profftobe
JF-Expert Member
- Sep 12, 2017
- 906
- 929
Umesema vema na siyo mapadri tu dhambi ya uzinzi inatafuna wengi. Kwa maana nyingine ni kuwa kutozini ni amri ya Mungu. Hivyo tusiwanyoshee mapadri vidole tukasahu madhambi yetu wenyewe. Kila mkristo amezuiwa kushiriki ngono. Kila anayeshiriki anafanya dhambi na kama ulivyosema askofu Yuda na yeye anajua vema kuwa mapadri wengi wanazini mbona hawafungii na siyo kwamba nahukumu lakini uenda hata yeye alishawahi kupiga hata mara chache maishani mwake. Hivyo hukumu aliyotoa kwa huyo matonya ni ya kibabe na ya kibaguzi haikubaliki hata kidogo.1.Moja ni uzushi kusema alifia kwa mwanamke japo simkingii kifua baba na mlezi wangu huyu aliyetangulia mbele ya haki kuwa alikuwa anapenda sana alikotoka. Ukweli ni kwamba alikunywa sumu na kama ungekuwa umepata nafai ya kuishi naye na kumsikiliza jinsi alivyokuwa mfuasi kamili wa falsafa za Socrates ungefahamu kuwa kwake kujiua ni aina ya kifo alichokwisha kukichagua.
2.Labda uwe hujawahi kuishi na mapadri,, lakini kama umewahi kuishi nao utakubaliana na mimi kuwa ni wachache sana hawana doa la dhambin ya uzinzi japo siungi mkono pia,, hoja yan kumuacha azikwe na katekista haina mjadala maana ndo utaratibu wa kanisa lakini alipaswa kufahamu kuwa yule ni binadamu na yeye hakupaswa kumhukumu kwani wapo mapadri wengi tu vituko ila Mungu anawatumia bado na ni lazima tuwaheshimu maana Mungu ana makusudi nao. Kama alivyo fanya Mfalme Daud kwa kutothubutu kumuua Sauli ila Askof Rwaichi alilihandle hili suala like a mere person na ndio maana mapadri wenzake walishindwa kujuzuia walienda msibani japo walisimama umbali wa mita kadhaa kutoka mahala alipokuwa anazikwa Fr. Matonya.