Rasmi: Kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rasmi: Kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma 2011

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ESAM, Jul 29, 2011.

 1. E

  ESAM JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hii sasa ni rasmi kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma Tanzania kwa mwaka 2011, kimepanda kutoka shilingi za Kitanzania 135,000/= mpaka 150,000/=. Hii ni kwa mujibu mishahara iliyolipwa Julai 2011.

  Nawasilisha.
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante kwa taarifa. Zile 260,000 zilizoahidiwa wakati wa kampeni ziliishia wapi?

  Watumishi wasipoamka iko siku wataongezewa buku buku na ndiyo itakuwa faida ya kuchagua waendesha mambo kimjini mjini!
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nilidhani ingekuwa 40%
   
 4. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kwa gharama za vitu zilivyopanda bado haitoshi kitu hiyo ni sawa na $100 kwa rate iliyopo sasa 100x1565=156500/= mfanyakazi wa serikali kima cha chini analipwa chini ya dolla 100$ kwenye nchi yenye kila utajiri wa hali ya juu sana ni wehu....yaani ni $%$!*@nge tu :(
   
 5. Jimbi

  Jimbi JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2011
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  hadi siku mtakapo pata akili, ya kuacha kuchagua hawa wababaishaji ndipo mabadiliko mtakapoyaona
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  duh! yaani tsh 5,000/- hazimtoshi mwanafunzi kwa siku ila zinamtosha baba/mama yake kwa siku hiyohiyo moja!

  hii serikali yetu kiboko kwa kweli!
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hawa wafanyakazi ni miongoni mwa kundi tiifu sana kwa serikali ya ccm.

  Tulikuwa na uchaguzi mkuu mwaka jana na wakaamua kuichagua ccm huku wakijua kwamba itawatelekeza lakini wakaichagua tu.

  Wakiambiwa waandamane ama wagome ili serikali iwalipe kiwango kinachokidhi mahitaji wanagwaya, ngoja waendelee kupigika wala siwahurumii katika hili.

  Wanafunzi wa vyuo vikuu wameongezewa kiwango cha posho kwa kuwa walishaanza kuishikisha adabub serikali na kama isingeongeza posho moto ungewawakia.
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,156
  Trophy Points: 280
  Utajiri hauji bila ya kuufanyia kazi, wajitahidi kusoma waondoke kwenye kima chini au waingie kwenye ujasiriamali.
   
 9. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Dada acha roho mbaya bwana, inamaana wasiosoma hawana haki? Wangesoma wote kwa kiwango cha juu nani angekubali kuwa messanger? nani angekuwa mhudumu? unapoongea vitu uwe unafikiria nafananisha maneno yako sawa na mtakula nyasi lkn ndege ya rahisi lazima tununue. Acha ubinafsi wewe nyie ndo mnakuwa mayes bosi na usomi wako.
   
 10. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndo wale waliochukua akili za mbayuwayu wakachanganya na za kwao nini? hapo kinachofuata no utendaji ni majungu tu ofisini, wizi na unzinzi wa kutembea na mabosi/wenye vipato vikubwa hasa kwa hao dada zetu wenyekutaka makuu na wanaume wataolewa na wanawake wenye vipato vya juu.
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ninavyojua mimi, mishahara ya serikali ni mfumo ambao ukiongeza KCC vima vyote huongezeka automatically. na pressure za kuongeza KCC huwa ni technique tu ila kimsingi ni presure ya kuongeza vima vyote serikalini. KCC ni indicator tu ya welfare ya wafanyakazi serikalini na hata kama wafanyajazi wote watasoma na kupata promotion (which is practically impossible) bado KCC kama welfare indicator (or benchmark) itaendelea kuwepo!
   
 12. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  We kweli bumunda!, kwa kianzio hicho utafanya ujasiriamali gani?, utalipa ada ya shule?, nakuambia hata 30000 za fomu TCU huziwezi! Tutake radhi
   
 13. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Tuhurumie tuu aisee!, hatukuwachagua waliiba kura!, tumebanwa ile mbaya, hatuna jeuri ya kuishi kwa amani mwezi mzima bila mshahara, sasa tukiandamana wanatusimamisha kazi kwa kosa la kuleta siasa katika kituo cha kazi (si unajua kituo wanataja sehemu?, mf dar, morogoro manispaa etc) hali ni mbaya sana!
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  ok nimekubaliana na wewe kwamba hamkuwachagua, sasa mbona mmeshindwa kusimamia maslahi yenu wenyewe? Ni vizuri mfahamu na kuzingatia kwamba hatma yenu iko mikononi mwenu wenyewe.

