Rasimu ya Katiba Yatelekeza Serikali za Mitaa.

kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,025
494
Katika kupitia kwa undani na kwa urefu nimebaini kuwa Rasimu ya Katiba haijatoa mwelekeo wowote katika mustakabali wa Serikali za Mitaa na uwakilishi wa watu na hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kujisifu na kutamba pasipo uwakilishi na ushirikishwaji wa wananchi katika serikali za Mitaa.Ilo ni pungufu kubwa katika rasimu hii ya katiba. Serikali za Mitaa hata kwenye katiba ya 1977 imeahinishwa na kutambuliwa kisheria na hivyo rasmu ya katiba ya Serikali ya shirikisho lazima pia ijenge msingi wa kuainisha ibara na nafasi ya Serikali za wanannchi ambazo ni serikali za Mitaa.Siyo hiari na kutofikri vizuri kama kutakuwa na mawazo mgando kuwa serikali za Mitaa sheria yake itambulike kwenye katiba ya Jamhuri ya Tanganyika tu wakti kwenye serikali kuu ya shirikisho jambo ilo halijabainishwa.Hapo Waryoba umeteleza nafasi ya serikali za mitaa katika nchi hii ni kubwa japo serikali ya mafisadi na ccm makao makuu wanaona hazina maana.
 
Back
Top Bottom