John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Ethiopia, leo Jumapili inatarajiwa kufua umeme kutoka kwenye Bwawa la The Grand Ethiopian Renaissance linalokabiliwa na utata lililoko katika Mto Nile.
Bwawa hilo limekuwa chanzo kikuu cha mzozo wa kikanda tangu kuanza kwa ujenzi wake muongo mmoja uliopita. Mataifa jirani ya Ethiopia, Misri na Sudan, yanasema bwawa hilo ni kitisho kwao kutokana na utegemezi wao wa Mto Nile huku Ethiopia ikisema mradi huo ni muhimu kwa ajili ya usambazaji wa umeme na maendeleo.
Bwawa hilo lililogharimu dola bilioni 4.2 linalotarajiwa kuwa mradi mkubwa zaidi wa umeme unalozalishwa kwa nguvu za maji barani Afrika, hatimaye litazalisha zaidi ya megawati elfu 5 za umeme.
Mradi huo utaongeza maradufu uzalishaji wa sasa wa umeme nchini Ethiopia. Mataifa hayo matatu jirani yamefanya duru kadhaa za mazungumzo kuhusu jinsi bwawa hilo linavyopaswa kufanya kazi lakini kufikia sasa, hakujakuwa na dalili ya muafaka.