RASMI: Baada ya Lyon kuiondoa Manchester City. Nusu fainali ya Bayern Vs Lyon

waterproof

JF-Expert Member
Aug 14, 2020
387
348
Wakulungwa tumeshuhudia leo Manchester city akifungashiwa virago na watoto wa ufaransa Olympic Lyon na hivyo kufanya nusu fainali kuzidi kunoga maana wengi tulitegemea Man City leo hii atatinga hatua ya nusu fainali lakini haikua bahati.

Jana tumeshuhudia upana na umahiri wa kikosi cha Munich kikimuangamiza Barca bao 8 kwa 2 na kutinga hata ya nusu fainali.

Ngoma inakua nagwa kwa Lyon kwamba wataweza kuwazuia watoto wa Bavarian? Jibu Mimi sina hapo.

Au ndio tusubiri kuna MTU anapgwa dazani maana tunaweza sema itakua rahisi kwa Munich kutoboa kwenda final alafu mambo yakageuka maana mpira haunaga adabu.
 
Lolote linawezekana

team yangu ya Barcelona ni mbovu

imebaki jina tu ndo mana hawajachukua kombe hata 1 msimu huu

lyon kwa sasa wako ktk ubora kuliko barca

kuwatoa Juventus na Manchester city inathibitisha ubora wao kwa sasa
 
Back
Top Bottom