda Na Pesa. Kubali Tu Mzee Hujui Kubet Ulikuwa Unatuchangia Wengine
 
Sure odds halafu umeweka 3-Way ati man ashinde au liver ashinde! Kinachotokea wanatoa draw af inabaki story
Betting ina disappoint sidhani kama kunakitu kitakuja nidisappoint kama ilivyofanya betting,.unaona kabisa hizi odds 2 au 3 muhindi achomoki nikiweka 50k faida 50k alooo ngoja waanze kucheza utafurahi na roho yako
 
Mie kwa kuogopa hizo dissapointments nimeamua kuhamia kwenye mchezo tofauti! Thats the only way ila mpira unakera kuliwa ni compulsory timu haziko stable yani!
 
Kumbe Bado Unaendeshwa Na Maono Ya Bahat Basi Cheza Biko.

Bahat Ni Kitu Cha Ziada Tu Kene Maisha, Betting Ni Kazi Ndo Maana Tunawekeza Muda Na Pesa. Kubali Tu Mzee Hujui Kubet Ulikuwa Unatuchangia Wengine
Sio kweli mkuu inaonekana wewe ndio bado hujafunguka .
Betting ni game of chance kama ulikuwa hujui.
Pesa ambayo nimewahi kula in a single day ni nyingi mno sidhani kama utokuja kuishinda, hata stake ninazoweka ni kubwa mno. Lakini zote hizo muhindi kazirudisha na kunifirisi hadi nilizokuwa nazo.
Take time uchunguze betting history yako utapata majibu, whether kuna faida au hasara
 
Ila mwindi anajua kuyumba aisee. Yaani hata ukiweka ashinde yoyote ngoma inaisha sare.

Ukiweka coner zifike 8, zinaishia 7. Ukiweka magoli yafike 2 hawafungani.
Ila mimi pamoja na vipigo navyopata simwachi, mpaka natembea na fimbo.😁😁😁😁
 
Tatizo wengi huwa wanatangaza kuacha lakini hurejea kimya kimya.

Ukiendekeza betting hata nguvu za kiume zitapungua.
Ulipo hapo hata demu utakuwa huna, kama unaye basi migogoro haiwaishi.
Kuliko kumpa shem matumizi unaona bora umpe mhindi akutunzie hela.
Kweli kabisa ndugu hadi hapa sina serious relationship, siku nimepiga hela ya maana ndio naanza pekua phonebook nione nitaenda mbandua nani.Au siku kama nimepigwa kipigo cha mbwa koko naweza tena toa balance niliyobaki nayo kwenda kujipooza nayoyote atakae jishobokesha mbele yangu,
 
Ila mwindi anajua kuyumba aisee. Taani hatabukiweka ashinde yoyote ngoma inaisha sare.

Ukiweka coner zifike 8, zinaishia 7. Ukiweka magoli yafike 2 hawafungani.
Ila mimi pamoja na vipigo navyopata aimwachi, mpaka natembea na fimbo.
Mimi juzi nikaweka, goli la kwanza, halitokuwa la kujifunga. Ila nimezubaa nafatila live score sinikaona Own goal ikabidi nitupe simu
 
Kweli kabisa ndugu hadi hapa sina serious relationship, siku nimepiga hela ya maana ndio naanza pekua phonebook nione nitaenda mbandua nani.Au siku kama nimepigwa kipigo cha mbwa koko naweza tena toa balance niliyobaki nayo kwenda kujipooza nayoyote atakae jishobokesha mbele yangu,
 
Sio kweli mkuu inaonekana wewe ndio bado hujafunguka .
Betting ni game of chance kama ulikuwa hujui.
Pesa ambayo nimewahi kula in a single day ni nyingi mno sidhani kama utokuja kuishinda, hata stake ninazoweka ni kubwa mno. Lakini zote hizo muhindi kazirudisha na kunifirisi hadi nilizokuwa nazo.
Take time uchunguze betting history yako utapata majibu, whether kuna faida au hasara

Sijui Umeanza Kubet Lini. Mimi Nina Uzoefu Wa Miaka 9 Kene Football Betting, Sidhani Kama Tunashindana Ila Huwezi Kunishawishi. Kuhusu Stake Ni Siri Na Uwezo Wa Mtu, Stake Inaweza Kuwa Ndogo Na Ikawa Tiki Every Single Day.

Ww Unaamini Sana Kene Bahati, Ila Ukweli Ni Kwamba Kazi Ikiwa Ngumu Huna Budi Kuacha, Mzee Betting Ni Maji Ya Shingo Kwako Huiwezi
 
Mie kwa kuogopa hizo dissapointments nimeamua kuhamia kwenye mchezo tofauti! Thats the only way ila mpira unakera kuliwa ni compulsory timu haziko stable yani!
Mimi basketball na football ndio nimewekeza muda mwingi, hizo cricket, kukimbiza farasi huwa sizifatilii.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom