Rasmi Apple yainunua App ya Shazam kwa bilioni 897.58

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,497
apple-shazam.jpg
Baada ya tetesi za muda kampuni ya Apple imetangaza rasmi kuinunua App maarufu ya kutambua muziki ya Shazam.

Katika taarifa iliyotolewa na pande zote mbili kulionesha mafanikio yaliyofikiwa kwa makubaliano yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 400 sawa na pesa ya Tanzania yenye thamani ya 897,580,000,000.

Apple wamesema wanafuraha kwa shazam kujiunga nao na wana mipango mizuri juu ya uboreshaji wa App ya Shazam. Kwa upande wa Shazam wamesema wamefanya makubaliano kuwa sehemu ya timu ya Apple.

Shazam ni moja ya programu zinazopendwa na kupakuliwa sana na mamilioni ya wengi duniani ambapo kazi yake kubwa ni kutambua muziki wowote ambao unautafuta.

Mfano kuna muziki unausikia na ungependa kujua umeimbwa na nani unachofanya ni kufungua App ya Shazam na kusikilizisha muziki huo na punde itautambua muziki huo kwa jina lake na ni nani aliyeuimba.

Kununuliwa kwa Shazam kunaweza kuwa pigo kwa watumiaji wa simu za mfumo wa Android kwani kuna uwezekano mkubwa App hiyo kuondolewa katika Play store na kubaki kwenye duka la AppStore pekee.

Muungwana
 
Ivi IT wa bongo wanashindwa nini kutengeneza kitu wakapata mapesa kama wale jamaa wa whatsapp na hawa wa shazam??
wanaweza ila njia wanazotumia kufanya app zao ziwe maarufu ndipo shida inapo anzia hii inachagizwa pia na watanzania walio wengi kutokupenda kusapoti kazi za nyumbani.

nitakupa mfano mwaka juzi kama sijakosea palitokea kijana wa UDOM alitengeneza kitu kama facebook na watu wakaonekana kuikubali ila mpaka sasa sijui aliishia wapi na siamini kama kuna mtanzania anaetembelea hiyo project ya jamaa.
 
Mkuu ukiangalia hayo mapesa ni mengi sana yaani mtu unakaa ndani na ku code alafu baada ya muda apple wanakufwata daaah!! Nakumbuka hata fb wakati wanaanza yahoo waliwafwata ili wanunue fb na walimwaga mapesa mengi ila mark zuck akakataa na leo ndio unaiona fb ilivyo..

Ni kweli, ila pia kama unajua kuna fb na insta why usijaribu kutengeneza kitu kingine??
 
kila kitu ni ushindani sio kwasbb kuna insta au Facebook basi watu waache kutengeneza vitu kama hivyo
watu watengeneze ila wawe wabunifu zaidi kumbuka Facebook aliiona WhatsApp kama threat kwake na akaamua kuwafanya partners

kulikua na Skype
akaja imo n.k
wote wanatoa vitu vyenye kuendana

vipi BBM? wangemwacha pekeyake leo tungekuwa na WhatsApp?

cha msingi ni kutumia udhaifu wa aliyekutangulia kwa kuboresh zaidi hata kama umekopi na kupest kutoka kwake

vivyo hivyo utaona ligi ipo kwenye maswala ya antivirus
 
Teknolojia inalipa na itaendelea kulipa kwasababu kila aina ya biashara na huduma itafanywa kwa mfumo wa kompyuta.

Itafikia wakati ukitaka nyumba ya kupanga/kiwanja unaingia kwenye app fulani ili kutafuta nyumba ya kupanga/kiwanja.

Itafikia wakati biashara nyingi zitakuwa computerised.

Tuamke sasa.
 
kila kitu ni ushindani sio kwasbb kuna insta au Facebook basi watu waache kutengeneza vitu kama hivyo
watu watengeneze ila wawe wabunifu zaidi kumbuka Facebook aliiona WhatsApp kama threat kwake na akaamua kuwafanya partners

kulikua na Skype
akaja imo n.k
wote wanatoa vitu vyenye kuendana

vipi BBM? wangemwacha pekeyake leo tungekuwa na WhatsApp?

cha msingi ni kutumia udhaifu wa aliyekutangulia kwa kuboresh zaidi hata kama umekopi na kupest kutoka kwake

vivyo hivyo utaona ligi ipo kwenye maswala ya antivirus
Nimekupata mkuu, tatizo litabaki kwenye ubunifu kitu ambacho wenda ma IT wetu hawana!!

Ila nnavyoona achilia mbali ubunifu pia marketing ni jambo la msingi sana!!
 
yeah ndo hizo njia nilizokua nasema kwenye marketing wanaanguka hasa kwenye international levels
 
Hivi vitu vinafanyika sema changamoto kujitangaza na kosa kubwa tunashindwa kujifunza kwa wenzetu waliofanikiwa kujitangaza na kujenga brand kitu kama jf max melo hajatumia pesa nyingi sana wakati anaanza lakini naamini kuna njia zimemfanikisha kufika hapa
 
wanaweza ila njia wanazotumia kufanya app zao ziwe maarufu ndipo shida inapo anzia hii inachagizwa pia na watanzania walio wengi kutokupenda kusapoti kazi za nyumbani.

nitakupa mfano mwaka juzi kama sijakosea palitokea kijana wa UDOM alitengeneza kitu kama facebook na watu wakaonekana kuikubali ila mpaka sasa sijui aliishia wapi na siamini kama kuna mtanzania anaetembelea hiyo project ya jamaa.
Sasa si kwa sababu tayari kuna hiyo facebook...
Hakuna kinachotamba zaidi ya ambacho tayari kilikuwepo.
Namaanisha tubuni cha tofauti.
 
Back
Top Bottom