  Mkigoma wafanyakazi wote, hususan hao wa kima cha chini kuanzia wizara, mashirika ya umma na idara za serikali watawafukuza wote?

  Kama bado hamfahamu kwamba kuna sheria za kuwalinda mnapotaka kufanya mgomo basi mtaendelea kukandamizwa maisha yenu yote ya utumishi wa umma. Muhimu ni kufuata utaratibu wa kisheria kabla ya kuitisha mgomo.
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Issue hapa ni kulipa KCC ambayo inakidhi mahitaji.

  Tafiti zilizofanywa na TUCTA miaka mitatu iliyopita zilibainisha "living wage" ilitakiwa kuwa Tsh.315,000.00

  Kwahiyo hapa tunazungumzia KCC inayoweza kumtosheleza mfanyakazi. Na mfumo huo huo unaweza kutengenezwa in such a way kwamba serikali itakuwa na uwezo wa kuhimili mahitaji ya wafanyakazi wake. Sasa hivi kuna wachache wanakula mishahara minono sana, tena hao hawalipi hata kodi na kuna kundi kubwa sana wanalipwa mishahara midogo huku wakikatwa na kodi.
   
 16. Jimbi

  Jimbi JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2011
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  wewe ni kada wa magamba, ama kijana wa nape kazini?
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wafanyakazi hawatafuti utajiri, hapa wanatafuta KCC inayokidhi "living wage" na kwakuwa magamba wengi wanawaza utajiri pasipokufanya kazi, si ajabu serikali yake kuwajaza mapesa watumishi wa kada za juu tena hawalipi kodi wakati watumishi wengi wa kundi la KCC wakisahaulika.

  Mnafanya ufisadi na kuiba sana ili mtajirike badala ya kuwatumikia watanzania.
   
 18. g

  graceirene Member

  #18
  Jul 31, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wabunge wetu na baraza la mawaziri mna sura za mbuzi mee , sitting allowance yenu kwa siku moja mnageuza kuwa mshahara wa mwezi kwa wananchi ambao kura zao ndiyo cv ya nyie kulipwa mamilioni ya fedha .
  Kweli watanzania waanze kufuatilia usalama wa kura kabla hajaipiga aangalie
  Ni yupi anampa haiwezekani wabunge wanalalamika malipo ya kukalia kiti kwa siku ni madogo yaongezwe bila haya wanataka yafike laki 5 huku wakipitisha kwa kishindo mshahara wa laki na nusu kwa mpiga kura wake ambaye kimsingi ndiye bosi wake . Tanzania bora wakoloni weupe kuliko hawa ngozi nyeusi
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,156
  Trophy Points: 280
  Haki wanayo, hilo halina ubishi, ili nchi iweze kulipa kila mtu vizuri, inabidi kila mtu afanye kazi kwa bidii, ama ya kuajiriwa ama ya kujiajiri na kodi zilipwe na kiwango kikubwa cha wananchi, leo Tanzania walipa kodi ni kidogo sana ukilinganisha na mataifa yanayolipa vizuri. Hivi mnategemea hiyo mishahara ya Serikalini itoke wapi? wakati tunajua kabisa kuwa kipato cha Serikali ni kodi.
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,156
  Trophy Points: 280
  Waache kazi, waende wakalime, ardhi safi tunayo.

  Ukiona mtu kang'ang'ania kazi na kipato cha hapo hakimtoshi ujue ana kipato kingine cha ziada. Sioni sababu ya mtu kung'ang'ania kufanya kazi sehemu ambayo akilipwa mshahara wake haumtoshi hata kula wiki moja!

  Tuwe realistic na tusiwe na majungu bila kuutazama ukweli ulivyo, hivi nauliza, kama mtu anapokea 135,000/= kwa mwezi, ambazo ni ukweli usiofichika hazimtoshi hata kula wiki moja, hizo wiki tatu hukaa na njaa?

  Mimi namjuwa dereva wa serikali, kwa miaka 8 tu, na hasafiri nje ya Dar. yupo hapa hapa mjini, ana nyumba tatu kajenga baada ya kuanza kazi hiyo ya udereva, hana shamba hana biashara nyingine. Jiulize, anatowa wapi hiyo fedha nyingine ya ziada ya kuweza kujengea nyumba tatu Dar? tena sehemu nzuri tu, Nyumba si vibanda.
   
Loading...