Rasmi Manji arudi yanga ataanza kazi january,simba kazi mnayo

craq

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
859
1,864
-Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuph Manji ametangaza kurejea kazini na bado yeye ni Mwenyekiti wa klabu ya Yanga. Kupitia barua yake iliyosomwa mbele ya wanachama katika makao makuu ya klabu hiyo leo inasema Manji amekubali kurejea Yanga na ataanza kazi January 2019.

Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la klabu Yanga Kapteni George Mkuchika amesema Yussuf Manji amerejea katika nafasi yake baada ya kumuandikia burua ya kukubali ombi la Wanachama wa klabu hiyo kumtaka atengue uamuzi wake wa kujiuzulu

Akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kikao kilichoitishwa na Baraza hilo, Kapteni Mkuchika ameonyesha barua iliyoandikwa na Manji kuridhia kurejea katika nafasi ya Uwenyekiti wa Yanga.

Kapteni Mkuchika amesema Manji aliandika barua ya kujiuzulu lakini wanachama walilikataa ombi lake kupitia Mkutano halali wa klabu hiyo na kumuomba arejee katika nafasi yake.

Barua hiyo aliyoandika ni uthibitisho kuwa ameridhia maombi ya wanachama wa Yanga na sasa ni rasmi amerejea katika nafasi yake.

Kapteni Mkuchika amesema Manji ndio Mwenyekiti wa Yanga huku Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Thobas Langalanga aliyekuwa ameteuliwa kukaimu wadhifa huo hatambuliki
FB_IMG_1541964916402.jpg
FB_IMG_1541964848302.jpg
FB_IMG_15419656485643117.jpg
 
Ni sawa tu.
Ila inampasa kufuata taratibu za uongozi kama katiba inavyoelekeza.
Achukue fomu, agombe nafasi ya Uenyekiti wa Yanga.
Wanachama wamchague.
Kipindi chake cha uingozi kikipita, agombee tena ili achaguliwe tena.
Ndivyo anavyotakiwa kufanya na sio kuwa mwenyekiti miaka yote bila kuanyika uchaguzi.
 
Uchaguzi January 13 yeye atarejea January 15 kuanza kazi tumia akili zako kuwajua kinachoendelea katika club cha Yanga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom